Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Serengeti Safari Marathoni yanayotarajiwa kufanyika tarehe 14 Novemba 2020 kuanzia lango la Ndabaka wilayani Busega mkoani Simiyu
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Novemba 12, 2020 ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amesema mbio hizo zitahusisha mikoa miwili ya Simiyu na
Mara na akatoa wito kwa wananchi wa
mikoa ya hiyo kujitokeza kwa kushiriki katika mbio hizi ambazo zinalenga
kutangaza hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo asilimia 70 ipo mkoa wa Mara na
asilimia 30 ipo mkoa wa Simiyu.
“Mhe.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atakuwepo hapa tarehe 13/11/2020, tarehe 14/11/2020
ataanzisha rasmi mbio hizo na atashiriki mbio za kilomita tano na baadaye
ataongoza uvalishaji wa medali kwa wachezaji na washiriki watakaokuwepo kwenye
mbio ndefu,” alisema Mtaka.
Kwa upande wake Mkurungenzi wa Serengeti Safari Marathon Bw.Timothy Mdinka amesema lengo kubwa la Serengeti Safari Marathon ni kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi ambapo amebainisha kuwa Mbio hizi zimeanza tarehe 12/11/20 na Kilele chake ni 14/11/2020.
Kutakuwa na aina nne za mbio; ambazo ni kilomita 42 (Half Marathon), Kilomita 21 (Half Marathon), Kilometa 10 (Executive Run) na kilomita tano (Fun Run); kwa washindi zinategemeana na aina ya Mbio, Zawadi zitaanzia Tsh. 100,000/= hadi Tsh.600,000/=, ,” alisema Mdinka.
Mdinka ameongeza kuwa wanatarajia kuwa na washiriki takribani 800, kutoka mikoa yote nchini, ,Afrika Mashariki
na Ulaya ya Mashariki ambapo pia amebainisha kuwa kutakuwa na mbio za watoto,
lengo likiwa kuwahamasisha watoto wawe wakimbiaji wazuri wa baadaye.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment