Wednesday, July 5, 2017

WAKAZI 2228 WILAYANI ITILIMA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA

Jumla ya wakazi 2228 wa mji wa  Lagangabilili Wilayani Itilima  wanatarajia kuondokana na  adha ya kupata huduma ya  maji umbali mrefu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa chanzo cha maji ya bomba chenye uwezo wa  kutoa maji kiasi cha lita za ujazo 15000 kwa saa.
 Chanzo hicho cha maji chenye mtandao wa  mabomba ya maji ya urefu wa mita 29,431 na vituo vya kuchotea 20 vitawasaidia wananchi hao kupunguza muda  waliokuwa wakiupoteza kufuata huduma ya maji umbali wa kilometa zaidi ya mbili

 Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo wa maji kwa  kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Amour Hamad Amour,mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Itilima Goodluck  Masige amesema kuwa wananchi wa mji wa lagangabilili  wamekuwa wakifuata  maji kwa umbali  mrefu hali inayopelekea kupoteza muda mwingi ambao wangetumia  kutekeleza  shughuli za maendeleo.

Masige amesema kuwa mradi huo ambao utagharimu jumla ya shilingi milioni 978 hadi kukamilika kwake utasaidia  kupunguza tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi, ambapo amesema pamoja na kuwaduhumia wananchi utaweza kutoa huduma ya maji kwa taasisi mbalimbali katika Mji wa Lagangabilili  na kunywesha mifugo.
 
 Aidha kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahishwa sana na mradi huo ambao utawatua ndoo vichwani akinamama na kuwapumzisha mzigo mzito waliokuwa wakiubeba kwa kipindi kirefu.

 "Nimefurahishwa sana na mradi huu...ni  mradi ambao utakuwa na manufaa makubwa katika ustawi wa maendeleo ya wananchi sambamba na kuwatua akinamama hawa ndoo kichwani,jambo  ambalo ni azma ya Serikali ya awamu ya Tano  “ amesema

Aidha,  kiongozi huyo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kuunda kamati za watumia maji ili kuboresha huduma za utoaji maji kwa wananchi wote bila kujali tofauti za kiitikadi, dini ,rangi siasa wala kabila na kusimamia utunzaji wa miradi yote ya maji.

Sambamba na hilo Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la Msingi katika jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima amepongeza Wakala wa Majengo wa Taifa(TBA) kwa kujenga jengo kubwa lenye vyumba zaidi ya 40 katika ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.

Ndg.Amour amesema jengo hilo litakapokamilika watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima walitumie vizuri kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa uadilifu na kuacha mazoea katika utendaji.

Pamoja na kuweka jiwe la Msingi katika Chanzo cha Mradi wa Maji Lagangabilili na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya, Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Itilima umezindua vyumba vinne vya madarasa na klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Budalabujiga,kuweka jiwe msingi Bweni la Wavulana Kanadi Sekondari na kuona maboresho ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa ufugaji wa nyuki.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani(kushoto) akijiandaa kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(kulia) Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuanza kuukimbiza katika wilaya yake.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akifungua chanzo cha  mradi wa maji ya bomba katika Mji wa Lagangabilili wilayani Itilima
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akivikwa skafu na vijana wa skauti wa Wilaya ya Itilima.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wa Lagangabilili mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akisisitiza jambo mara baada ya kufungua vyumba vinne katika Shule ya Sekondari Budalabujiga wilayani Itilima.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la msingi Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akiangalia sabuni zinazotengenezwa na vikundi vya wanawake wakati alipokwenda kuona maboresho ya viwanda Kanadi Itilima.
Wakazi wa Lagangabilili wilayani Itilima wakichota maji  baada ya kuweka jiwe la msingi katika chanzo cha maji ya bomba.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima akitoa maelezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru juu ya mradi wa utengeenzaji wa sabuni unaotekelezwa na vikundi vya wanawake wa Kanadi wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour(wa nne kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa Klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Budalabujiga wilayani Itilima.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Budalabujiga wilayani Itilima wakiushangilia Mwenge wa Uhuru mara tu ulipowasilis shuleni hapo kuzindua vyumba vinne vya madara na klabu ya wapinga rushwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Amour Hamad Amour akiwa na baadhi ya viongozi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika bweni la wavulana katika shule ya sekondari Kanadi wilayani Itilima.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!