Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru 2017 Ndg. Amour Hamad Amour ametoa wito kwa wananchi kupenda na
kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Amour ametoa wito huo
wakati alipokuwa akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuweka
jiwe la Msingi Mradi wa kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao Kilimo cha BUSEGA
MAZAO LIMITED katika kijiji cha Mwanangi wilayani Busega.
Amesema wananchi
watakapotumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini watasaidia kuongeza uzalishaji
kutokana na kuwepo kwa soko la uhakika kwa viwanda na hatimaye kuongeza uchumi
wa nchi.
Ameongeza kuwa
wawekezaji wanapaswa kuzalisha bidhaa bora ambazo zitakidhi vigezo vya
kiushindani sawa sawa na zile zinazotoka nje ya nchi ili kupunguza uingizwaji
wa bidhaa za nje na kulifanya Taifa kuongeza pato lake.
“.....bidhaa ambazo
zinazotoka nje zinapoingia hapa ndani zinakuwa na bei ndogo kuliko
zinazozalishwa hapa nchini, ni kwa
sababu bado hatujajipanga kuzalisha kiushindani, sasa tuzalishe bidhaa zenye
ushindani ili kuweza kuua soko la bidhaa ambazo zinatoka nje tuweze kukuza
uchumi wa Taifa letu” alisema.
Aidha, amesema
mwekezaji wa kiwanda cha BUSEGA MAZAO LIMITED atakapoanza uzalishaji atoe kipaumbele cha ajira kwa wananchi wa
wilaya ya Busega na ahakikishe wanafanya kazi katika hali ya usalama na kupewa
haki na maslahi yao kama inavyostahili.
Kiongozi huyo wa Mwenge
wa Uhuru 2017 pia amewataka wakazi wa
Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanazalisha kwa
wingi mazao yote yanayotakiwa katika kiwanda hicho ukiwepo mpunga na mahindi
kwa kuwa kitatoa soko la uhakika na kupelekea ongezeko la pato la mtu mmoja
mmoja.
Akisoma taarifa ya
mradi wa kiwanda hicho,Ndg. Lazaro Japhet kutoka BUSAGA MAZAO LIMITED amesema
Kiwanda hicho kitawasaidia wakulima kupata soko, kuhifadhi na kuongeza mazao
yao.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera amesema Serikali wilayani humo iko tayari
kushirikiana na wawekezaji ambao watakuwa tayari kuwekeza katika wilaya hiyo.
Sambamba na hayo
Ndg.Amour Hamad Amour amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii, kulinda
rasilimali za nchi na kuendelea kupambana na rushwa, dawa za kulevya, malaria
na UKIMWI ili kuweza kufikia Tanzania ya Uchumi wa Kati.
Akizungumza na wananchi
na wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mkula Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa 2017 amesisitiza wanafunzi wa shule za sekondari kuwa na Klabu za
wapinga rushwa, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, malaria na UKIMWI ili
waweze kufikia malengo yao.
Mwenge wa Uhuru ukiwa
Wilayani Busega umepitia jumla ya miradi 9 katika sekta ya Elimu, Afya,
Maji,Utawala Bora, Viwanda na Maendeleo ya jamii, yenye thamani ya zaidi ya
shilingi bilioni 1.5.
|
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(wa tano kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa watumishi katika Kiwanda Cha BUSEGA
MAZAO LIMITED mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho wilayani
Busega |
|
Mkuu
wa Wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkimbiza
Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Salome Mwakitalima tayari kwa kuanza kuukimbiza katika
Wilaya yake.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akikagua moja ya
vyumba vinne vya madarasa vilivyofunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Shule ya
Sekondari Mkula wilyani Busega.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour
akipanda mti katika Shule ya Sekondari Mkula Wilayani Busega.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour
akizindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Mkula Wilayani
Busega
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(kulia) na Mkuu wa
Wilaya wakishangilia baada ya Klabu ya Wapinga rushwa kuzinduliwa katika Shule
ya Sekondari Mkula.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amourakiangalia moja ya
miundombinu ya maji katika Mradi wa Maji wa Lukungu kabla ya kufungua mradi
ambao utaanza kwa kuwahudumia takribani wananchi 4022.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akifungua mradi wa
Maji wa Lukungu wilayani Busega ambao utaanza kwa kuwahudumia wananchi 4022 na
kufikia mwaka 2030 utawahumia wananchi 11,500.
Lazaro
Japhet akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamni ya azaoya kilimo cha BUSEGA MAZAO LIMITED kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(hayupo pichani) kabla ya
kuwekwa kwa jiwe la msingi la kiwanda hicho.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akimtwisha ndoo ya
maji Mkimbiza Mwenge Kitaifa Salome Mwakitalima mara baada ya kufungua mradi wa
Maji wa Lukungu wilayani Busega.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akikata utepe
kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kusindika nafaka cha BUSEGA
MAZAO LIMITED wilayani Busega.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la
Msingi kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao BUSEGA MAZAO LIMITED wilayani
Busega.
Baadhi ya viongozi na
wananchi wilaya ya Busega wakimfuatilia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(hayupo pichani) akikagua Kiwanda
cha BUSEGA MAZAO LIMITED kabla kuweka jiwe la msingi.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwanangi kabla ya
kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017
,Ndg.Amour Hamad Amour kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 baada ya
kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha BUSEGA MAZAO LIMITED.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na
kikundi cha wanawake wajasiriamali wakionesha bidhaa mbalimbali
wanazotengeneza.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na
kikundi cha wanawake wajasiriamali wakionesha bidhaa mbalimbali
wanazotengeneza.
|
0 comments:
Post a Comment