Saturday, December 5, 2020

ASKOFU LEKUNDAYO AONGOZA MAOMBI KUMSHUKURU MUNGU KULIVUSHA TAIFA KATIKA JANGA LA CORONA, UCHAGUZI MKUU

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo ameongoza viongozi na mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi la Mtaa wa Ntuzu lililopo Bariadi mjini ambapo  Waumini wa kanisa hilo pamoja na wengine kutoka mkoa wa Mwanza na Mara wamewakilisha waumini wengine hapa nchini, ambapo ibada hiyo imehudhuriwa pia na viogozi wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

“Nilikuwa naangalia takwimu za hali ya janga la Corona ilivyo duniani leo asubuhi (Desemba 05, 2020) hadi sasa zinaonesha watu 66,281,000 wamepatwa na Corona, waliokufa mpaka sasa 1,525,294 ikiwa ulikuwa umechukulia kiurahisi, hizi takwimu zikuamshe kwamba Mungu ametupendelea sana Tanzania tunamshukuru sana Mungu kwa niaba ya wenzetu,” alisema Dkt. Lekundayo.

Awali akitoa mahubiri kabla ya maombi hayo pamoja na kuwasihi waumini kumshukuru Mungu kuwapitisha katika janga la Corona, Askofu Lekundayo pia ametoa wito kwa waumini kuendelea kumshukuru Mungu pia kwa namna ambavyo amelipitisha Taifa katika Uchaguzi Mkuu, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya jambo ambalo litabaki kumbukumbu yao juu ya neema ya Mungu katika masuala hayo.

Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema Tanzania kupitishwa katika Janga la Corona haikuwa bahati bali ni neema ya Mungu, hivyo akawashukuru viongozi wa Dini kwa kuliombea Taifa kwa juhudi na Mungu akajibu.

Aidha, Kiswaga amesema Serikali inaendelea kuheshimu mchango wa kanisa na itaendelea kushirikiana nalo katika majukumu yake ya kitume na kimaendeleo, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze kufanya kazi kwa manufaa na ustawi wa Watanzania.

“Katika neno la Mungu kuna habari ya wale wakoma kumi ambao waliponywa na Bwana Yesu lakini aliyerudi kushukuru ni mmoja tu, ninaamini maombi haya ya shukrani yaendelea kuiponya nchi yetu na majanga ambayo yanaonekana kwa macho na ambayo hayaonekani,” alisema Kiswaga.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye  amesema kuna baadhi ya watu waliobeza Mhe Rais alivyotangaza  kumtanguliza Mungu kwa kutangaza siku tatu za kuliombea Taifa ili aliponye Taifa  na Janga la Corona lakini baada ya kuona matokeo ya maombi naamini wameona kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi.

MWISHO

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akihubiri  katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani  hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye akiongoza maombi katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(kushoto), iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Kwaya kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Kwaya kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Sabasaba Musoma mkoani Mara ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye, katika  ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Kutoka kushoto Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt. Mch. Godwin Lekundayo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Waadventisa Wasabato wakichangia ujenzi wa Kibweta kama alama ya shukrani kwa Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt. Mch. Godwin Lekundayo,, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye akitoa salamu katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika salama hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazin kwa amani i mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakishiriki maombi katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akihubiri  katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani  hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akivishwa skafu na vijana watengeneza njia katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(Kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Wednesday, December 2, 2020

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA MKOANI SIMIYU

Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limewakamata wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega. 

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Desemba 02, 2020 katika Kituo cha Polisi cha Lamadi, Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Simiyu, Mariam Mwanzalima amesema wahamiaji haramu hao wamekamatwa  Desemba 02, 2020 na askari  waliokuwa doria . 

“ Katika maelezo yao wanasema wametokea Kenya walikuwa wanaelekea  Malawi wakisindikizwa na Wakenya wawili, walipofika Lamadi ilitokea purukushani kati yao na wasindikizaji wao baada ya kuwalazimisha kupanda kwenye mitumbwi ili watembee nao ziwani; ndiyo wakakimbia na kuelekea mashambani, bahati nzuri askari wetu walikuwa doria wakafanikiwa kuwakamata” alisema Mwanzalima.

Ameongeza kuwa wahamiaji haramu hao watafikishwa mahakamani kwa kuwepo nchini kinyume cha sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 rejeo la mwaka 2016 kifungu cha 4 hukumu yao ikiwa ni kifungo kisichopungua miaka miwili, huku akibainisha kuwa Vyombo vya usalama vinaendelea kuwatafuta wasindikizaji wa wahamiaji hao na watakapokamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. 

Aidha, Mwanzalima ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufanya kazi zitakazowaingizia kipato halali na kuwaonya wasijiingize katika biashara haramu ikiwemo ya kusafirisha wahamiaji haramu jambo ambalo linaweza kupelekea wao kushtakiwa,  nyumba na vyombo vya usafiri vitakavyotumika katika biashara hiyo kutaifishwa.

“Natoa onyo kwa Mtanzania yeyote aliyeko Mkoa wa Simiyu atakayejishughulisha kuwasaidia, kuwaonyesha njia ya kwenda popote tukimkamata sheria inasema atafungwa kifungo kisichopungua miaka 20, atakayewahifadhi kwenye nyumba yake atafungwa na nyumba itataifishwa na serikali; ambaye chombo chake kitatumika kuwasafirisha atafungwa miaka 20, atalipa faini isiyopungua milioni 20 na chombo chake kitataifishwa,” alisema Mwanzalima. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewataka wananchi kuwa makini na kuhakikisha kuwa wageni wanaoingia katika maeneo yao wanawafahamu na ikitokea kuna watu wanaowatilia shaka  watoe taarifa kwa viongozi walio katika mamlaka zao za utawala na viongozi hao washirikiane na  vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe haraka. 

