Monday, July 10, 2017

MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI SIMIYU

Mwenge wa Uhuru 2017 umehitimisha Mbio zake Mkoani Simiyu na kukabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10/07/2017.

Akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Halmashauri zote sita za Mkoa huo katika umbali wa kilometa 780.

Sagini amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Simiyu umeweza kuweka mawe ya msingi, kufungua, kuzindua, kukagua na kuona jumla ya miradi 43 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 8,450,841,622/= ambazo ni fedha kutoka Serikali Kuu, Halmashauri, nguvu za wananchi,sekta binafsi na washirika wa maendeleo.


Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 zimebeba Ujumbe Mkuu “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU”
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Ndg Albert Msovela katika Kijiji cha Kinampanda Wilaya ya Kishapu Mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Dkt.Seif Shekalaghe (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(kulia) kabla ya kuukabidhi katika mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(kulia) akimtakia Kila la Heri Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Ndg Albert Msovela(kushoto)  katika Kuukimbiza Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga mara baada ya makabidhiano.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akiagana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akiagana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu muda mfupi kabla ya makabidhiano ya ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkoa wa Simiyu na Shinyanga.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017,Vatima Yunus Hassan  kutoka Kusini Pemba(kushoto) na Shukran Islam Msuri kutoka Mjini Magharibi wakiagana na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa 2017 Salome Obadia Mwakitalima akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Dkt.Seif Shekalaghe
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017 wakiagana na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu muda mfupi kabla ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika ya Mkoa wa Simiyu na Shinyanga.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!