Monday, November 16, 2020

SIMIYU KUFANYA MAJARIBIO KUTUMIA VYETI VYA VYUO VIKUU KUDHAMINI MIKOPO

Katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya majaribio ya kutumia vyeti vya taaluma kwa wahitimu wa vyuo vikuu kama dhamana ya mikopo ili kuwawezesha  kupata mitaji na kujiajiri kupitia sekta ya kilimo na viwanda. 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alipokutana na baadhi ya vijana jana Novemba 15, 2020 mjini Bariadi kwenye mjadala wa ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo ambao ulihudhuriwa pia na wadau wa maendeleo akiwemo  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi.

“Tunataka (tu pilot) tufanye majaribio na tutakuwa (number one) wa kwanza, tutawafuata wadau (UNDP) kuwaeleza kuwa tumekuja na namna ya kuwasaidia vijana waliomaliza vyuo vikuu ili tuone kama vyeti vyao vinaweza kusimama kama dhamana badala ya vyumba na viwanja ambavyo wao hawana,”

“Tutawaambia vijana hao wenye maandiko ya miradi  wawasilishe iwe ni kwa mtu binafsi au kikundi, tutajadiliana tuone ‘risk’ zikoje,” alisema Mtaka.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bibi. Christine Musisi ametoa wito kwa vijana kuhamasika kubadili mitazamo kutoka kwenye mawazo tegemezi kwenda katika mawazo ya kujitegemea wenyewe na kwenda mbele zaidi kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka, huku akiahidi kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na Mkoa wa Simiyu kama mdau wa maendeleo.

Baadhi ya vijana wametoa mapendekezo mbalimbali ambayo yakifanyiwa kazi na serikali, vijana wenyewe na wadau wengine yataweza kuchangia kuleta ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana.

“Tunaomba Serikali ituboreshee miundombinu ya kilimo tutoke kwenye kilimo cha kutegemea mvua twende kwenye kilimo cha umwagiliaji ili tuzalishe malighafi ya kupeleka viwandani,” alisema Adrian Paul.

“Njia nyingine ya kuongeza ajira kwa vijana na Serikali kufufua viwanda vilivyokufa na kuanzisha viwanda vipya ili iweze kuzalisha ajira kwa rika zote wakiwemo vijana,” alisema Afisa Vijana Itilima

“Elimu ya kujitegemea irudishwe na ianze kufundisha mashuleni ili kuwaanda watoto tangu wakiwa wadogo kujitegemea ili hata atakapomaliza masomo akakasa ajira aweze kujiajiri mwenye na kujitegemea,” alisema Asia Kimaro kutoka Wilayani Maswa.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka UNDP, Bw. Amon Manyama ameahidi kushirikiana na mkoa wa Simiyu katika maandiko ya miradi huku akitoa wito kwa vijana kujituma na kutokuridhika kwa kufanya kazi moja badala yake kila mmoja aone umuhimu wa kuwa kazi zaidi ya mbili.

MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa huo katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa wa Simiyu katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Asia Kimaro mmoja wa Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka (wa saba kulia), katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga,  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi (wa sita kulia), baadhi ya vijana wasomi kutoka maeneo mbalimbali na baadhi ya maafisa kutoka UNDP kabla ya kushiriki mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Afisa Vijana wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Zena Mchujuko akiwasilisha maada katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mwandishi wa vitabu na Mtumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa wa Simiyu katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa Vijana akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi ukihusisha baadhi ya vijana na wadau wa maendeleo .
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), akizungumza na baadhi ya vijana wasomi kutoka mikoa mbalimbali nchini juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi mkoani Simiyu.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa huo katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa Vijana akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi ukihusisha baadhi ya vijana na wadau wa maendeleo .
Mkurugenzi wa Jembe ni Jembe Company Limited,  Dkt. Sebastian Ndege akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa Vijana akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi ukihusisha baadhi ya vijana na wadau wa maendeleo .
Mmoja vijana wasomi kutoka mkoa wa Mara, Dkt. Makaranga akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mgunduzi na mmiliki wa dawa ya kuua wadudu ya Vuruga,  Dkt. Neva  akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya vijana wasomi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Kijana Msomi na Mjasiriamali kutoka  jijini Dar es salaam Bi. Juliana Mataba akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka UNDP, Bw. Amon Manyama akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa wa Simiyu katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Mmoja wa wadau wa  maendeleo wa mkoa wa Simiyu, Bw. Joshua Mirumbe akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya vijana wasomi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi na baadhi ya wadau  juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya vijana wasomi juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, katika mjadala uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mgunduzi na mmiliki wa dawa ya kuua wadudu ya Vuruga,  Dkt. Neva  (kulia) akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, katika mjadala uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Sunday, November 15, 2020

