Tuesday, November 28, 2017

RC MTAKA AWAKABIDHI PIKIPIKI NA GARI MAAFISA UGANI ITILIMA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amekabidhi pikipiki za maafisa Ugani na Gari la Idara ya Kilimo  wilayani Itilima na kusisitiza kuwa vyombo hivyo vitumike kwa ajili ya kuwafikia wananchi ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao hususani zao la pamba.

Vyombo hivyo ambavyo awali vilikuwa vimeegeshwa vimefanyiwa matengenezo kwa gharama za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka, aliyoyatoa wakati wa ziara yake  aliyofanya katika Halmashauri zote Mkoani humo kwa lengo la kuhimiza kilimo.

Mtaka amesema zao la pamba linachangia mapato ya Halmashauri kwa kiasi kikubwa Mkoani humo  hivyo Wakurugenzi wanapaswa kuhakikisha vyombo vya usafiri vinafanya kazi muda wote wa msimu ili wataalam waweze kuwafikia wakulima(wananchi) na kuwasaidia kuzalisha kwa tija.

“ Mwaka 2016/2017 Itilima ilipata milioni 500 kutokana na pamba lakini Idara ya Kilimo iliyosababisha Pamba kuleta fedha hizo  haikutengewa fedha kwenye bajeti, haikuwa na gari wala pikipiki” amesema Mtaka.

“ Wakati wa kilimo hakuna  magari kwa ajili ya kuwafikia wakulima, wakati wa kukusanya ushuru magari yote yanakuwa mazima na yanawekwa mafuta ili kufuatilia ushuru, maelekezo yangu kwa Halmashauri zote ni kwamba wakati wote wa msimu wananchi kuanzia wanapoandaa mashamba ni lazima pikipiki na magari yafanye kazi kwenye Idara ya Kilimo ” amesititiza  Mtaka.

Wakipokea pikipiki na gari la Idara Maafisa Ugani hao wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanawafikia wakulima wote walio katika maeneo yao, ili kupitia utaalamu wao waweze kuwasaidia kuongeza uzalishaji, ambapo wamekusudia kuongeza uzalishaji wa pamba kwa mwaka 2017/2018 kutoka kilo 650 hadi 1200 kwa ekari.

Mkoa wa SIMIYU ni mkoa unaozalisha pamba kwa wingi ambapo  unazalishaji asilimia 60 ya pamba yote hapa nchini
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Ugani na Viongozi wa Wilaya ya Itilima (baadhi hawapo pichani) kabla ya kukabidhi pikipiki za Maafisa Ugani na Gari la Idara ya Kilimo , vyote vimetengenezwa na Halmashauri ya Itilima kutekeleza agizo alilotoa wilayni humo wakati wa ziara yake ya kuhamasisha Kilimo. 



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!