Monday, November 16, 2020

SIMIYU KUFANYA MAJARIBIO KUTUMIA VYETI VYA VYUO VIKUU KUDHAMINI MIKOPO

Katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya majaribio ya kutumia vyeti vya taaluma kwa wahitimu wa vyuo vikuu kama dhamana ya mikopo ili kuwawezesha  kupata mitaji na kujiajiri kupitia sekta ya kilimo na viwanda. 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alipokutana na baadhi ya vijana jana Novemba 15, 2020 mjini Bariadi kwenye mjadala wa ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo ambao ulihudhuriwa pia na wadau wa maendeleo akiwemo  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi.

“Tunataka (tu pilot) tufanye majaribio na tutakuwa (number one) wa kwanza, tutawafuata wadau (UNDP) kuwaeleza kuwa tumekuja na namna ya kuwasaidia vijana waliomaliza vyuo vikuu ili tuone kama vyeti vyao vinaweza kusimama kama dhamana badala ya vyumba na viwanja ambavyo wao hawana,”

“Tutawaambia vijana hao wenye maandiko ya miradi  wawasilishe iwe ni kwa mtu binafsi au kikundi, tutajadiliana tuone ‘risk’ zikoje,” alisema Mtaka.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bibi. Christine Musisi ametoa wito kwa vijana kuhamasika kubadili mitazamo kutoka kwenye mawazo tegemezi kwenda katika mawazo ya kujitegemea wenyewe na kwenda mbele zaidi kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka, huku akiahidi kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na Mkoa wa Simiyu kama mdau wa maendeleo.

Baadhi ya vijana wametoa mapendekezo mbalimbali ambayo yakifanyiwa kazi na serikali, vijana wenyewe na wadau wengine yataweza kuchangia kuleta ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana.

“Tunaomba Serikali ituboreshee miundombinu ya kilimo tutoke kwenye kilimo cha kutegemea mvua twende kwenye kilimo cha umwagiliaji ili tuzalishe malighafi ya kupeleka viwandani,” alisema Adrian Paul.

“Njia nyingine ya kuongeza ajira kwa vijana na Serikali kufufua viwanda vilivyokufa na kuanzisha viwanda vipya ili iweze kuzalisha ajira kwa rika zote wakiwemo vijana,” alisema Afisa Vijana Itilima

“Elimu ya kujitegemea irudishwe na ianze kufundisha mashuleni ili kuwaanda watoto tangu wakiwa wadogo kujitegemea ili hata atakapomaliza masomo akakasa ajira aweze kujiajiri mwenye na kujitegemea,” alisema Asia Kimaro kutoka Wilayani Maswa.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka UNDP, Bw. Amon Manyama ameahidi kushirikiana na mkoa wa Simiyu katika maandiko ya miradi huku akitoa wito kwa vijana kujituma na kutokuridhika kwa kufanya kazi moja badala yake kila mmoja aone umuhimu wa kuwa kazi zaidi ya mbili.

MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa huo katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa wa Simiyu katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Asia Kimaro mmoja wa Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka (wa saba kulia), katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga,  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), Bibi. Christine Musisi (wa sita kulia), baadhi ya vijana wasomi kutoka maeneo mbalimbali na baadhi ya maafisa kutoka UNDP kabla ya kushiriki mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Afisa Vijana wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Zena Mchujuko akiwasilisha maada katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mwandishi wa vitabu na Mtumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa wa Simiyu katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa Vijana akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi ukihusisha baadhi ya vijana na wadau wa maendeleo .
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP), akizungumza na baadhi ya vijana wasomi kutoka mikoa mbalimbali nchini juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi mkoani Simiyu.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa huo katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa Vijana akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi ukihusisha baadhi ya vijana na wadau wa maendeleo .
Mkurugenzi wa Jembe ni Jembe Company Limited,  Dkt. Sebastian Ndege akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa Vijana akichangia hoja katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi ukihusisha baadhi ya vijana na wadau wa maendeleo .
Mmoja vijana wasomi kutoka mkoa wa Mara, Dkt. Makaranga akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mgunduzi na mmiliki wa dawa ya kuua wadudu ya Vuruga,  Dkt. Neva  akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya vijana wasomi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Kijana Msomi na Mjasiriamali kutoka  jijini Dar es salaam Bi. Juliana Mataba akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka UNDP, Bw. Amon Manyama akizungumza na baadhi ya Vijana  wa mkoa wa Simiyu katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.

Mmoja wa wadau wa  maendeleo wa mkoa wa Simiyu, Bw. Joshua Mirumbe akizungumza na  baadhi ya vijana wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuwahamsisha(motivating), katika mjadala kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya vijana wasomi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi na baadhi ya wadau  juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana  na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi akizungumza na baadhi ya vijana wasomi juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, katika mjadala uliofanyika jana Mjini Bariadi.
Mgunduzi na mmiliki wa dawa ya kuua wadudu ya Vuruga,  Dkt. Neva  (kulia) akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa(UNDP),  Bibi. Christine Musisi juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na mapendekezo ya suluhisho la changamoto hiyo, katika mjadala uliofanyika jana Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!