WATANZANIA TUMUUNGE MKONO JPM KULINDA HIFADHI ZA TAIFA: KIKWETE

Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ulinzi wa hifadhi za Taifa ni pamoja na kutoruhusu mifugo kuchungiwa kwenye hifadhi ili hifadhi hizo endelevu kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo. 

Dkt. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu,  Mara pamoja na washiriki wa Mbio za Serengeti Safari Marathon kutoka mikoa mbalimbali nchini na wengine kutoka nje ya nchi na nje ya bara la Afrika zilizofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.

“Mikoa miwili ya  Simiyu na Mara tu ina ng’ombe zaidi ya milioni tano, tukisema turuhusu mifugo ichungiwe kwenye hifadhi hakuna mnyama atakayebaki na hapo hakutakuwa na hifadhi tena hili siyo suala la kisiasa; sisi viongozi wa kisiasa tukilipigia siasa jambo hili hiyo sifa tunayoisema ya Serengeti kuwa  Hifadhi ya kwanza Duniani haitakuwepo baada ya kuruhusu ng’ombe kuingia kwenye hifadhi,” alisema Dkt. Kikwete.

Aidha, Dkt. Kikwete amewapongeza waandaaji wa Serengeti Safari Marathon kwa namna kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zao jipya la utalii ambayo ikitangazwa vizuri itatangaza utalii nchini na kuweza kulifikia lengo la serikali la kufikisha watalii 5,000,000 ifikapo 2025 kutoka 1,300,000 wa sasa, huku akitoa wito kwa wadau wa utalii kujenga hoteli kwa ajili ya kuwapokea wageni/watalii.

Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 kupitia lango la Ndabaka katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Baadhi ya viongozi wa mikoa ya Simiyu na Mara pamoja na baadhi ya washiriki wakiwa katika mbio fupi za kilomita tano katika mashindano ya Serengeti Safari Marathon Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti  Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon, Bibi. Josien Vergroesien kutoka nchini Netherland, ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.

Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Anthony Mtaka wilayani Busega aliyeshiriki  mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akifurahia jambo na Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 14, 2020  mara baada ya kumpokea katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ( kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.

Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Kikundi cha ngoma kikitoa burudani wakati wa mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Baadhi ya washiriki wa Mbio za Serengeti Safari Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo  katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nane kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kufunga mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.

Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kufunga mashindano ya Mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo  zimefanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha medali mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha medali mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya siasa ya mkoa wa Simiyu (CCM) mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega, Novemba 14, 2020  kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mara, UNDP na waandaaji wa Serengeti Safari Marathon baada ya kufunga  mbio hizo Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Serengeti Safari Marathon Henri Kimambo akiwasilisha taarifa ya mbio za Serengeti Safari  Marathon zilizofanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mara, UNDP na waandaaji waSerengeti Safari Marathon baada ya kufunga  mbio hizo Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka.
Baadhi ya viongozi wa mikoa ya Simiyu na Mara pamoja na baadhi ya washiriki wakiwa katika mbio fupi za kilomita tano katika mashindano ya Serengeti Safari Marathon Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mjasiriamali kutoka Busega Mkoani Simiyu akimkabidhi zawadi Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kufunga mashindano ya mbio hizo ambazo  zimefanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifuatilia matukio mbalimbali katika ufungaji wa mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo  zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya wananchi wa mikoa ya Simiyu na Mara, washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo  zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.







Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!