Monday, November 25, 2019

WANANCHI SIMIYU WASHAURIWA KUFANYA MAZOEZI, KUACHA ULAJI USIOFAA KUZUIA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kuacha ulaji usiofaa kwa kuacha kutumia vyakula vyenye sukari, mafuta na chumvi nyingi na nafaka zilizokobolewa kwa lengo la kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani.

Dkt Dugange ameyasema hayo Novemba 22, 2019 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza, ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

“ Asilimia 43 ya wagonjwa wanaotibiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya wana matatizo yanayotokana na  magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kutofanya mazoezi kunachangia kwa asilimia 60 magonjwa yasiyoambukiza, hivyo ni vema wananchi wakafanya mazoezi na kuepuka ulaji usiofaa ili kudhibiti magonjwa haya,” alisema Dkt. Dugange.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka watumishi wa idara ya afya mkoani hapa, kuwafikishia wananchi elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi, lishe bora na madhara ya kutumia vilevi kupita kiasi.

Aidha, Sagini amesisitiza wataalam wa afya kuelimisha jamii namna ya kutambua magonjwa yasiyoambukiza kupitia upimaji na kufuatilia watu wenye magonjwa sugu yasiyoambukiza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema atashirikiana na viongozi wengine kusimamia ufanyaji wa mazoezi ya viungo ikiwemo utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi Jumamosi ya pili ya kila mwezi ili kuwahamasisha wananchi kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.

“Tutakachokifanya sasa hivi ni kugawa vituo vya mazoezi ya mara kwa mara kulingana na kanda kwa kuwa mji unakuwa, lakini pia tutaweka viongozi kwa kila kanda, ili kila inapofika Jumamosi ya pili mwezi viongozi wanakuja na watu wao tunajumuika pamoja katika mazoezi,”alisema Kiswaga.

Kwa upande wao watumishi walioshiriki katika mazoezi hayo wamewashukuru viongozi wa Mkoa kwa kuhamasisha watumishi na wananchi kushiriki mazoezi haya, kwa sababu wanatumia muda mwingi kazini wakiwa wamekaa hali inayoweza kuchangia wao kupata magonjwa yasiyoambukiza, hivyo wakaomba utaratibu huo uwe endelevu na waahihidi kushiriki kila wakati ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

“Watumishi wengi tumekuwa tukijihusisha  zaidi na shughuli zetu za kikazi tunasahau na wakati mwingine tunashindwa  kufanya mazoezi ambayo ni muhimu kwa afya zetu na ufanisi wa kazi zetu, ninashukuru viongozi wetu kuandaa na kufanikisha zoezi hili na sisi kama watumishi tunaahidi kuwa suala hili litakuwa endelevu,” alisema Marko Igenge mtumishi idara ya afya.

Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi na utaratibu wa kufanya mazoezi ya viungo utaendelea kufanyika kila Jumamosi ya pili katika kila mwezi.
MWISHO

Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi  na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi  na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi  na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.


Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi  na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi  na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

.

Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu(wenye jezi za zambarau) na timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa(wenye jezi nyeupe) wakicheza mechi ya kirafiki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa umma na wananchi, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na watumishi wa umma na wananchi, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.




Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(mwenye fulana ya mistari)  akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu kabla ya mechi ya kirafiki iliyochezwa kati ya timu hiyo na timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(mwenye fulana ya mistari)  akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kabla ya mechi ya kirafiki iliyochezwa kati ya timu hiyo na timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu(wenye jezi za zambarau) na timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa(wenye jezi nyeupe) wakicheza mechi ya kirafiki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.




Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi  na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza  ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Friday, November 22, 2019

DKT BANA AOMBA WIZARA YA FEDHA KUWEZESHA UJENZI WA MABWENI IFM KAMPASI YA SIMIYU


Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Balozi Dkt. Benson Bana ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kuwezesha ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi  takribani 500 wanaotarajiwa kudahiliwa mwezi Machi, 2020 katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo hicho Mkoani Simiyu, ili kuwaondolea adha ya kupanga mitaani.

Dkt. Bana ametoa ombi hilo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji alipofanya ziara Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo  kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Dkt. Bana amesema kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaoomba udahili wa masomo, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kimeanzisha Kampasi ya Kanda ya Ziwa iliyopo Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Simiyu, ambapo mwezi Machi 2020 wanafunzi takribani 1000 wanatarajiwa kuanza masomo.

“Ili tuweze kufikia malengo yetu tunaomba mabweni ya kuhimili angalau wanafunzi 500 tu, Mhe. Naibu Waziri tunaomba kuwezeshwa kujenga mabweni haya mengine utuachie tutafanya, tusipofanikiwa hili Mhe. Naibu Waziri, juhudi za Mhe. Mkuu wa Mkoa na viongozi wenzake zinaweza kuishai mahali ambapo si pazuri,” alisema Dkt. Bana.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inatambua juhudi za Mkoa wa Simiyu katika elimu na kuahidi kujenga mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kama alivyoomba Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, ili wanafunzi watakaodahiliwa wapate malazi hususani wanafunzi wa kike.

