Saturday, January 30, 2021

WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO YA ASILIMIA MBILI KUTOKA HALMASHAURI

 

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe.Ummy Nderiananga amewataka watu wenye ulemavu nchini kujitokeza kuchukua mikopo inayotolewa na halmashauri bila riba kutoka katika asilimia mbili ya mapato ya ndani ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na adha ya kutumikishwa kama omba omba. 

Mhe. Nderiananga ametoa wito huo jana Januari 29, Mjini Bariadi wakati alipokutana na kuzungumza na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu akiwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Simiyu, iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu..

" Licha ya baadhi ya Halmashauri kufanya vizuri katika kutenga fedha kwa ajili ya watu wenye ulemavu, kuna taarifa kuwa baadhi yenu mmekuwa waoga kukopa fedha zinazotengwa kwa ajili yenu, nitoe rai kwenu tumieni fursa hiyo kopeni ili mpate mitaji ya kuwasaidia kufanya shughuli za kuwaingizia kipato, fedha hizi ni kwa ajili yenu na Serikali imefanya kazi kubwa sana ili mpate fedha hizi,” alisema Nderiananga. 

Katika hatua nyingine Nderiananga amewaasa watu wenye ulemavu wanaochukua mikopo hiyo kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa miongozo na taratibu za utoaji wa mikopo hiyo ili kutoa fursa kwa kila mmoja anayehitaji  mikopo hiyo kuipata kwa wakati. 

“Natoa wito kwa watu wenye ulemavu ambao mmekuwa mkikopeshwa fedha itokanayo na asilimia mbili ya mapato ya ndani ya halmashauri kurejesha nawaomba msile, mkila mtafanya watu wenye ulemavu wasiaminike,” alisema Nderiananga 

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa viungo (CHAWATA) Mkoa wa Simiyu, Bw Gera Makasi ameomba Viongozi na wataalam kutoka Serikalini waendelee kutoa elimu juu ya mikopo hiyo ili watu wenye ulemavu wapate uelewa mpana juu ya namna mikopo hiyo inavyotolewa, inavyorejeshwa na namna sahihi ya kuitumia kwa manufaa. 

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu unawajali sana watu wenye ulemavu  huku akibainisha kuwa Simiyu imejipanga kuanzisha namna ya tofauti (unique model) ya utoaji wa mikopo kwa watu wenye ulemavu, wanawake na vijana ili mikopo itolewayo kutoka katika asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri iwe na tija kwa makundi lengwa ( watu wenye ulemavu asilimia mbili, vijana asilimia nne na wanawake asilimia nne)

Akitoa taarifa ya mkoa kwa Naibu Waziri, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amesema watu wenye uemavu mkoani hapa wamekuwa wakishirikishwa katika shughuli za kijamii na uhamasishaji unaendelea kufanyika ili waweze kuunda vikundi kurahisisha upatikanaji wa mikopo, ambapo  mpaka sasa takribani vikundi 45 vya watu wenye ulemavu vimeshaundwa.

Aidha , Mujungu ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka 2020/2021  kiasi cha shilingi milioni mia mbili na laki sita kimetengwa katika halmashauri zote sita za mkoa wa Simiyu (Bariadi Mjini, Bariadi Vijijini, Busega, Itilima, Maswa na Meatu)  kwa ajili ya kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu.

MWISHO 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya siku moja mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Mmoja wa wakalimani wa lugha ya alama mkoani Simiyu akitafsiri hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga kwa viziwi wakati akizungumza na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi akiwa katika  ziara yake ya siku moja mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi , Mhe. Festo Kiswaga akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa watu wenye Ulemavu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Jacob Mwinula katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA)  Mkoa wa Simiyu, Bi. Josephine Shimula akitoa taarifa ya shirikisho hilo katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Bi. Rachel Buluba kutoka wilayani Bariadi akiwasiliha hoja yake katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga katika kikao cha Naibu waziri huyo na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi , Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakifuatilia kikao cha Naibu waziri huyo na viongozi wa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu jana Januari 29, 2021 Mjini Bariadi, wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo  mkoani hapa iliyolenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu mara baada kuhitimisha ziara yake jana Januari 29, 2021 mjini Bariadi ambayo ililenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga(mwenye mtandio wa njano) akifurahia jambona baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na badhi ya watu wenye ulemavu mara baada ya kuhitimisha ziara yake jana Januari 29, 2021 mjini Bariadi ambayo ililenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ule

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, baadhi ya maafisa na baadhi ya watu wenye ulemavu mara baada kuhitimisha ziara yake jana Januari 29, 2021 mjini Bariadi ambayo ililenga kufanya ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu.

