Monday, July 10, 2017

MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI SIMIYU

Mwenge wa Uhuru 2017 umehitimisha Mbio zake Mkoani Simiyu na kukabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10/07/2017.

Akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Halmashauri zote sita za Mkoa huo katika umbali wa kilometa 780.

Sagini amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Simiyu umeweza kuweka mawe ya msingi, kufungua, kuzindua, kukagua na kuona jumla ya miradi 43 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 8,450,841,622/= ambazo ni fedha kutoka Serikali Kuu, Halmashauri, nguvu za wananchi,sekta binafsi na washirika wa maendeleo.


Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 zimebeba Ujumbe Mkuu “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU”
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Ndg Albert Msovela katika Kijiji cha Kinampanda Wilaya ya Kishapu Mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Dkt.Seif Shekalaghe (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(kulia) kabla ya kuukabidhi katika mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(kulia) akimtakia Kila la Heri Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Ndg Albert Msovela(kushoto)  katika Kuukimbiza Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga mara baada ya makabidhiano.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akiagana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akiagana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu muda mfupi kabla ya makabidhiano ya ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkoa wa Simiyu na Shinyanga.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017,Vatima Yunus Hassan  kutoka Kusini Pemba(kushoto) na Shukran Islam Msuri kutoka Mjini Magharibi wakiagana na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa 2017 Salome Obadia Mwakitalima akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Dkt.Seif Shekalaghe
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017 wakiagana na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu muda mfupi kabla ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika ya Mkoa wa Simiyu na Shinyanga.

Sunday, July 9, 2017

WAZAWA WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE MAENEO YA UWEKEZAJI

Halmashauri ya wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu imetakiwa kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wazawa pindi wanapogawa maeneo ya uwekezaji wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira na uchumi ndani na nje ya Mkoa, ambapo jumla ya ekari 1000 zimeshatengwa kwa ajili yauwekezaji.

 Wito huo umetolewa leo na Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour wakati wa kukagua na kukabidhi hati ya eneo la uwekezaji wa viwanda kwa Mkurugenzi wa  Halmashauri  lililopo katika kata ya Nyalikungu Wilaya ya Maswa
 .
Kiongozi huyo amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Maswa kwa kutekeleza agizo la Serikali la kutenga eneo la uwekezaji na kusema kuwa ni vema wazawa wakapewa kipaumbele kwa kupatiwa maeneo hayo, ili waanze ujenzi wa viwanda mbalimbali vitakavyokuza ajira, kuchangia pato la Halmashauri, pato la mwananchi mmoja mmoja  na uchumi wa Nchi kwa ujumla.

 "Nashauri Halmashauri kutoa kipaumbele kwa wazawa kwa kuwapatia maeneo hayo ya viwanda ili wafanye shughuli za kimaendeleo ambazo zitagusa moja kwa moja maisha ya Wananchi wa Wilaya ya Maswa, mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja suala la ajira kwa vijana ....Alisema.
Pamoja na kuwapa kipaumbele wazawa Ndg. Amour ameutaka uongozi wa Wilaya ya Maswa kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wageni na kutoa maeneo kwa wote watakaokidhi masharti ya kuwekeza na kujenga viwanda  kwa mujibu wa sheria za nchi.

Aidha Amour ameishauri Halmashauri hiyo kuanzishwa viwanda ambavyo vitayaongezea thamani mazao na kutoa bidhaa zitakazoingia sokoni moja kwa moja,  badala ya kung'ang'ana viwanda vinavyoandaa malighafi zitakazotumiwa na viwanda vilivyo nje ya nchi; kama ilivyo kwa viwana vingi vya pamba huandaa pamba inayoenda kuzalisha nguo nje ya nchi.

 Pia amefurahishwa na kuupongeza uongozi  mzima wa Halmashauri hiyo kwa jitihada wanazozifanya za kuanzisha viwanda vinavyoiongezea halmashauri mapato kikiwemo kiwanda cha Chaki, sambamba na kuhakikisha wanaendana na kasi ya Mhe Rais ya kuwa na Tanzania ya viwanda .

Naye Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa John Nkoko amesema kuwa tayari wameshatenga ekari 1000 kwa ajiri ya eneo la viwanda na tayari eneo la ekari 315.64 limeshaandaliwa michoro ya mipango miji.
Nkoko amesema kuwa lengo la Halmashauri yao kutenga eneo hilo ni kuhakikisha wanatengeneza fursa ya ajira kwa wananchi wao pamoja na kukuza uchumi wao wa ndani na nje ya Mkoa .

 Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Dk Fredrick Sagamiko alisema Wilaya yake itahakikisha inapambana kuwa na uchumi wa kati kwa kuanzisha viwanda mbalimbali ambapo mpaka sasa wameanza ujenzi mpya wa kiwanda kikubwa cha chaki ambacho kitakuwa cha kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na teknolojia mpya.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Maswa umeweka mawe ya mingi, kuzindua, kufungua na kuona miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Viwanda, Afya, Elimu, Kilimo, Utawala Bora,Maendeleo ya Jamii,Ardhi Maliasili na Mazingira.

Akitoa Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika maeneo mbalimbali ya miradi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amewaasa wananchi kufanya kazi kwa bidii, kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za nchi pamoja na kupambana na rushwa, dawa za kulevya, malaria na UKIMWI.  

Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Shughuli za Uzalishaji katika Kiwanda cha Kusaga na Kuhifadhi Nafaka kilichopo Malampaka Wilayani Maswa, Epifania Labia.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Busega ,Mhe.Tano Mwera katika Kijiji cha Malita wilayani Maswa..
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akimkaribisha Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour tayari kwa kuanza Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilayani humo.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akifungua Mradi wa Bwalo la Chakula katika Shule ya Sekondari Malampaka.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wa Kata ya Kadoto mara baada ya kufungua nyumba ya Watumishi wa Zahanati ya Kadoto(inayoonekana pichani)
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akipata maelezo juu ya mradi wa Kitalu cha Miti ya Kivuli na Matunda unaosimamiwa na Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour juu ya shughuli za utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazofanywa na kikundi cha vijana.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akipata maelezo juu ya mradi wa kiwanda cha uzalishaji chaki kutoka kwa Kiongozi wa Kikundi cha Maswa Family.

Baadhi ya Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Maswa wakishuhudia Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour (hayupo pichani) akikagua eneo llililotengwa maalum kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda lenye ukubwa wa ekari 1000.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akifungua nyumba ya kuishi watumishi wa Zahanati ya Kadoto ilyopo Kata ya Kadoto wilayani Maswa.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi mara baada ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bangi zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Maswa.
Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha Wanawake wajasiriamali wilayani Maswa.

Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Klabu ya Wapnga Rushwa katika Shule ya SekondariMalampaka






Saturday, July 8, 2017

WANANCHI WAHIMIZWA KUPENDA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Ndg. Amour Hamad Amour ametoa wito kwa wananchi kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Amour ametoa wito huo wakati alipokuwa akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Mradi wa kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao Kilimo cha BUSEGA MAZAO LIMITED katika kijiji cha Mwanangi wilayani Busega.

Amesema wananchi watakapotumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini watasaidia kuongeza uzalishaji kutokana na kuwepo kwa soko la uhakika kwa viwanda na hatimaye kuongeza uchumi wa nchi.

Ameongeza kuwa wawekezaji wanapaswa kuzalisha bidhaa bora ambazo zitakidhi vigezo vya kiushindani sawa sawa na zile zinazotoka nje ya nchi ili kupunguza uingizwaji wa bidhaa za nje na kulifanya Taifa kuongeza pato lake.

“.....bidhaa ambazo zinazotoka nje zinapoingia hapa ndani zinakuwa na bei ndogo kuliko zinazozalishwa hapa nchini, ni  kwa sababu bado hatujajipanga kuzalisha kiushindani, sasa tuzalishe bidhaa zenye ushindani ili kuweza kuua soko la bidhaa ambazo zinatoka nje tuweze kukuza uchumi wa Taifa letu” alisema.

Aidha, amesema mwekezaji wa kiwanda cha BUSEGA MAZAO LIMITED atakapoanza uzalishaji  atoe kipaumbele cha ajira kwa wananchi wa wilaya ya Busega na ahakikishe wanafanya kazi katika hali ya usalama na kupewa haki na maslahi yao kama inavyostahili.

Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru 2017  pia amewataka wakazi wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanazalisha kwa wingi mazao yote yanayotakiwa katika kiwanda hicho ukiwepo mpunga na mahindi kwa kuwa kitatoa soko la uhakika na kupelekea ongezeko la pato la mtu mmoja mmoja.

Akisoma taarifa ya mradi wa kiwanda hicho,Ndg. Lazaro Japhet kutoka BUSAGA MAZAO LIMITED amesema Kiwanda hicho kitawasaidia wakulima kupata soko, kuhifadhi na kuongeza mazao yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera amesema Serikali wilayani humo iko tayari kushirikiana na wawekezaji ambao watakuwa tayari kuwekeza katika wilaya hiyo.

Sambamba na hayo Ndg.Amour Hamad Amour amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii, kulinda rasilimali za nchi na kuendelea kupambana na rushwa, dawa za kulevya, malaria na UKIMWI ili kuweza kufikia Tanzania ya Uchumi wa Kati.