“Hizi changamoto mlizozitaja na hasa hili la mabweni kwa ajili ya watoto wetu linafanyiwa kazi kwa haraka na ujenzi wa mabweni ya watoto 500 mpaka tutakapofika mwezi Machi inawezekana,” alisema Dkt.  Kijaji.

Naye Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameushukuru uongozi wa Chuo cha IFM kwa uamuzi wa kujenga Kampasi mpya Simiyu na kuamua kuifungua mwaka 2020 ambapo amesema kuwepo kwa chuo hicho kutachangia kuongeza mwamko wa elimu katika mkoa wa Simiyu, huku akiwaalika wawekezaji kuwekeza katika huduma mbalimbali katika kampasi hiyo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof.Tadeo Satta amewashukuru viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa namna walivyowezesha kupata eneo la ujenzi lenye ukubwa wa ekari 30 ambalo lilitolewa bure na pia walivyosaidia katika hatua ya ujenzi ambapo wametoa wataalam kusaidia kusimamia ujenzi na kupelekea ujenzi kwenda kwa kasi.

Ameongeza kuwa majengo yanayotarajiwa kujengwa katika kampasi ya Simiyu ni jengo la utawala, maktaba, madarasa, maabara ya kompyuta, hosteli za wanafunzi, nyumba za wafanya kazi, kafteria na holi kwa ajili ya mikutano; ambapo kwa awamu ya kwanza ujenzi ulianza mwezi Julai 2019 mpaka sasa jengo la utawala lenye ghorofa moja limefikia asilimia 62 na madarasa yamefikia asilimia 92.
MWISHO



Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba (mbele) akiwaongoza  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea majengo  ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha Usimamizi  wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya  kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), juu ya ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo hicho, wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi katikati), juu ya ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo hicho, wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo Kijiji cha  Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu aliyofanya kwa lengola kuona maendeleo ya ujenzi.


Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mhe. Balozi Dkt. Benson Bana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Satta, mara baada ya mazungumzo kati yake na wajumbe wa Baraza la Uongozi wa  Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa katika Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi.
Sehemu ya jengo la Utawala katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) katika Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambayo ujenzi wake umefikia asilimi 62 na ikitarajiwa kukamilika.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza na Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  na viongozi wa mkoa wa Simiyu(baadhi hawapo pichani), kabla ya  kutembelea majengo  ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha Usimamizi  wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara yake katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya  kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi huo.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mara baada ya mazungumzo kati yake na wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kufunguliwa Machi 2020.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), juu ya ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo hicho, wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu  kushoto) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.

Diwani wa Kata ya Sapiwi akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba (mbele kushoto) akiwaongoza  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea majengo  ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha Usimamizi  wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya  kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji(kushoto)  akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020


Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba (mbele) akiwaongoza  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea majengo  ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha Usimamizi  wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya  kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.


Jengo la Maktaba katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambalo liko katika hatua ya ukamilishaji  ikitarajiwa kukamilika kabla ya Machi 2020.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa ameongozana na  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea majengo  ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya  Chuo cha Usimamizi  wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya  kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.


Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Chuo(IFM), Prof. Tadeo Satta  na viongozi wengine wakiwasikiliza baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi ambao walikuwa wakiwasilisha hoja zao kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi katikati) ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho  katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mhe. Balozi Dkt. Benson Bana wakati wajumbe wa bodi hiyo, walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza wakati wa ziara yake  katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho,  Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho,  Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho, Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi  Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiagana na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), mara baada ya mazungumzo kati yake na wajumbe hao walipomtembelea ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.


Wednesday, November 20, 2019

SERIKALI KUCHIMBA VISIMA KUMI KUKABILIANA NA ADHA YA MAJI MEATU


Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali itachimba visima kumi vya maji mara moja katika eneo la Mto Semu Kijiji cha Magwila wilayani Meatu na kujenga mtandao wa bomba kutoka katika visima hivyo mpaka  mjini Mwanhuzi wilayani humo Mkoani Simiyu, ili kukabiliana na adha ya maji kwa wananchi baada ya kukauka kwa bwawa la Mwanyahina.

Prof. Mbarawa amesema hayo jana Novemba 19, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Mwanhuzi mara baada ya kutembelea na kuona Bwawa la Mwanyahina lililokauka ambalo ndiyo chanzo kikuu cha maji katika Mji huo na eneo la Mto Semu kilipo kisima kinachotumiwa sasa, ambapo watu wanachota maji kwa magari na kuwauzia wananchi mjini Mwanhuzi.

“ Mhe.Rais amenielekeza kwamba tutachimba visima kumi haraka kutoka kule ambako maji yanachotwa sasa, tutajenga mtandao wa bomba kutoka kwenye visima mpaka  hapa mjini, ili maji yale yatolewe visimani na kuletwa kwenye mfumo wa maji wa hapa mjini,” alisema  Mbarawa.

Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa amesema Wizara ya maji imetoa magari matatu kwa ajili ya kusaidia kubeba maji kutoka kisima na kusambaza kwa wananchi, huku akiagiza ukarabati wa Bwawa la Mwanyahina kufanyika kwa kutoa tope.

Awali akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema Bwawa la Mwanyahina limekauka kutokana na kujaa tope na ukame uliotokea wilayani humo katika msimu wa mvua wa mwaka 2018/2019.

Aidha, Dkt. Chilongani ameomba Wizara ya maji iweze kutoa kipaumbele kwa miradi yote ya maji iliyosanifiwa iweze kutekelezwa katika Wilaya ya Meatu, ili kuongeza hali ya upatikanaji wa maji vijijini na mjini.

Kwa upande wao wananchi wa Mji wa Mwanhuzi wameishukuru Serikali kwa kukubali kuwachimbia visima ambavyo vitawasaidia kuondokana na adha maji baada ya Bwawa la Mwanyahina kukauka na kusababisha wao kununua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi 100 hadi 200.

“Sasa hivi tunauziwa ndoo ya lita ishirini kwa shilingi 200, tunaishukuru Serikali kuona kilio chetu, pia tunamshukuru Waziri wetu wa Maji kwa mpango aliokuja nao wa kutuchimbia visima na kutuletea maji  hapa mjini, tunaomba mpango huu ufanyike haraka, ili tuondakane na shida ya maji tuliyonayo sasa,” alisema Mariam Kashinje mkazi wa Mwanhuzi.

“Binafsi namshukuru Mbunge wetu kwa kutoa gari lake ambalo linatoa huduma ya maji bure, pia tunamshukuru Mhe. Diwani wetu Zakaria kuruhusu watu kuchota maji kwenye kisima chake na kubeba  kwenye maboza na sisi wananchi  tunanunua; lakini nimefurahishwa sana na mpango wa Waziri wa  Maji aliyesema Mhe. Rais anataka tuchimbiwe visima naamini tatizo hili litaisha,” alisema Mboi Ngidinga.
MWISHO



 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(mwenye miwani katikati) akipata maelezo kuhusu kisima kilichopo eneo la Mto Semu kijiji cha Magwila wilayani Meatu, ambacho kinatumiwa kutoa huduma kwa sasa kwa wananchi wa Mji wa Mwanhuzi baada kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina ambalo ndiyo chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi.



Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(wa tatu kulia) kuelekea katika kisima kilichopo eneo la Mto Semu kijiji cha Magwila wilayani Meatu Novemba 19, 2019, ambacho kinatumiwa kutoa huduma kwa sasa kwa wananchi wa Mji wa Mwanhuzi baada kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina ambalo ndiyo chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi.



Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum Khamis (mwenye kofia) akimuonesha jambo Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(mwenye miwani kulia)alipotembelea kuona eneo la chujio la Maji katika Mji wa Mwanhuzi wilayani Meatu Novemba 19, 2019.



Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(wa pili kulia) kuhusu Bwawa la Mwanyahina chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi ambalo limekauka kwa sasa, wakati wa ziara yake Novemba 19, 2019.



Sehemu ya Bwawa la Mwanyahina chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi ambalo limekauka kwa sasa ambalo Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameagiza lifanyiwe ukarabati kuondolewa tope.



Baadhi ya wananchi wa Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu wakipata huduma ya maji kutoka kwenye magari yanayosomba maji kutoka katika Kisima baada ya changamoto ya maji katika mji huo iliyosababishwa kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina.



Baadhi ya wananchi wa Mji wa Mwanhuzi wakiwa katika foleni ya kupata huduma ya maji kutoka kwenye magari yanayosomba maji kutoka katika Kisima baada ya changamoto ya maji katika mji huo iliyosababishwa kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina.



Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(wa tatu kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya  Meatu, Mhe. Joseph Chilongani moja ya gari litakalotumika kwa dharura kusomba maji kutoka kisima kilichopo eneo la mto Semu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kuchimbwa kwa visima kumi , wakati wa ziara yake Novemba 19, 2019.

Baadhi ya wananchi wa Mji wa Mwanhuzi wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(hayupo pichani) wakati akizungumza nao, Novemba 19, 2019  mara baada ya kutembelea na kuona Bwawa la Mwanyahina lililokauka na eneo la Mto Semu kilipo kisima kinachotumiwa sasa ambapo maji yanachotwa na kubebwa kwa magari na kupelekwa mjini ambapo wananchi wananunua.

Baadhi ya vijana wakipakia maji katika matanki kwa ajili ya kuwapelekea wananchi huduma ya maji katika Mji wa Mwanhuzi baada ya changamoto ya maji katika mji huo iliyosababishwa kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina.



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (wa pili kulia) akimshukuru  Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kwa kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya  Meatu, Mhe. Joseph Chilongani(wa nne kushoto)  moja ya gari litakalotumika kwa dharura kusomba maji kutoka kisima kilichopo eneo la mto Semu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kuchimbwa kwa visima kumi , wakati wa ziara yake Novemba 19, 2019.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(mwenye miwani katikati) akiangalia maji yanayotoka katika kisima kilichopo eneo la mto Semu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kuchimbwa kwa visima kumi , wakati wa ziara yake Novemba 19, 2019.


Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwa na baadhi ya viongozi katika eneo la Chujio la Maji Mjini Mwanhuzi wakati wa zaira yake wilayani Meatu Novemba 19, 2019.




Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!