Takribani
vijana 664 mkoani Simiyu wanatarajia kunufaika
na ajira za muda katika msimu huu
,baada ya kupata mafunzo ya matumizi sahihi ya
viuatilifu kwa ajili ya kukabiliana na wadudu wasumbufu wa zao la Pamba.
Hayo
yamebainishwa jana Novemba 24, 2020 wakati wa kufunga mafunzo ya matumizi
sahihi ya viuatilifu kwa wapuliziaji sumu katika zao la pamba yaliyotolewa na
Gatsby Africa kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu
(TPRI) katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu ambayo yalihitimishwa na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga.
Vijana hao
wamebainisha mafunzo waliyoyapata pamoja na kuwasaidia kupata ajira
yatawawezesha kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba kwa kuwa wamefahamu
matumizi sahihi ya viuatilifu ilinganishwa na awali walipokuwa wakifanya kazi
hiyo kienyeji.
“Tulikuwa
tunafanya kienyeji lakini kwa sasa tumepata ujuzi mfano tumejifunza ni dawa ipi
inatumika kuua aina gani ya wadudu kwa wakati gani; lakini pia tumejifunza ni
kwa namna gani tunaweza kutumia viuatilifu pasipo kuathiri mazingira yetu,”
alisema Samwel Salum mpuliziaji viuatilifu vya zao la pamba Meatu.
“Mafunzo haya
kwangu yana umuhimu mkubwa sana maana nitakuwa nikipulizia viuatilifu kwenye
mashamba ya wakulima napata hela, lakini pia nitatumia mbinu nilizojifunza
kupulizia kwenye mashamba yangu na nitaongeza uzalishaji,” alisema Mayunga
Mlyaza mpuliziaji viuatilifu vya zao la pamba Meatu.
Afisa Kilimo wa
Kata ya Sakasaka Wilayani Meatu, Sylvester Mholi amesema mafunzo hayo
yamewaongezea uwezo wa kujiamini katika kutambua viuatilifu ambavyo
vinasambazwa na wasambazaji kwa kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali
inayohitajika.
Mwakilishi wa
Gatsby Africa shirika lililoshirikiana na Mkoa kuandaa mkakati wa mapinduzi
kilimo cha pamba (2019-2024) katika mafunzo hayo Bw.Michael Kahindi amesema wakulima waliofikiwa na
wapuliziaji hawa wa viuatilifu katika msimu uliopita wamefanikiwa kuongeza tija
katika Uzalishaji wa pamba kutoka kilo 250 mpaka kufikia kilo 600 kwa hekali.
Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesisitiza uadilifu wakati wa
utekelezaji zoezi la upuliziaji dawa katika mashamba ya wakulima “tusifanye
udanganyifu kwa wakulima, ukimdanganya mteja wako kesho hatarudi tena kwako;
sisi kama mkoa tunaona fahari kuwa tunao vijana 664 ambao tumewaongezea thamani
kwenye kazi walizonazo.”
Mtafiti wa kudhibiti visumbufu vya
mazao/mimea kutoka Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu nchini(TPRI), Bw. Ramadhan
Kilewa amesema matarajio ya TPRI ni kuwa vijana hao wataenda kufanya kazi nzuri
baada ya mafunzo hayo kwa kuwa awali baadhi yao walieleza kuwa walikuwa
wakifanya kazi hiyo tofauti na maelekezo ya matumizi sahihi ya viuatilifu.
Kwa uapnde wake kaimu Katibu Tawala Msaidizi-Seksheni
ya Uchumi na Uzalishaji, Bibi. Kija Kayenze amesema “Lengo ni kuongeza tija
hivyo tunatarajia tija itaongezeka sana kwa sababu wakulima wengi watakauwa
wameshapata elimu sahihi ya matumizi ya viuatilifu
MWISHO
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Meatu, Bw. Albert Rutaihwa akizungumza na baadhi ya vijana
wanaotarajiwa kupata ajira za muda upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba
wakati Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifunga mafunzo
hayo Novemba 24, 2020 Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu.
Baadhi ya
vijana waliopewa mafunzo ya upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba
wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakati akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini
Mwanhuzi wilayani Meatu.
Baadhi ya
vijana waliopewa mafunzo ya upuliziaji wa viuatilifu katika zao la pamba
wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakati akifunga mafunzo hayo Novemba 24, 2020 Mjini
Mwanhuzi wilayani Meatu.
0 comments:
Post a Comment