PICHA ZAIDI KATIKA ZIARA YA NAIBU WAZIRI NDERIANANGA

Thursday, December 17, 2020

RC SIMIYU ASITISHA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI MGODI WA LUBAGA

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesitisha matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika mgodi wa Dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake katika uendeshaji wa shughuli za madini.

 

Mtaka ametoa uamuzi huo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika eneo la mgodi Desemba 17, 2020 akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kwa ajili ya kwenda kusikiliza kero za wachimbaji wadogo mgodini hapo na kuzitafutia ufumbuzi.

 

“Sisi kama viongozi wa mkoa tunasitisha matumizi ya leseni za eneo lote hili, mpaka pale waziri mwenye dhamana atakapokuja kutoa ufafanuzi kwa wananchi, kwa sababu sheria inamtamka waziri kwenye kufuta leseni lakini sisi mkoa kwa tuliyoyaona hapa tunasitisha; kwa sasa  mgodi utaendelea kuwa chini ya usimamizi wa maelekezo ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa,” alisema Mtaka.

 

Aidha, Mtaka amesema Maafisa kutoka katika Ofisi zote zinazopaswa kutoa huduma kwa wachimbaji hao ikiwa ni pamoja na maafisa wa Soko la Madini kuanzia Desemba 18, 2020 watakuwa katika eneo la mgodi ili kuwapunguzia wachimbaji hao adha ya kufuata huduma mbali na eneo hilo huku akisisitiza wachimbaji hao wauze dhahabu kwa bei iliyopo sokoni.

 

Mtaka pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Bariadi na Busega kufanya tathmini ya mashamba yaliyoharibiwa na shughuli zinazoendelea katika eneo la mgodi ili wakulima hao waweze kulipwa fidia, huku akiwataka Wakurugenzi hao  pia kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa matundu ya vyoo yasiyopungua 12 kuimarisha hali ya usafi mgodini.

 

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa onyo kwa wachimbaji na watu wote wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji madini kujiepusha na utoroshaji wa dhahabu, kwamba  watakapobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutaifisha dhahabu hiyo.

 

Awali wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wamiliki wa maduara  waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye mgodi huo ambazo baadhi zilipatiwa ufumbuzi  na uongozi wa mkoa na baadhi zitashughulikiwa na Waziri mwenye dhamana ya madini.

 

“Usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwenye mgodi huu uimarishwe zaidi, ili Serikali ipate sehemu yake, wachimbaji na sisi tupate sehemu yetu na kila tozo au ushuru wanaotutoza wahakikishe wanatoa risiti za kielektriniki,” alisema Flugence Ekondo mchimbaji mdogo.

 

“Katika ugunduzi wa mgodi huu mke wangu alikuwa anapalilia mahindi akaokota jiwe, alivyolileta tulikuwa na wasiwasi nalo tukalipeleka mgodi wa Gasuma tukaambiwa ni dhahabu, hiyo ilikuwa tarehe 05/11/2020 kesho yake wachimbaji wakaanza kuchimba na mgao ukafanyika; binafsi nilijua hiyo itakuwa rashi itakayotunufaisha wachimbaji wadogo na jamii inayotuzunguka,lakini baadaye tukasikia kuna leseni tunaomba tusaidiwe na sisi tupate haki yetu kwenye mgao,” Ntimba Masalu mwakilishi wa wenye mashamba

 

Akitoa ufafanuzi kuhusu mgao, Afisa madini Mkazi wa Mkoa, Mhandisi. Oscar Kalowa amesema “katika mifuko 100 asilimia saba ni fedha ya serikali, wamiliki wa mashamba asilimia 15, msimamizi/mmiliki wa leseni asilimia 15 na mwenye duara husika anapata asilimia zinazobaki na huu ndiyo utaratibu unaohusika.”

MWISHO

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesitisha matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika mgodi wa Lubaga uliopo mpakani mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake katika uendeshaji wa shughuli za madini.

Baadhi ya wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa  Wilaya ya Bariadi na Busega, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipotembelea mgodi huo akiwa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia walioketi) akiwa na baadhi viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo (waliosimama) katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa  Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Kutoka kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhe. Enock Yakobo,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakiteta jambo  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

:-Afisa Madini Mkazi mkoa wa Simiyu, Oscar Kalowa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Majengo kilichopo Kata ya Dutwa wilayani Bariadi akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakielekea kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika eneo la Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Debora John mmoja wa wachimbaji wadogo  kwenye Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega katika mktano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo hilo, Desemba 17, 2020.