Akizungumza na wananchi na wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mkula Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017 amesisitiza wanafunzi wa shule za sekondari kuwa na Klabu za wapinga rushwa, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, malaria na UKIMWI ili waweze kufikia malengo yao.


Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Busega umepitia jumla ya miradi 9 katika sekta ya Elimu, Afya, Maji,Utawala Bora, Viwanda na Maendeleo ya jamii, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5.



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(wa tano kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa watumishi katika Kiwanda Cha BUSEGA MAZAO LIMITED mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho wilayani Busega

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Salome Mwakitalima tayari kwa kuanza kuukimbiza katika Wilaya yake.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akikagua moja ya vyumba vinne vya madarasa vilivyofunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Shule ya Sekondari Mkula wilyani Busega.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akipanda mti katika Shule ya Sekondari Mkula Wilayani Busega.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akizindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Mkula Wilayani Busega
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(kulia) na Mkuu wa Wilaya wakishangilia baada ya Klabu ya Wapinga rushwa kuzinduliwa katika Shule ya Sekondari Mkula.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amourakiangalia moja ya miundombinu ya maji katika Mradi wa Maji wa Lukungu kabla ya kufungua mradi ambao utaanza kwa kuwahudumia takribani wananchi 4022.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akifungua mradi wa Maji wa Lukungu wilayani Busega ambao utaanza kwa kuwahudumia wananchi 4022 na kufikia mwaka 2030 utawahumia wananchi 11,500.
Lazaro Japhet akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamni ya azaoya kilimo cha BUSEGA MAZAO LIMITED kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(hayupo pichani) kabla ya kuwekwa kwa jiwe la msingi la kiwanda hicho.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akimtwisha ndoo ya maji Mkimbiza Mwenge Kitaifa Salome Mwakitalima mara baada ya kufungua mradi wa Maji wa Lukungu wilayani Busega.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kusindika nafaka cha BUSEGA MAZAO LIMITED wilayani Busega.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la Msingi kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao BUSEGA MAZAO LIMITED wilayani Busega.
Baadhi ya viongozi na wananchi wilaya ya Busega wakimfuatilia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour(hayupo pichani) akikagua Kiwanda cha BUSEGA MAZAO LIMITED kabla kuweka jiwe la msingi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwanangi kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha BUSEGA MAZAO LIMITED.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na kikundi cha wanawake wajasiriamali wakionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa Mwaka 2017 ,Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na kikundi cha wanawake wajasiriamali wakionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza.


Friday, July 7, 2017

WANAFUNZI WA SEKONDARI WAHIMIZWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

Wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamehimizwa kusoma masomo ya sayansi ili kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Uchumi wa Viwanda kama inavyoelezwa pia katika Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour wakati wa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani BARIADI.

Amour amesema Serikali imejenga maabara  na kuweka vifaa katika shule mbalimbali za sekondari kwa lengo la kuwezesha wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo ili kuwaandaa kuwa wataalam katika maeneo tofauti.

Amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzitumia vizuri maabara zilizopo ili wapate ujuzi wa nadharia na vitendo utakaowaandaa kuwa wabobezi kwenye maeneo mbalimbali yanayohitaji utalaam wa kisayansi.

“, nahimiza huduma nzuri za maabara vijana hawa waweze kusoma masomo ya kemia, fizikia, bailojia na hisabati ili waende sawa na Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu ya “Shiriki katika Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu” wakashike nafasi mbalimbali wawe wakemia, wahandisi katika viwanda, wawe madaktari na nafasi nyingine nyingi" amesema Amour

Akizungumzia mapambano dhidi ya dawa za kulevya amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kuziba mianya yote na kutokomeza shughuli za uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya na wasisite kutoa taarifa katika vyombo vya dola wanapobaini watu wanaofanya shughuli hizo ili wachukuliwe hatua..

Aidha, akizungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali ambayo Mwenge wa Uhuru umeweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo, Ndg.Amour amewapongeza na kuwataka wananchi kuendelea kuchangia miradi hiyo na kutokubaliana na viongozi wanaowashawishi kuacha kuchangia maendeleo yao.

