Jumla
ya Vijiji 347 Mkoani Simiyu vinatarajia kupata Umeme kupitia Mradi wa Umeme
Vijijini (REA) awamu ya Tatu ambao utatekelezwa katika kipindi cha miezi 24
kuanzia mwezi Julai 2017.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani wakati wa
Uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu na utambulisho wa
Mkandarasi wa mradi katika Kijiji cha Nangale, Kata ya Ndolelezi Wilaya ya Itilima
Mkoani Simiyu.
“Mradi wa REA awamu ya tatu utapeleka
Umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Simiyu hilo la kwanza, pili mradi huu utapeleka
Umeme katika vitongoji vyote hata vijiji ambavyo vilipelekewa Umeme lakini baadhi
ya vitongoji vyake bado havina, katika awamu hii navyo vinapelekewa” amesema
Kalemani.
Ameongeza kuwa Umeme wa REA awamu
ya tatu pamoja na kuwanufaisha wananchi katika makazi yao kwenye vijiji vyote 347
vilivyosalia pia utapelekwa katika Taasisi za Umma zikiwepo shule, vituo vya
kutolea huduma za afya, visima na mitambo ya miradi ya maji pamoja na nyumba za
ibada( makanisa na misikiti).
Aidha, Dkt.Kalemani amewataka
wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuutumia umeme huo kibiashara hususani katika
shughuli za uzalishaji ambazo zitawaongezea kipato badala ya kuutumia kwa ajili
ya kuwasha taa majumbani tu.
Ameupongeza uongozi wa Mkoa wa
Simyu kwa kasi nzuri ya utekelezaji wa Sera
ya Viwanda ambapo amebainisha kuwa utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)
awamu ya Tatu mkoani humo utasaidia kuwezesha shughuli za viwanda kufanyika
vizuri hali itakayowawezesha wananchi kukuza uchumi kwa kuwa mazao yao
yataongezewa thamani kupitia viwanda hivyo.
Wakati huo huo Dkt.Kalemani
amesema Serikali ina mkakati wa kujenga vituo viwili vya kupozea umeme Mkoani
Simiyu, ambapo kimoja kitajengwa Mjini Bariadi na kingine katika Mji wa Lalago
wilayani Maswa na kuwahakikishia wananchi kuwa mkoa huo utapata umeme wa kutosha
ambao utatumika pia katika viwanda.
Akimkabidhi Mkandarasi wa Mradi
wa REA Awamu ya Tatu ambaye ni Kampuni ya JV White City International kwa
Wananchi wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Kalemani amemtaka kuhakisha kuwa anatekeleza mradi ndani ya muda uliopangwa (miezi 24),
akiwatumia wakandarasi wasaidizi wenye sifa kutoka ndani ya mkoa na kuwapa
ujira wao kama inavyotakiwa pamoja na kununua vifaa vyote zikiwemo nguzo na
transifoma hapa nchini.
Amemtaka Meneja wa TANESCO Mkoa
wa Simiyu, Mhandisi Rehema Mashinji kusimamia na kuhakikisha kuwa wakandarasi
watakaowaunganishia wananchi Umeme ni wale walioidhinishwa na shirika hilo ili
kuepuka Vishoka ambao watawaongezea wananchi gharama zisizo za lazima.
Amesema Serikali ina mpango wa
kujenga Ofisi za TANESCO kila Wilaya na kuweka vituo vya kuhudumia wateja
katika kila kata na tarafa ambapo yataanzishwa madawati ya huduma kwa wateja.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameomba Shirika la Umeme TANESCO kuona namna ya kuweka nguvu katika Mkoa huo
ili ujitosheleze kwa umeme wa uhakika kuwezesha utekelezaji wa miradi ya
viwanda inayoendelea kutekelezwa chini ya Kauli Mbiu ya Mkoa ya “Wilaya Moja Bidhaa
Moja Kiwanda Kimoja”
Mtaka ameongeza kuwa Mkoa huo umejipanga
kufanya mapinduzi kupitia teknolojia ambapo utatengeneza mpango mkakati wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT Strategy),kujenga ICT Hub ya mkoa na vituo vya mawasiliano katika
baadhi ya shule, ili wanafunzi wa madarasa ya mitihani waweze kupata unafuu wa kufundishwa
kupitia teknolojia hususani kwenye masomo ya sayansi, hivyo akasisitiza umeme
kupelekwa katika shule na Taasisi nyingine za Umma.
Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa
wa Simiyu kupitia CCM, Mhe.Leah Komanya ametoa Rai kwa TANESCO kuhakikisha
wanatoa elimu kwa wananchi ili wajue taratibu zote za kuunganishiwa umeme ikiwa
ni pamoja kufahamu gharama ambayo ni shilingi elfu 27,000/= ili wasidanganywe
na kutumia gharama kubwa kinyume na mpango wa Serikali.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi
wa mradi huo Mkazi wa Kijiji cha Nangale Bw.Mathias Mabula Mageni ameishukuru
Serikali kuwafikishia umeme kupitia REA ambapo amesema utawasaidia katika
kukuza uchumi kwa kuwa watautumia katika shughuli mbalimbali zitakazowaingizia
kipato kama vile kuchomelea vyuma, kuanzisha mashine za kusaga na kukoboa
nafaka, kuanzisha saluni za kike na za kiume pamoja na viwanda vidogo.
Mradi wa Umeme Vijijini (REA)
Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu unatekelezwa na Mkandarasi JV White City International
Contractors ambalo ni Kampuni ya
Kitanzania kwa kushirikiana na Guangdong Jianneng Electronic Power Engineering Co.
Ltd.
|
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani akizindua Mradi wa Umeme Vijijini
(REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu katika Kijiji cha Nangale wilayani Itilima (kushoto)
Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani (mwenye suti nyeusi katikati) akikata
utepe kabla ya kuzindua Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu Mkoani
Simiyu katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani akizungumza na wannachi wa Wilaya ya
Itilima wakati wa Uzinduzi waMradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe.Medard Kalemani akiwaonesha wananchi Kifaa kiitwacho
UMETA(Umeme Tayari) ambacho hutumika kuleta nishati ya umeme katika nyumba
ambazo haziwezi husukwa nyaya wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini
(REA) Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu katika
Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu akitoa salamu za Mkoa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme
Vijijini (REA)Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima Mkoani humo.
Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Simiyu kupitia CCM,
Mhe.Esther Midimu akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima wakati wa
uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu katika Kijiji cha
Nangale wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Mbunge
wa Itilima, Mhe.Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima
wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha
Nangale wilayani Itilima.
Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe.Leah Komanya akizungumza na wananchi wa
Wilaya ya Itilima wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya
Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika
Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani( wa tatu kulia) akicheza wimbo
maalum wa Kisukuma pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu wakati wa uzinduzi wa Mradi
wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji
cha Nangale wilaya ya Itilima.
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt. Medard Kalemani( wa tatu kushoto) akiteta jambo
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Dkt.Titus
Kamani wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani
Simiyu katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani( wa pili kulia) pamoja na baadhi
ya viongozi wa mkoa wa Simiyu wakicheza kuelekea kuwatuza wasanii waliokuwa
wakitoa burudani (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini
(REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya
ya Itilima.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mh.Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini
(REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya
ya Itilima.
Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Simiyu, Dkt.Titus Kamani akizungumza na wananchi wa Itilima wakati
wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu
uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akiteta jambo na Mbunge wa Itilima Mhe.Njalu Silanga wakati
wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofamyika
katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima, (kushoto) ni Mbunge wa Maswa
Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki.
Mmoja
wa Wazee 10 waliopewa kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA katika Kata ya Ndolelezi
Wilayani Itilima na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani
akitoa shukrani wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya
Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
Baadhi ya
wananchi wa Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Mhe.Dkt.Medard Kalemani(hayupo pichani) wakati wa wakati wa uzinduzi wa Mradi
wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu katika Kijiji cha Nangale wilaya
ya Itilima.
Kikundi
cha Kwaya kutoka wilayani Itilima wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu katika
Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
Msanii Elizabeth
Maliganya (mwenye kipaza sauti katikati) akicheza wimbo wa Kisukuma na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani(kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali
wa Mkoa wa Simiyu kufurahia uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya
Tatu Mkoani humo katika kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.
|
0 comments:
Post a Comment