Changamoto ya upungufu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa mkoani Simiyu imepungua kutoka asilimia 57 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 34 mwaka 2019 kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na viongozi, watendaji na wananchi, ikiwa ni pamoja na kulipa kipaumbele suala la lishe.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige wakati
akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika
jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.
Magige
amesema Elimu ya kujirudiarudia imewafanya wananchi wapate uelewa wa kutosha
juu ya ulaji sahihi ambapo amesisitiza kuwa pamoja na elimu mkoa uliweka
mkakati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuongeza nguvu katika katika
utoaji wa vidonge vya kuongeza damu kwa wasichana.
“Suala
la lishe limepewa kipaumbele katika mkoa wetu na elimu inaendelea kutolewa
katika vituo vya kutolea huduma za afya, ngazi ya jamii ambapo wanawake
wanafundishwa kuandaa chakula kwa usahihi katika makundi yote matano ya
vyakula,” alisema Dkt. Magige.
Katika
hatua nyingine Magige amesema katika kukabiliana na udumavu mkoani Simiyu, Mkoa
umejiwekea mikakati kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya namna ya kuandaa
vyakula vya kuwalisha watoto walio vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya
jamii, elimu ya unyonyeshaji sahih, elimu ya mabadiliko ya ulaji na kuhimiza
wananchi kwenda kuapata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza
na wajumbe wa kamati ya lishe ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bibi.
Miriam Mmbaga ametoa rai kwa viongozi na watendaji kuendelea kutimiza wajibu
wao na kila mmoja kutambua kuwa suala la lishe ni la muhimu huku akisisitiza
ushirikiano ili kuwaokoa wananchi wa mkoa wa Simiyu kuondokana na athari
zitokanazo na lishe duni.
Kwa
upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bi. Happiness
Kubona amesema Maafisa Lishe wataendelea kuwajengea uwezo wahudumu wa afyangazi
ya jamii, ngazi ya vituo kuwatambua watoto wenye utapiamlo na kuwaingiza katika
matibabu .
Ameongeza
kuwa hamasa ya kujiunga na Mfuko Afya ya Jamii ulioboreshwa(ICHF) kwa wananchi itaendelea
kutolewa ili waweze kupata huduma za matibabu na hususani wanawake waweze kupata huduam ya
vidonge vya kuongeza damu ili wasipungukiwa damu wakati wa ujauzito.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kamati ya lishe mkoa kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi
Mdauwa Lishe kutoka shirika lisilo la kiserikali la CUAMM akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi, kushoto ni Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
akichangia hoja katika kikao cha kamati ya lishe mkoa kilichofanyika jana
Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment