Mwandishi wa Vitabu Bw. Richard
Mabala ametoa msaada wa nakala 120 za vitabu
vya fasihi vya "Hawa The Bus Driver" na "Mabala the Farmer
" kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili katika shule za
Mkoa wa Simiyu.
Akikabidhi msaada huo Novemba 06, 2020 kwa wanafunzi wa shule ya
sekondari Bariadi kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Afisa Elimu
Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime amewataka wanafunzi hao kujisomea
vitabu hivyo wapate maarifa yatakayowasaidia katika mitihani yao na maisha kwa
ujumla ili kutimiza kusudi la mtoa msaada huo.
“Mvitumie vitabu hivi vizuri,
mkijenga tabia ya kujisomea kuanzia kidato cha kwanza na cha pili mtakapofika
kidato cha tatu na cha nne fasihi kwenu itakuwa rahisi kwenu; hakikisheni
mnautumia msaada huu vizuri msome na siku moja akija Simiyu tutamleta awaulize
maswali,” alisema Simime.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa
Shule, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba amemshukuru
Mwandishi wa Vitabu Ndg. Richard Mabala ambapo amesema wameupokea msaada huo
kwa mikono miwili huku akimhakikishia kuwa vitabu hivyo vitasomwa na wanafunzi
na vitasaidia kuongeza ufaulu katika mitihani yao.
Nao wanafunzi wa Shule ya sekondari
Bariadi wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wao wa mkoa wa Simiyu wameshukuru
kupata msaada huo na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Tunamshukuru sana Mabala kwa msaada
wake na tumeupokea kwa mikono miwilitunaahidi tutasoma kwa bidii vitabu hivyo
na vitatusadia kujibu maswali ipasavyo ili tuweze kufaulu katika mitihani yetu,”
alisema Kija Nyerere mwanafunzi wa kidato cha Kwanza Bariadi sekondari.
“Msaada huu una faida sana kwetu
maana vitabu vinaelimisha, vinaburudisha naamini tutafanya vizuri katika
mitihani yetu kwa sababu pia itatusaidia kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kuachana na mila potofu,” alisema mwakilishi wa wanafunzi wa kidato
cha pili shule ya sekondari Bariadi.
MWISHO
Afisa Elimu Taaluma
mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa kidato cha
pili katika shule ya sekondari Bariadi nakala ya kitabu ikiwa ni sehemu ya vitabu 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine. Baadhi ya wanafunzi
kutoka shule ya sekondari Bariadi wakionesha nakala za vitabu walivyopokea
ikiwa ni sehemu ya vitabu 120 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine. Baadhi ya wanafunzi
kutoka shule ya sekondari Bariadi wakiangalia nakala za vitabu walivyopokea ikiwa ni sehemu
ya vitabu 120 120 vilivyotolewa msaada
na Mwandishi wa Vitabu Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa
Novemba 06, 2020 shuleni hapo kwa niaba ya shule nyingine. Baadhi ya wanafunzi
kutoka shule ya sekondari Bariadi wakionesha nakala za vitabu walivyopokea
ikiwa ni sehemu ya vitabu 120 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine, aliyesimama mbele kulia ni Afisa Elimu wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi. Baadhi ya wanafunzi
kutoka shule ya sekondari Bariadi wakiangalia nakala za vitabu walivyopokea ikiwa ni sehemu
ya vitabu 120 vilivyotolewa msaada na
Mwandishi wa Vitabu Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa
Novemba 06, 2020 shuleni hapo kwa niaba ya shule nyingine. Mkuu wa Shule ya
Sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba akiwagawia nakala za vitabu ikiwa ni sehemu
ya vitabu 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine. Afisa Elimu Taaluma
mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa kidato cha
pili katika shule ya sekondari Bariadi nakala ya kitabu ikiwa ni sehemu ya vitabu 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine. Afisa Elimu Taaluma
mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa kidato cha
pili katika shule ya sekondari Bariadi nakala ya kitabu ikiwa ni sehemu ya vitabu 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine. Afisa Elimu Taaluma wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi akizungumza na
wanafunzi wa Shule ya sekondari Braiadi (hawapo pichani) Novemba 06, 2020
wakati wa makabidhiano ya msaada vitabu
vya fasihi vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu Richard Mabala kwa mkoa
wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni hapo kwa niaba ya shule
nyingine. Baadhi ya wanafunzi
kutoka shule ya sekondari Bariadi wakionesha nakala za vitabu walivyopokea
ikiwa ni sehemu ya vitabu 120 120 vilivyotolewa msaada na Mwandishi wa Vitabu
Richard Mabala kwa mkoa wa Simiyu ambavyo vimepokelewa Novemba 06, 2020 shuleni
hapo kwa niaba ya shule nyingine, aliyesimama mbele kulia ni Afisa Elimu wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
0 comments:
Post a Comment