Mmoja wa wachimbaji wadogo  kwenye Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega katika mktano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo hilo, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Festo Kiswaga  akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020


Baadhi ya wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa  Wilaya ya Bariadi na Busega, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipotembelea mgodi huo akiwa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakielekea kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika eneo la Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Wednesday, December 16, 2020

WAZIRI WA KILIMO PROF. MKENDA, NAIBU WAZIRI TAMISEMI DKT DUGANGE WANOGESHA RCC SIMIYU

 

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda na Naibu  Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange wameshiriki kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), ambapo walitumia fursa hiyo kuwasilisha masuala ya kilimo na afya kwa viongozi wa chama na serikali, wakuu wa Taasisi za Umma na binafsi, viongozi wa Dini na wadau wengine wa maendeleo.

 

Akizungumzia kuhusu kilimo cha zao la pamba katika kikao hicho kilichofanyika Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara ya kilimo itafanya mapitio ya  mifumo mbalimbali ya kitaasisi ili kuongeza tija katika  uzalishaji wa pamba kufikia lengo la kuzalisha tani milioni moja ndani ya miaka mitano ijayo.

Miongoni mwa mifumo aliyoibainisha Profesa Mkenda ni pamoja na mfumo wa kushughulikia pembejeo za kilimo huku akibainisha kuwa Wizara yake  inaendelea kufanya uchunguzi ili kuona kama uwezekano wa kuzalisha viuatilifu  nchini ili kupunguza uagizaji wa viuatilifu kutoka nje ya nchi na kuweza kudhibiti ubora wa viuatilifu hivyo.

“ Katika kufikia tija kwenye zao la pamba pia tunapitia upya na kwa haraka sana mfumo mzima wa kitaasisi wa kuzalisha na kugawa mbegu za pamba, utaratibu mpya hautakuwa umekamilika kwa kipindi hiki cha msimu huu, lakini tumekusudia na tumekubaliana tutafanya mapitio ili wakulima wapate mbegu bora kwa wakati,” alisema Profesa Mkenda.

Awali Kabla ya kuzungumza katika  kikao hicho Prof. Mkenda, wajumbe wa Kikao cha RCC waliwasilisha changamoto mbalimbali katika kilimo cha pamba ikiwa ni pamoja na tatizo la upungufu wa mbegu na mbegu kutowafikia wananchi kwa wakati.

“Kumekuwa na changamoto ya upungufu wa mbegu kwa wakulima, ninashauri ili mbegu ziwafikie wakulima wote na kwa wakati, makampuni yanayozalisha mbegu yazipeleke kwa Mkurugenzi ambaye ndiye mwenye wataalam wa kilimo wanaofahamu idadi ya wakulima na ukubwa wa maeneo wanayolima,” alisema Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi.

“Pamoja na kutatua changamoto ya pamba, tunaomba serikali iajiri maafisa ugani  ili wananchi waweze kupata huduma za ugani na kuzalisha kwa tija,tutakapozalisha kwa tija tutapata mavuno mengi na mkulima atanufaika pamba yake, suluhisho la bei ya pamba ni kujenga kiwanda cha nguo mkoani Simiyu,” Mhe. Esther Midimu Mbunge Viti Maalum.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ametoa rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Busega, Bariadi na Itilima kuanza kununua vifaa tiba kwenye Hospitali za Wilaya zilizojengwa kwa kutumia mapato ya ndani  huku akibainisha kuwa Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa kila hospitali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Dkt. Dugange pia amesema katika miaka mitano ijayo Serikali ina mpango wa kujenga vituo vya kutolea huduma za afya takribani 655 huku akifafanua kuwa itaanza na ukamilishaji wa maboma yaliyojengwa na kwa nguvu za wananchi na kuomba Halmashauri kuweka mpango wa kuanza kukamilisha maboma hayo.

Dkt.Dugange amesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa mifumo ya ukusanyaji mapato  katika vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo amebainisha kuwa makusanyo yakiwa mazuri yatazipunguzia Halmashauri mzigo wa utegemezi kwa Serikali Kuu na wadau mbalimbali wa afya na kuwezesha vituo hivyo kujiendesha ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kununua dawa.

Akifunga kikao cha RRC Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi hao kushiriki katika kikao hicho, huku akitoa wito kwa viongozi wote wa Mkoa huo kuifanya elimu kuwa ajenda ya kudumu ya mkoa na ujenzi wa vyumba vya madarasa kuwa ni kipaumbele chao cha kwanza ili kila mwanafunzi aliyefaulu aweze kwenda shule.

MWISHO.

 

Waziri wa kilimo, Mhe. Profesa. Adolf Mkenda akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali, wakuuwa Taasisi za Umma na binafsi, viongozi wa Dini na wadau wengine wa maendeleo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu(RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali, wakuu wa Taasisi za Umma na binafsi, viongozi wa Dini na wadau wengine wa maendeleo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia kikao hicho  kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifunga kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu(RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe, Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu(RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiwasilisha taarifa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Leah Komanya akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga wakiteta jambo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega  Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Sheikh wa mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi




Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!