Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour
Hamad Amour amewataka watalaam wa afya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya
dawa kwa wananchi ili kuepuka madhara mbalimbali kiafya.
Ndg.Amour ameyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa Duka la Dawa katika Hospitali ya Somanda Mjini
Bariadi.
Amesema baadhi ya watu
wamekuwa wakitumia dawa kwa mazoea pasipo kufuata maelekezo ya madaktari na
wauguzi hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
“
Wapo watu wanatumia dawa kiholela na kuathiri kinga ya mwili, inafika kipindi
dawa zinawaathiri moja kwa moja hata wanapotakiwa kuzitumia kutibu maradhi
waliyonayo haziwasaidii, wapeni elimu wananchi watumie dawa kulingana na
maelekezo ya wataalam”
Aidha, amewataka
madaktari na wauguzi kutoa huduma stahiki kwa wananchi kupitia duka hilo kwa kuwauzia
dawa kwa bei elekezi na kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote, ili wanapoandikiwa dawa na kuikosa hospitali,
vituo vya afya na zahanati wazipate katika duka hilo.
Kwa upande wake mmoja
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg.Fredrick Ndahani ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto kwa jitihada za kuhakikisha kuwa kila
Hospitali ya Mkoa na Wilaya inakuwa na Duka la dawa la Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD), ambayo yatawawezesha
wananchi kupata dawa zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu.
Sanjali na hilo Ndahani ametoa wito kwa
wanachi wote kujenga utamaduni wa kuangalia tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa(expire
date) kabla ya kutumia ili wasitumie dawa zilizokwisha muda wake.
Akiwasilisha taarifa ya
mradi wa duka la dawa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mganga
mkuu wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Dkt.Akilimali Mponzemenya amesema lengo la
kujenga duka hilo ni kuwezesha
upatikanaji wa dawa zilizothibitishwa na Mamlaka ya Dawa kwa urahisi na kwa bei
nafuu zaidi kwa wananchi.
Katika hatua nyingine
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na wananchi wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika maeneo tofauti, ametoa wito kwa wananchi
wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi bidii na kulinda rasilimali za nchi hii.
Mwenge wa Uhuru unaendele
na Mbio zake Mkoani na leo upo katika Halmashauri ya Mji Bariadi, ambapo umeweka
mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika
sekta ya Afya, Elimu , Maji, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii na jumla ya miradi 6
imepitiwa pamoja na klabu ya wapinga rushwa kufunguliwa katika Shule ya
Sekondari Bariadi.
0 comments:
Post a Comment