Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa huo kwa Kiongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.Amour Hamad Amour katika kijiji cha Bukundi wilaya ya Meatu ukitokea katika mkoa Singida.
Mtaka amesema kati ya fedha hizo shilingi 680,285,524 zinatokana na Nguvu za wananchi ,Serikali Kuu shilingi 4,524,439,388, Halmashauri Shilingi 352,000,875, Washirika wa Maendeleo Shilingi 635,559,935 na Sekta binafsi Shilingi 2,258,555,900/=
Amesema Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13,
kutembelea
na kuona miradi 16 katika sekta ya
Elimu,Afya,Maji,Vijana na wanawake,Miundombinu ya barabara, Sekta ya Viwanda,
Maliasili, Kilimo, Ushirikana Utawala bora.
Aidha, Mtaka amesema katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umeweza kujipambanua katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”

“Katika utekelezaji huu mkoa umefanikiwa kuanzisha kiwanda cha Chaki wilayani Maswa, Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu na Upembuzi yakinifu unaendelea kwa miradi mingine ambayo pia itatekelezwa katika Halmashauri zetu nyingine nne”
Ameongeza katika miradi kuwa kukamilika kwa viwanda hivyo kutasaidia
kutoa ajira kwa vijana wa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kutokana na kuwa malighafi zinazotumika na
zitakazotumika katika viwanda hivyo zinazalishwa hapa nchini.
Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , Ndg. Amour Hamad Amour akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu mbali na kuipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za wananchi wake hususani wanawake wajawazito pia alitaka mradi huo utunzwe na uthaminiwe.
“Mradi huu ni mzuri na mimi nimefurahi kuona naanza kuzindua miongoni mwa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa akinamama wajawazito hivyo basi nitoe wito kwa wanawake kutumia vizuri jengo hili badala ya kujifungulia majumbani hali inayoweza kuhatarisha afya zenu, vile vile mradi huu utunzwe na kuthaminiwa ili uendelee kutusaidia,”alisema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa wilaya ya Meatu wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza miradi ambayo imewasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika huduma za jamii ikiwemo maji na afya kwa kuwa itawasaidia kupata huduma hizo karibu na kwa ubora unaotakiwa.
“Wakina mama wengi walikuwa wanapoteza maisha kwa
kujifungulia njiani , kwa kweli naishukuru sana serikali maana kuwepo kwa jengo
la upasuaji lililozinduliwa leo na mwenge wa uhuru,kutatusaidia sana ” amesema
Tatu Athumani mkazi wa Bukundi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg.
Amour Hamad Amour akimtwisha mkazi wa Kijiji cha Bukundi ndoo ya maji mara
baada ya kufungua mradi wa maji katika kijiji hicho leo.
Congratulations viongozi wote kwa miradi ya maendeleo inayogusa wananchi wetu
ReplyDelete