“ Kila mradi tuliopita taarifa inaonesha kuna nguvu ya wananchi, nawapongeza sana kwa kushirikiana na Serikali kutekeleza miradi ya elimu, afya, maji na mingine mingi,nawasihi msikubaliane na watu wanaowataka kutochangia miradi ya maendeleo” amesema

Mara baada ya kuweka mawe ya msingi, kuzindua na kufungua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya BARIADI Mwenge wa Uhuru tarehe 08/07/2017 utakimbizwa wilayani BUSEGA.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akicheza pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkololo baada ya Mwenge wa Uhuru kufika katika Shule hiyo kwa ajili ya kuzindua klabu ya wapinga rushwa, klabu ya kupambana na dawa za kulevya na kuona mradi wa hifadhi ya mazingira

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Abdallah Malela akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Festo Kiswaga Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuupokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji(hayupo pichani)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akikagua na kuona mraidi wa hifadhi ya mazingira katika Shule ya sekondari Nkololo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akikagua moja ya vyumba vitatu vya madara vilivyofunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Shule ya Msingi Nkololo “B” wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akisalimiana na baaadhi ya watalaam wa Afya mara baada ya kufungua Kituo cha Ushauri, upimaji na matibabu(CTC)kwa watu wenye VVU katika Kituo cha Afya cha Songambele wilaya ya Bariadi, Mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akimkabidhi cheti mmoja wa wanachama wa Klabu ya kupambana na dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Nkololo mara baada ya kuzindua klabu hiyo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akimkabidhi cheti cha Utunzaji wa Mazingira Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkololo mara baada ya kutembelea na kuona mrai huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akiangalia baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kikundi cha vijana kutoka Kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Nkololo mara baada ya kuweka jiwe la msingi kisima kirefu cha maji kijijini hapo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akitoa ujumbe wa Mwenge kwa  wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkololo pamoja na wananchi wa Nkololo mara baada kuzindua na kuona miradi mbalimbali shuleni hapo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Kisima kirefu katika kijiji cha Nkololo ilaya ya Baraidi, Mkoani Simiyu.


 

Thursday, July 6, 2017

WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour amewataka watalaam wa afya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wananchi ili kuepuka madhara mbalimbali kiafya.

Ndg.Amour ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Duka la Dawa katika Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia dawa kwa mazoea pasipo kufuata maelekezo ya madaktari na wauguzi hali ambayo ni hatari kwa afya  zao.

“ Wapo watu wanatumia dawa kiholela na kuathiri kinga ya mwili, inafika kipindi dawa zinawaathiri moja kwa moja hata wanapotakiwa kuzitumia kutibu maradhi waliyonayo haziwasaidii, wapeni elimu wananchi watumie dawa kulingana na maelekezo ya wataalam”

Aidha, amewataka madaktari na wauguzi kutoa huduma stahiki kwa wananchi kupitia duka hilo kwa kuwauzia dawa kwa bei elekezi na kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote,  ili wanapoandikiwa dawa na kuikosa hospitali, vituo vya afya na zahanati wazipate katika duka hilo.

Kwa upande wake mmoja wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg.Fredrick Ndahani ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto kwa jitihada za kuhakikisha kuwa kila Hospitali ya Mkoa na Wilaya inakuwa na Duka la dawa la Bohari  ya Dawa ya Taifa(MSD), ambayo yatawawezesha wananchi kupata dawa zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu.

 Sanjali na hilo Ndahani ametoa wito kwa wanachi wote kujenga utamaduni wa kuangalia tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa(expire date) kabla ya kutumia ili wasitumie dawa zilizokwisha muda wake.

Akiwasilisha taarifa ya mradi wa duka la dawa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Dkt.Akilimali Mponzemenya amesema lengo la kujenga duka hilo ni  kuwezesha upatikanaji wa dawa zilizothibitishwa na Mamlaka ya Dawa kwa urahisi na kwa bei nafuu zaidi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika maeneo tofauti, ametoa wito kwa wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi bidii  na kulinda rasilimali za nchi hii.


Mwenge wa Uhuru unaendele na Mbio zake Mkoani na leo upo katika Halmashauri ya Mji Bariadi, ambapo umeweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu , Maji, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii na jumla ya miradi 6 imepitiwa pamoja na klabu ya wapinga rushwa kufunguliwa katika Shule ya Sekondari Bariadi. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akikagua duka la dawa la Serikali lilolopo katika Hospitali ya Somanda mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi katika Mtaa wa Nyangokolwa Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kulia) akimpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour katika wilaya yake.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akifungua daraja la Gabasingilya Mjini Bariadi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akifuatilia maelekezo ya mmoja wa wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Bariadi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi  Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Bariadi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akizindua duka la dawa la Serikali katika Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akiangalia namna kikundi cha vijana kinavyofanya shughuli zake katika mradi wa kukoboa na kusaga nafaka Mjini Bariadi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha wanawake cha Elimika Mjini Bariadi.
Mwenge wa Uhuru ukitoka katika eneo la Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi baada ya kuzindua Duka la Dawa la Serikali.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg.Fredrick Ndahani akizungumza na wakazi wa Bariadi Mjini katika eneo la Hospitali ya Somanda baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua Duka la dawa la Serikali.


Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!