Sunday, July 9, 2017

WAZAWA WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE MAENEO YA UWEKEZAJI

Halmashauri ya wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu imetakiwa kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wazawa pindi wanapogawa maeneo ya uwekezaji wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira na uchumi ndani na nje ya Mkoa, ambapo jumla ya ekari 1000 zimeshatengwa kwa ajili yauwekezaji.

 Wito huo umetolewa leo na Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour wakati wa kukagua na kukabidhi hati ya eneo la uwekezaji wa viwanda kwa Mkurugenzi wa  Halmashauri  lililopo katika kata ya Nyalikungu Wilaya ya Maswa
 .
Kiongozi huyo amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Maswa kwa kutekeleza agizo la Serikali la kutenga eneo la uwekezaji na kusema kuwa ni vema wazawa wakapewa kipaumbele kwa kupatiwa maeneo hayo, ili waanze ujenzi wa viwanda mbalimbali vitakavyokuza ajira, kuchangia pato la Halmashauri, pato la mwananchi mmoja mmoja  na uchumi wa Nchi kwa ujumla.

 "Nashauri Halmashauri kutoa kipaumbele kwa wazawa kwa kuwapatia maeneo hayo ya viwanda ili wafanye shughuli za kimaendeleo ambazo zitagusa moja kwa moja maisha ya Wananchi wa Wilaya ya Maswa, mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja suala la ajira kwa vijana ....Alisema.
Pamoja na kuwapa kipaumbele wazawa Ndg. Amour ameutaka uongozi wa Wilaya ya Maswa kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wageni na kutoa maeneo kwa wote watakaokidhi masharti ya kuwekeza na kujenga viwanda  kwa mujibu wa sheria za nchi.

Aidha Amour ameishauri Halmashauri hiyo kuanzishwa viwanda ambavyo vitayaongezea thamani mazao na kutoa bidhaa zitakazoingia sokoni moja kwa moja,  badala ya kung'ang'ana viwanda vinavyoandaa malighafi zitakazotumiwa na viwanda vilivyo nje ya nchi; kama ilivyo kwa viwana vingi vya pamba huandaa pamba inayoenda kuzalisha nguo nje ya nchi.

 Pia amefurahishwa na kuupongeza uongozi  mzima wa Halmashauri hiyo kwa jitihada wanazozifanya za kuanzisha viwanda vinavyoiongezea halmashauri mapato kikiwemo kiwanda cha Chaki, sambamba na kuhakikisha wanaendana na kasi ya Mhe Rais ya kuwa na Tanzania ya viwanda .

Naye Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa John Nkoko amesema kuwa tayari wameshatenga ekari 1000 kwa ajiri ya eneo la viwanda na tayari eneo la ekari 315.64 limeshaandaliwa michoro ya mipango miji.
Nkoko amesema kuwa lengo la Halmashauri yao kutenga eneo hilo ni kuhakikisha wanatengeneza fursa ya ajira kwa wananchi wao pamoja na kukuza uchumi wao wa ndani na nje ya Mkoa .

 Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Dk Fredrick Sagamiko alisema Wilaya yake itahakikisha inapambana kuwa na uchumi wa kati kwa kuanzisha viwanda mbalimbali ambapo mpaka sasa wameanza ujenzi mpya wa kiwanda kikubwa cha chaki ambacho kitakuwa cha kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na teknolojia mpya.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Maswa umeweka mawe ya mingi, kuzindua, kufungua na kuona miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Viwanda, Afya, Elimu, Kilimo, Utawala Bora,Maendeleo ya Jamii,Ardhi Maliasili na Mazingira.

Akitoa Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika maeneo mbalimbali ya miradi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amewaasa wananchi kufanya kazi kwa bidii, kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za nchi pamoja na kupambana na rushwa, dawa za kulevya, malaria na UKIMWI.  

Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Shughuli za Uzalishaji katika Kiwanda cha Kusaga na Kuhifadhi Nafaka kilichopo Malampaka Wilayani Maswa, Epifania Labia.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Busega ,Mhe.Tano Mwera katika Kijiji cha Malita wilayani Maswa..
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akimkaribisha Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour tayari kwa kuanza Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilayani humo.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akifungua Mradi wa Bwalo la Chakula katika Shule ya Sekondari Malampaka.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wa Kata ya Kadoto mara baada ya kufungua nyumba ya Watumishi wa Zahanati ya Kadoto(inayoonekana pichani)
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akipata maelezo juu ya mradi wa Kitalu cha Miti ya Kivuli na Matunda unaosimamiwa na Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour juu ya shughuli za utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazofanywa na kikundi cha vijana.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akipata maelezo juu ya mradi wa kiwanda cha uzalishaji chaki kutoka kwa Kiongozi wa Kikundi cha Maswa Family.

Baadhi ya Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Maswa wakishuhudia Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour (hayupo pichani) akikagua eneo llililotengwa maalum kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda lenye ukubwa wa ekari 1000.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akifungua nyumba ya kuishi watumishi wa Zahanati ya Kadoto ilyopo Kata ya Kadoto wilayani Maswa.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi mara baada ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bangi zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Maswa.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha Wanawake wajasiriamali wilayani Maswa.

Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Klabu ya Wapnga Rushwa katika Shule ya SekondariMalampaka






0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!