Na Stella Kalinga
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein
amewasili Mjini Bariadi jioni hii kwa ajili ya Maadhimisho ya kilele cha mbio
za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana
yatakayofanyika kitaifa kesho tarehe 14 Oktoba, 2016 Mjini, Bariadi mkoani
hapa.
Mhe.
Rais wa Zanzibar ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru, Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana, tukio ambalo
ni la kihistoria kwa mkoa wa Simiyu.
Rais
Shein amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo viongozi wa Chama
na Serikali pamoja na wananchi wa Mjini Bariadi.
 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipewa heshima na vijana wa Skauti Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi.
 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa amevalishwa skafu na vijana wa Skauti Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi, ishara ya kumkaribisha, (kushoto) Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka.
 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi, watumishi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi.
 |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi, watumishi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi.
|
|
|
|
0 comments:
Post a Comment