Thursday, July 6, 2017

WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour amewataka watalaam wa afya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wananchi ili kuepuka madhara mbalimbali kiafya.

Ndg.Amour ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Duka la Dawa katika Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia dawa kwa mazoea pasipo kufuata maelekezo ya madaktari na wauguzi hali ambayo ni hatari kwa afya  zao.

Wapo watu wanatumia dawa kiholela na kuathiri kinga ya mwili, inafika kipindi dawa zinawaathiri moja kwa moja hata wanapotakiwa kuzitumia kutibu maradhi waliyonayo haziwasaidii, wapeni elimu wananchi watumie dawa kulingana na maelekezo ya wataalam”

Aidha, amewataka madaktari na wauguzi kutoa huduma stahiki kwa wananchi kupitia duka hilo kwa kuwauzia dawa kwa bei elekezi na kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote,  ili wanapoandikiwa dawa na kuikosa hospitali, vituo vya afya na zahanati wazipate katika duka hilo.

Kwa upande wake mmoja wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg.Fredrick Ndahani ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto kwa jitihada za kuhakikisha kuwa kila Hospitali ya Mkoa na Wilaya inakuwa na Duka la dawa la Bohari  ya Dawa ya Taifa(MSD), ambayo yatawawezesha wananchi kupata dawa zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu.

 Sanjali na hilo Ndahani ametoa wito kwa wanachi wote kujenga utamaduni wa kuangalia tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa(expire date) kabla ya kutumia ili wasitumie dawa zilizokwisha muda wake.

Akiwasilisha taarifa ya mradi wa duka la dawa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Dkt.Akilimali Mponzemenya amesema lengo la kujenga duka hilo ni  kuwezesha upatikanaji wa dawa zilizothibitishwa na Mamlaka ya Dawa kwa urahisi na kwa bei nafuu zaidi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika maeneo tofauti, ametoa wito kwa wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi bidii  na kulinda rasilimali za nchi hii.


Mwenge wa Uhuru unaendele na Mbio zake Mkoani na leo upo katika Halmashauri ya Mji Bariadi, ambapo umeweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu , Maji, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii na jumla ya miradi 6 imepitiwa pamoja na klabu ya wapinga rushwa kufunguliwa katika Shule ya Sekondari Bariadi. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akikagua duka la dawa la Serikali lilolopo katika Hospitali ya Somanda mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi katika Mtaa wa Nyangokolwa Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga (kulia) akimpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour katika wilaya yake.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akifungua daraja la Gabasingilya Mjini Bariadi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akifuatilia maelekezo ya mmoja wa wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Bariadi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi  Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Bariadi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akizindua duka la dawa la Serikali katika Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akiangalia namna kikundi cha vijana kinavyofanya shughuli zake katika mradi wa kukoboa na kusaga nafaka Mjini Bariadi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha wanawake cha Elimika Mjini Bariadi.
Mwenge wa Uhuru ukitoka katika eneo la Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi baada ya kuzindua Duka la Dawa la Serikali.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg.Fredrick Ndahani akizungumza na wakazi wa Bariadi Mjini katika eneo la Hospitali ya Somanda baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua Duka la dawa la Serikali.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!