Mmbaga ametoa wito kwa vijana wa Mkoa wa Simiyu kutumia fursa ya amani iliyopo hapa nchini kuendelea kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kufanya kazi zitakazo waingizia kipato halali na katu wasijiingize kwenye biashara haramu, huku akibainisa kuwa mkoa huo hautawafumbia macho wote watakaojihusisha na vitendo vya biashara haramu. 

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP. Richard Abwao ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale watakapowaona watu wasiowatambua katika maeneo yao ili kuendelea kuimarisha ulinzi wao pamoja na mali zao katika maeneo waliyopo.

MWISHO

Wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 waliokamatwa Desemba 02, 2020 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu wakiwa katika kituo cha Polisi cha Lamadi.

Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Simiyu, Mariam Mwanzalima akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tukio la  kukamatwa kwa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega, Desemba 02, 2020 katika . kituo cha Polisi cha Lamadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega Desemba 02, 2020 katika . kituo cha Polisi cha Lamadi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega Desemba 02, 2020 katika  kituo cha Polisi cha Lamadi.

Baadhi ya wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega wakiwa katika Kituo cha Polisi Lamadi Wilayani Busega Desemba 02, 2020.

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Maafisa wa jshi la Polisi na Idra ya Uhamiaji wakiwa katika katika Kituo cha Polisi Lamadi Wilayani Busega Desemba 02, 2020 kabla ya Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Simiyu, Mariam Mwanzalima kutoa taarifa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu 34 raia wa Ethiopia Desemba 02, 2020 na kupelekwa kituoni hapo.

 Wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 34 waliokamatwa Desemba 02, 2020 katika kitongoji cha Mwalukonge Kijiji cha Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu wakiwa katika kituo cha Polisi cha Lamadi.

WANANCHI SIMIYU WAHIMIZWA KUPIMA VVU KUJUA HALI ZAO ZA MAAMBUKIZI

 Wito umetolewa kwa Wananchi mkoani Simiyu kujitokeza kupima Virusi vya UKIMWI (VVU) ili kujua hali za maambukizi ili wale watakaobainika kuwa na maambukizi waweze kuanzishiwa dawa mara moja na ambao watabainika kutokuwa na maambukizi kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya maambukizi hayo.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba wakati akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 mjini Bariadi, ambapo amebainisha kuwa pamoja na huduma za upimaji kutolewa bila malipo bado mwitikio wa upimaji ni mdogo.

“Hadi kufikia Juni 2020 ni asilimia 74 tu ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika mkoa wa Simiyu walikuwa wanafahamu hali zao za maambukizi, takwimu hizi zinaonesha kwamba katika kila wana Simiyu 100 wanaoishi na VVU, 26 miongoni mwao hawajapima kujua hali zao za maambukizi,”alisema Dkt. Kulemba.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba(mwenye suti nyeusi)  akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga (aliye kushoto kwake) juu namna Mkoa unavyotekeleza mpango wa Tohara kinga wakati alipotembelea banda la Maonesho la Shirika lisilo la Kiserikali la Intra Health ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mtaalam wa Maabara kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la CUAMM, Juma Lupembe akichukua damu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  kwa ajili ya kufanya vipimo, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa mbalimbali,  katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Msanii wa Kizazi kipya Fid Q akitoa burudani katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga (wa pili kushoto ) akipokea maelezo juu ya namna Mradi wa Afya kamilifu unavyotekelezwa na AMREF Health Africa,  katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga akizungumza na baadhi ya watumishi wanaofanya kazi katika Mradi wa Afya kamilifu unavyotekelezwa na AMREF Health Africa, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wadau wa afya mkoani hapa, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga, akimkabidhi sanduku la kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa ajili ya kulitumia kukusanya michango ya wananchi na wadau kwenye mfuko huo, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga , akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Maonesho la Shirika lisilo la Kiserikali la Intra Health kwa ajili ya kupata maelezo juu namna Mkoa unavyotekeleza mpango wa Tohara kinga akiwa  amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wadau wa afya mkoani hapa, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Msanii wa Kizazi kipya Fid Q akitoa burudani katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wadau wa afya mkoani hapa, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mtaalam wa Afya kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors with Africa, Frank Adolf akimpima urefu Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mtaalam wa Afya kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors with Africa, akitoa maelezo ya uwiano wa urefu na uzito na hali ya lishe kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, viongozi wa dini  na baadhi ya wadau wa afya mkoani hapa, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Meneja Mradi wa Afya Kamilifu mkoa wa Simiyu unaotekelezwa na AMREF Health Africa, Dkt. Mathias Abuya akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) juu ya mradi huo, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba(kushoto)  akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga (katikati) juu namna Mkoa unavyotekeleza Mradi wa Afya Kamilifu mkoa wa Simiyu chini ya AMREF Health Africa, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba(katikati)  akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga (kulia) na viongozi wengine kuelekea kukagua mabanda ya huduma, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu , wadau wa afya na wajumbe wa kamati za usimamizi wa afya za wilaya (CMHT) , katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba(kushotoi)  akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga (katikati) na viongozi wengine kuelekea kukagua mabanda ya huduma, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Ekwabi Mujungu akisalimiana na msanii wa kizazi kipya Fid Q mara baada ya msanii huyo kutoa burudani, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba(wa  tatu kushotoi)  akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo  Kiswaga (katikati) na viongozi wengine kuelekea kukagua mabanda ya huduma, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Kwaya ya AICT Bariadi wakiimba wimbo maalum kuhusu UKIMWI, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe. Festo Kiswaga wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani yaliyofanyika kimkoa Desemba 01, 2020 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!