Kampuni ya
Simu za Mkononi ya TIGO Mkoa wa Simiyu imetoa msaada wa karatasi kwa ajili ya
maandalizi ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mkoani hapa, unaotarajia
kufanyika kuanzia tarehe 23 Novemba, 2020.
Akikabidhi msaada huo jana kwa niaba
ya Meneja wa TIGO Mkoa wa Simiyu, msimamizi wa Duka la TIGO Bariadi Mjini Bi.
Anna Kazimoto amesema msaada huo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya
kampuni hiyo na Mkoa wa Simiyu huku akitoa rai kwa wanafunzi kusoma kwa bidii
ili waweze kufikia malengo yao.
“Tumetoa msaada huu ili ninyi ndugu
zetu msome msiwe na uhaba wa karatasi kwa ajili ya kuchapisha mitihani na
majaribio kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne, tumetoa
rimu 45 zenye thamani ya shilingi 450,000/=” alisema Bi. Anna Kazimoto.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo
Simime ameishukuru kampuni ya simu ya Tigo na kuahidi kutumia msaada huo kwa
matumizi yaliyokusudiwa.
Nao wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Simiyu wameishukuru Tigo kwa msaada huo na kuahidi kuwa msaada huo utawasaidia
kufikia malengo yao ikiwa ni pamoja na kujiandaa vema na mtihani waTaifa kwa
kuwawezesha kupata karatasi kwa ajili ya kujibia majaribiao ya mara kwa mara
kuelekea Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne.
“Mitihani inahitaji maandalizi
msaada huu utawasaidia sana kidato cha nne kuondokana na uhaba wa karatasi kwa
ajili ya kufanya mitihani na majaribio, tunawashukuru sana Tigo na tunaamini
dada zetu na kaka zetu watafanya vizuri na hiyo itakuwa ni sehemu ya shukrani
kwa Tigo,” alisema Kuyala Lameck kutoka Shule ya sekondari Simiyu.
Kwa upande wake Mwalimu Kulwa
Mtanzania ameishukuru Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo kwa msaada huo na
kutoa wito kwa kampuni hiyo kuendelea kuwa mdau muhimu wa elimu wa mkoa wa
Simiyu.
MWISHO
Mwakilishi
wa Meneja wa Kampuni ya Simu za mkononi mkoa wa Simiyu, Bi. Anna Kazimoto
akikabidhi msaada wa karatasi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari
Simiyu Mjini Bariadi Novemba 06, 2020 waliopokea msaada huo kwa niaba ya wenzao,
ambao umetolewa kwa ajili ya kusaidia katika maandalizi ya mtihani wa kidato
cha nne. Mwakilishi
wa Meneja wa Kampuni ya Simu za mkononi mkoa wa Simiyu, Bi. Anna Kazimoto
akikabidhi msaada wa karatasi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari
Simiyu Mjini Bariadi Novemba 06, 2020 waliopokea msaada huo kwa niaba ya wenzao,
ambao umetolewa kwa ajili ya kusaidia katika maandalizi ya mtihani wa kidato
cha nne. Baadhi ya wanafunzi wa
Shule ya sekondari Simiyu wakifuatilia mapokezi ya msaada wa karatasi ulitolewa
na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani
Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa
unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020 Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akimshukuru mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo baada ya makabidhiano ya msaada wa karatasi uliotolewa na kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020.
Baadhi ya karatasi ziliotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020Afisa Elimu Taaluma
mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akiteta jambo na wawakilishi wa Kampuni ya
simu za mkononi ya Tigo baada ya makabidhiano ya msaada wa karatasi uliotolewa
na kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa
ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020. Afisa Elimu Taaluma
mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akizungumza na wanafunzi wa Shule ya
sekondari Simiyu (hawapo pichani) Novemba 06, 2020 wakati wa makabidhiano ya msaada wa karatasi uliotolewa na Kampuni
ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa Kidato
cha nne unaotarajiwa kuanza Novemba 23,
2020
0 comments:
Post a Comment