Mkoa wa Simiyu umejipanga kurasimisha kazi za
sanaa, utamaduni na baadhi ya michezo ili kutengeneza ajira kwa wananchi
ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu Tamasha la “Simiyu
Jambo Festival” litakalohusisha mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za
asili ambalo litafanyika Agosti 06, 2017 Mjini Bariadi.
Amesema Mkoa wake umekusudia kuandaa utaratibu wa kushirikiana
na wadau wengine wakiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Sanaa Bagamoyo
na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuona namna ambayo kazi za
sanaa,utamaduni na michezo zinazofanyika katika mkoa wa Simiyu zinaweza
kufanywa kibiashara na zikawanufaisha wananchi.
Ameongeza kuwa vikundi vya sanaa na utamaduni vya Mkoa wa
Simiyu vitapewa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kitaalam katika viwango
vinavyotakiwa, ili kazi ziweze kuuzika ndani na nje ya mkoa hususani kipindi
ambacho watalii wengi wanakuja hapa nchini kwa kuwa mkoa huo unapakana na mikoa
yenye hoteli nyingi za kitalii.
“Simiyu
ni mkoa unaopakana na mikoa yenye Hoteli za kitalii, tungehitaji tufike mahali
ambapo kazi za utamaduni na sanaa ndani ya mkoa wetu zinafanywa kibiashara;wakati
watalii wanapotembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kwenda kwenye hoteli za kitalii wasiishie kupiga picha,
tungehitahi vikundi vyetu vya sanaa na utamaduni viuze kazi zao huko” amesema
Mtaka
.Aidha, Mtaka amefafanua kuwa katika kufanikisha hayo Mkoa umeanza na mchezo wa Mbio za baiskeli kupitia Mashindano yatakayofanyika Agosti 06, mwaka huu ambapo Mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson.
.Aidha, Mtaka amefafanua kuwa katika kufanikisha hayo Mkoa umeanza na mchezo wa Mbio za baiskeli kupitia Mashindano yatakayofanyika Agosti 06, mwaka huu ambapo Mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson.
Amesema vijana wengi
wa Mkoa huo wanafanya vizuri katika mchezo huo hivyo watafanyiwa utaratibu wa
kupewa mafunzo ya kuwaimarisha zaidi katika mchezo huo, ili Mkoa ufikie hatua
ya kutoa wawakilishi katika nchi kwenye mashindano makubwa ya mbio za baiskeli
kama ya Jumuiya ya Madola na Olimpiki.
“Tuko kwenye kutambua
vipaji vya watu na tunajaribu kuona kila mwananchi aliyeko ndani ya mkoa wa
Simiyu kile ambacho amejaliwa na Mwenyezi Mungu kinamsaidia kujipatia kipato
chake.Tunafanya yote haya kwenye Mkoa kwa kuwa tunaamini Kipaji cha mtu ni
biashara na kipaji ni ajira” amesema Mtaka.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa Chama cha baiskeli Mkoa wa Simiyu Joseph Paul amesema kuwa chama
chake kinaiwashukuru kampuni ya Jambo
Food Product kwa kudhamini mashindano
hayo ya Mbio za baiskeli ambayo yatahusisha makundi matatu; kilometa 200 kwa
wanaume, Kilometa 80 wanawake na Kilometa Tano kwa watu wenye Ulemavu.
Paul amesisitiza kuwa chama chake kimejipanga
vilivyo na zaidi ya washiriki 150 wamethibitisha kushiriki mashindano
hayo kutoka katika mikoa ya Simiyu,Geita,Mwanza, Shinyanga na Arusha
Naye Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Product Anthony Paul,amesema Kampuni hiyo ambayo
ni wadhamini wakuu wa Mashindano hayo wamejipanga
kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo Pikipiki itakayotolewa kwa mshindi wa Kwanza
(wanaume) na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 8 zitashindaniwa.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto)akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani)ofisini kwake kuhusu Simiyu Jambo Festival
itakayohusisha mashindano ya Mbio za Baiskeli na burudani ya ngoma za asili
yatakayofanyika Agosti 06 mwaka huu mjini Bariadi, (kushoto ) Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Joseph Paul.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Product Anthony
Paul (wa pili kushoto)akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
zawadi zitakazotolewa na kamunu hiyo kwa washindi wa mashindano ya baiskeli
yatakayofanyika Agosti 06, 2017 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka (mwenye pikipiki) akiwa katika picha ya pamoja na
baadh ya washiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kutoka mkoani humo ambayo
yatafanyika Agosti 06, 2017 Mjini Bariadi.
Baadhi ya
Waandishi wa Habari na wadau wa michezo wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Simiyu
akizungumza na waandishi wa Habari juu ya “Simiyu Jambo Festival” tamasha
litakalohusisha Mashindano ya Baiskeli na burudani ya wagika , wagalu na ngoma
za asili Agosti 06, 2017.
Manju wa
Kundi la Wagika, Sadam Chulichuli(katikati) akiwaeleza waandishi wa habari juu ya ushiriki
wao katika Tamasha la “Simiyu Jambo Festival” litakalohusisha mashindano ya
Baiskeli na Burudani kutoka kwa wagika, wagalu na ngoma nyingine za asili.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto)akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani)ofisini kwake kuhusu Simiyu Jambo Festival
itakayohusisha mashindano ya Mbio za Baiskeli na burudani ya ngoma za asili
yatakayofanyika Agosti 06 mwaka huu mjini Bariadi
0 comments:
Post a Comment