Tuesday, April 11, 2017

WANUFAIKA WA TASAF WATAKIWA KUBUNI MIRADI KUJIONGEZEA KIPATO

Wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III wametakiwa kubuni miradi midogo midogo kwa kutumia fedha wanazopata ili kujiongezea kipato.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini wakati wa ziara yake wilayani Itilima ya kukagua visima vya maji ambavyo ni miongoni mwa miradi  ya kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.

Sagini amesema wanufaika wa TASAF ikiwa ni pamoja na waliopata ajira za muda katika uchimbaji wa Visima na kulipwa ujira  kidogo watumie fedha hizo kujikimu na kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo ya biashara ndogo ndogo na ufugaji wa kuku, bata, mbuzi na kondoo.

“ Mradi huu hautadumu milele nawashauri katika kidogo mnachokipata mkitumie vizuri,  anzisheni miradi midogo midogo itakayowasaidia kuboresha kipato katika kaya zenu, wenye uwezo wa kufuga wafuge, wenye uwezo wa kufanya biashara ndogo ndogo wafanye” alisema Sagini. 

Mwenyekiti wa kijiji cha Nanga Dismas Lyang’ombe amesema baadhi ya wanufaika wa mradi wa TASAF waliohusika katika ujenzi wa visima vinne vilivyojengwa na Serikali kupitia Mradi wa TASAF kwa kushirikiana na wananchi na kupewa ujira wa shilingi 2300 kwa siku, wameonesha mabadiliko katika kaya zao tofauti na ilivyokuwa awali, ikiwa ni pamoja na kufuga kuku, mbuzi na kuezeka nyumba zao kwa bati.

Aidha,  Lyang’ombe ameishukuru Serikali kwa kujenga visima hivyo kwa kuwa vimewasaidia wananchi wake kupata huduma ya maji katika umbali mfupi

Kwa upande wao wananchi wa vijiji vya Nguno, Nanga na Laini B vyote vya Wilaya ya Itilima alivyovitembelea Katibu Tawala Mkoa Simiyu, wameomba Serikali hiyo kutibu maji yanayopatikana katika visima hivyo ili wapate maji safi na salama.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Ndg. Mariano Mwanyigu amesema  Halmashauri yake itaandaa utaratibu mzuri wa kitaalam  kupitia wahandisi wa maji kuhakikisha maji yanatibiwa na wananchi wanapata maji safi na salama.

 Miradi ya ajira za muda kwa wanufaika wa Mradi wa TASAF  hutekelezwa katika kipindi kigumu kiuchumi ili kuwasiadia wanufaika hao na katika wilaya ya Itilima imeanza kutekelezwa mwezi Disemba 2016 hadi Machi   2017.

Jumla ya miradi 161 imeibuliwa katika vijiji 65 vilivyo kwenye mpamgo, katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wa miradi ya kutoa ujira ni visima 161 vinavyotakiwa kukamilishwa  na visima 95 vimekamilika vinatoa maji, 66 viko katika hatua ya kufunikwa na vinatoa maji.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(wa tatu kulia) akitoa maelekezo ya kuboresha eneo la kisima kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nanga, Juma Maiga (kushoto) wakati wa ziara yake wilayani Itilima,  ya kukagua miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III
.Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(wa pili kushoto) akishuhudia mkazi wa kijiji cha Nguno wilayani Itilima akichota maji katika Kisima kilichojengwa na Serikali kupitia mradi wa TASAF na  wananchi (wanafaika wa mradi huo)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(wa tatu kulia) akitoa maelekezo ya kuboresha ujenzi wa  kisima kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nguno (hayupo pichani) wakati wa ziara yake wilayani Itilima,  ya kukagua miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Mratibu wa TASAF  Mkoa wa Simiyu, Ndg. Nyasilu Ndulu (wa pili kulia) akionesha eneo linalopaswa kuboreshwa  katika  ujenzi wa  kisima Kijiji cha Nguno Itilima,  kinachojengwa chini ya miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nguno wakati wa ziara yake wilayani Itilima,  aliyoifanya kwa lengo la  kukagua visima vilivyo katika miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  wakazi wa kijiji cha Nguno wakati wa ziara yake wilayani Itilima,  aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsilikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(hayupo pichani) alipozungumza nao baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III, (kushoto)n Mkurufgenzi mtandaji Mariano Mwanyigu(Katikati) Mkuu wa Wilaya, Mhe. Benson Kilangi
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsilikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini(hayupo pichani) alipozungumza nao baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo aliyoifanya kwa lengo la kukagua visima vilivyo katika miradi  ya ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF III.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!