Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ulinzi wa hifadhi za
Taifa ni pamoja na kutoruhusu mifugo kuchungiwa kwenye hifadhi ili hifadhi hizo
endelevu kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.
Dkt.
Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara pamoja na washiriki wa Mbio za Serengeti Safari
Marathon kutoka mikoa mbalimbali nchini na wengine kutoka nje ya nchi na nje ya
bara la Afrika zilizofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango
la Ndabaka.
“Mikoa
miwili ya Simiyu na Mara tu ina ng’ombe
zaidi ya milioni tano, tukisema turuhusu mifugo ichungiwe kwenye hifadhi hakuna
mnyama atakayebaki na hapo hakutakuwa na hifadhi tena hili siyo suala la
kisiasa; sisi viongozi wa kisiasa tukilipigia siasa jambo hili hiyo sifa
tunayoisema ya Serengeti kuwa Hifadhi ya
kwanza Duniani haitakuwepo baada ya kuruhusu ng’ombe kuingia kwenye hifadhi,”
alisema Dkt. Kikwete.
Aidha,
Dkt. Kikwete amewapongeza waandaaji wa Serengeti Safari Marathon kwa namna kwa
kuanzisha mbio hizo ambazo zao jipya la utalii ambayo ikitangazwa vizuri
itatangaza utalii nchini na kuweza kulifikia lengo la serikali la kufikisha
watalii 5,000,000 ifikapo 2025 kutoka 1,300,000 wa sasa, huku akitoa wito kwa
wadau wa utalii kujenga hoteli kwa ajili ya kuwapokea wageni/watalii.
Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari
Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba
14, 2020 kupitia lango la Ndabaka katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari
Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba
14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Baadhi ya viongozi wa
mikoa ya Simiyu na Mara pamoja na baadhi ya washiriki wakiwa katika mbio fupi
za kilomita tano katika mashindano ya Serengeti Safari Marathon Novemba 14,
2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adam Malima akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne,
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) wakati akitembea kuelekea lango
la Ndabaka katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua
mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti
Safari Marathon, Bibi. Josien Vergroesien kutoka nchini Netherland, ambazo
zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango
la Ndabaka. Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya
sekondari Anthony Mtaka wilayani Busega aliyeshiriki mashindano ya mbio za Serengeti Safari
Marathon katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
(kulia) akifurahia jambo na Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 14, 2020 mara baada ya kumpokea katika Hoteli ya Serenity
On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za
Serengeti Safari Marathon.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete ( kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka
katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua
mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Enock Yakobo mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani
Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari
Marathon. Kikundi cha ngoma kikitoa burudani wakati wa mashindano
ya mbio za Serengeti Safari Marathon yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Baadhi ya washiriki wa Mbio za Serengeti Safari
Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia
lango la Ndabaka. Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha medali mmoja wa washindi wa Serengeti
Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha medali mmoja wa washindi wa Serengeti
Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya siasa ya mkoa wa Simiyu (CCM) mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega, Novemba 14, 2020 kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mara, UNDP na waandaaji wa Serengeti Safari
Marathon baada ya kufunga mbio hizo
Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka. Mmoja wa Wakurugenzi wa Serengeti Safari
Marathon Henri Kimambo akiwasilisha taarifa ya mbio za Serengeti Safari Marathon zilizofanyika Novemba 14, 2020 katika
hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka. Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mara, UNDP na waandaaji waSerengeti Safari
Marathon baada ya kufunga mbio hizo
Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka. Baadhi ya viongozi wa
mikoa ya Simiyu na Mara pamoja na baadhi ya washiriki wakiwa katika mbio fupi
za kilomita tano katika mashindano ya Serengeti Safari Marathon Novemba 14,
2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mjasiriamali kutoka Busega Mkoani Simiyu
akimkabidhi zawadi Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete baada ya kufunga mashindano ya mbio hizo ambazo zimefanyika katika hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Rais mstaafu wa
Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi
mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14,
2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam
Malima, Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifuatilia matukio
mbalimbali katika ufungaji wa mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka. Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya wananchi wa mikoa ya Simiyu
na Mara, washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
0 comments:
Post a Comment