Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amewahakikishia wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Bulumbaka uliopo katika kijijj cha Gasuma wilayani Bariadi mkoani hapa kuwa watapata leseni za uchimbaji na kusisitiza kuwa kamwe hawataondolewa katika mgodi huo.
Prof. Msanjila ameyasema hayo jana Novemba 23, 2020 wakati akizungumza katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi na baadhi ya wachimbaji wadogo, katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
"Muombe leseni mtapewa, leseni haiwezi kutolewa kwa mtu kutoka huko aliko halafu hawa vijana ambao wanachimba sasa hivi wakaondolewa hapana; najua kuna maombi nayaonaona kwenye mitandao lakini msiwe na wasiwasi hayawezi kutoka," alisema Prof. Msanjila.
Aidha, Prof. Msanjila ameeleza utaratibu wa fidia kwa wenye mashamba "tusiichukulie kwamba kwa kuwa na shamba unakuwa na haki ya kuchimba, hapana; ila ni kwamba wale wanaochimba hawana fedha ya kukufidia, sasa tumeweka utaratibu kwamba fidia yako uipate taratibu kwenye mgao na naamini huwa ni nyingi kuliko fidia nyingine.”
Katika hatua nyingine Prof. Msanjila amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuanzisha upya mchakato wa kumpata msimamizi wa mgodi wa Bulambaka ambaye atahakikisha ulinzi unaimarishwa, mazingira yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa vyoo pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri miongoni mwa wachimbaji.
Awali baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba walisilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika mgodi huo ikiwa ni pamoja na kuomba uboreshaji wa miundombinu na upatikanaji wa huduma muhimu, ambapo Msanjila amebainisha kwamba Serikali inazifanyia kazi na baadhi zitatatuliwa na msimamizi wa mgodi huo baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata ambao utaanzishwa Mkuu wa Wilaya.
“Wachimbaji tumewekeza gharama kubwa sana, tunaomba serikali isaidie kuimarisha ulinzi na usimamizi wa mali tunazochimba na kuendelea kuboresha miundombinu ili tuweze kusafirisha mali tunazochimba hapa kwa urahisi,” alisema mchimbaji mdogo Wibelo Kihalata.
“Wenye Maeneo tuliomba leseni ili na sisi tuweze kufanya kazi na Watanzania wenzetu, tunashukuru kwa kuwa mmetueleza kuwa hata sisi tukijiunga tunaweza kupata leseni tukachimba na siyo wenye hela peke yao tu,” alisema Masuke Sahani Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja Bulumbaka Bariadi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema atahakikisha mchakato wa kumpata msimamizi wa mgodi linafanyika kwa uwazi na kusimamia uendeshaji wa mgodi huo kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo kutoka wizara ya Madini.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga
amesema Serikali ya mkoa wakati wowote itahakikisha inasimamia Serikali ya
wilaya katika kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika zinafuata sheria, kanuni
na taratibu.
MWISHO
Mchimbaji mdogo, Bw. Wibelo Kihalata akichangia hoja katika kikao
cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi
wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa
mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba
katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiagana na baadhi ya wananchi baada ya kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi
Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba
katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, akiwasilisha taarifa
katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu
wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma
wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiagana na
baadhi ya wananchi baada ya kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt.
Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi
ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji
cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba
katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt.
Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi
ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji
cha Gasuma wilayani Bariadi.
0 comments:
Post a Comment