Friday, December 29, 2017

NAIBU WAZIRI WA MADINI AFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU

Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Nyongo amefanya ziara yake ya kikazi leo Mkoani Simiyu.

Katika ziara hiyo Mhe.Nyongo amekutana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na watumishi wa Ofisi ya Madini ya Mkoa huo, lengo likiwa ni kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu usimamizi wa Sekta ya madini katika Mkoa wa Simiyu, ili kuleta tija kwa wanachi na Taifa kwa ujumla.

Mhe.Nyongo pia amepata fursa ya kutembelea na kuona Jengo la sasa la Ofisi ya Afisa Madini Mkazi na kuahidi kuwa Wizara yake ina mpango wa kujenga jengo la jipya la Ofisi hiyo.

Aidha, amesema atahakikisha tafiti juu ya ubora wa chumvi inayozalishwa wilaya ya Meatu zinafanyika ili kuweza kujua ikiwa inakidhi ubora unaotakiwa kwa matumizi ya binadamu iweze kuongezewa thamani na kutangazwa.

“Tutahakikisha tafiti hizi zinafanyika na mpango wetu ni kwamba zifanyike kwa haraka ili chumvi ya Meatu tuweze kuitangaza, kwa sababu Simiyu tumeshaitangaza vizuri kupitia Chaki sasa tuitangaze tena kwa chumvi yetu” amesisitiza.

Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, Fabian Mshai amesema wachimbaji wa chumvi wako tayari na wanaomba Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kufanya utafiti kwenye chumvi hiyo  na kushauri namna bora ya kufanya chumvi hiyo iwe bora, ili iweze kupata soko zuri ndani na nje ya nchi.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema ni vema Watendaji wa Ofisi ya Madini Mkoa wakasaidiwa kwa kuwezeshwa vitendea kazi pamoja na mahitaji mengine ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kuwafikia wachimbaji kwenye maeneo yanayochimbwa madini na Serikali iweze ipate stahili yake.


Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu (baadhi hawapo pichani) mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku moja (kushoto) Katibu Tawala Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini(katikati) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.
 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo aliyoifanya mkoani humo leo.


 Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Fabian Mshai akiwasilisha taarifa ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo. 

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watendaji katika Wizara ya Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo wakati Wizara yake Mkoani Simiyu leo.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo akiagana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kukamilisha ziara yake Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Simiyu alipokuwa Mkoani humo leo kwa ziara ya siku moja

 Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo wakati wa Ziara yake mkoani humo.
  

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!