Wanafunzi wa shule za sekondari wilayani
Bariadi mkoani Simiyu wamehimizwa kusoma masomo ya sayansi ili kuendana na azma
ya Serikali ya awamu ya tano ya Uchumi wa Viwanda kama inavyoelezwa pia katika
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour wakati wa uzinduzi wa miradi
mbalimbali ya maendeleo wilayani BARIADI.
Amour amesema Serikali imejenga
maabara na kuweka vifaa katika shule
mbalimbali za sekondari kwa lengo la kuwezesha wanafunzi kujifunza masomo ya
sayansi kwa vitendo ili kuwaandaa kuwa wataalam katika maeneo tofauti.
Amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na
kuzitumia vizuri maabara zilizopo ili wapate ujuzi wa nadharia na vitendo
utakaowaandaa kuwa wabobezi kwenye maeneo mbalimbali yanayohitaji utalaam wa
kisayansi.
“, nahimiza huduma nzuri za maabara vijana
hawa waweze kusoma masomo ya kemia, fizikia, bailojia na hisabati ili waende
sawa na Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu ya “Shiriki katika Kukuza
Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu” wakashike nafasi mbalimbali wawe
wakemia, wahandisi katika viwanda, wawe madaktari na nafasi nyingine nyingi" amesema Amour
Akizungumzia mapambano dhidi ya dawa za
kulevya amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kuziba mianya yote
na kutokomeza shughuli za uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya na wasisite
kutoa taarifa katika vyombo vya dola wanapobaini watu wanaofanya shughuli hizo
ili wachukuliwe hatua..
Aidha, akizungumza na wananchi katika
maeneo mbalimbali ambayo Mwenge wa Uhuru umeweka mawe ya msingi, kufungua na
kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo, Ndg.Amour amewapongeza na kuwataka wananchi
kuendelea kuchangia miradi hiyo na kutokubaliana na viongozi wanaowashawishi
kuacha kuchangia maendeleo yao.
“ Kila mradi tuliopita taarifa inaonesha
kuna nguvu ya wananchi, nawapongeza sana kwa kushirikiana na Serikali kutekeleza
miradi ya elimu, afya, maji na mingine mingi,nawasihi msikubaliane na watu
wanaowataka kutochangia miradi ya maendeleo” amesema
Mara baada ya kuweka mawe ya msingi, kuzindua
na kufungua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya BARIADI Mwenge wa
Uhuru tarehe 08/07/2017 utakimbizwa wilayani BUSEGA.
|
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akicheza pamoja na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkololo baada ya Mwenge wa Uhuru kufika katika
Shule hiyo kwa ajili ya kuzindua klabu ya wapinga rushwa, klabu ya kupambana na
dawa za kulevya na kuona mradi wa hifadhi ya mazingira
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Abdallah Malela akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi Mhe.Festo Kiswaga Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuupokea kutoka kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji(hayupo pichani)
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akikagua
na kuona mraidi wa hifadhi ya mazingira katika Shule ya sekondari Nkololo
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akikagua moja ya
vyumba vitatu vya madara vilivyofunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Shule ya
Msingi Nkololo “B” wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akisalimiana na
baaadhi ya watalaam wa Afya mara baada ya kufungua Kituo cha Ushauri, upimaji
na matibabu(CTC)kwa watu wenye VVU katika Kituo cha Afya cha Songambele wilaya
ya Bariadi, Mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akimkabidhi cheti
mmoja wa wanachama wa Klabu ya kupambana na dawa za kulevya katika Shule ya
Sekondari Nkololo mara baada ya kuzindua klabu hiyo.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akimkabidhi cheti cha
Utunzaji wa Mazingira Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkololo mara baada ya
kutembelea na kuona mrai huo.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akiangalia baadhi ya
bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kikundi cha vijana kutoka Kata ya Dutwa
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na wakazi
wa Kijiji cha Nkololo mara baada ya kuweka jiwe la msingi kisima kirefu cha
maji kijijini hapo.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akitoa ujumbe wa
Mwenge kwa wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Nkololo pamoja na wananchi wa Nkololo mara baada kuzindua na kuona
miradi mbalimbali shuleni hapo.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la
msingi katika Mradi wa Maji wa Kisima kirefu katika kijiji cha Nkololo ilaya ya
Baraidi, Mkoani Simiyu.
|
0 comments:
Post a Comment