Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM) Balozi Dkt. Benson Bana ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango
kuwezesha ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi takribani 500 wanaotarajiwa kudahiliwa mwezi
Machi, 2020 katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya
Chuo hicho Mkoani Simiyu, ili kuwaondolea adha ya kupanga mitaani.
Dkt.
Bana ametoa ombi hilo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu
Kijaji alipofanya ziara Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo
kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi
Mkoani Simiyu.
Dkt.
Bana amesema kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaoomba udahili wa masomo,
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kimeanzisha Kampasi ya Kanda ya Ziwa iliyopo
Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Simiyu, ambapo mwezi Machi 2020 wanafunzi
takribani 1000 wanatarajiwa kuanza masomo.
“Ili
tuweze kufikia malengo yetu tunaomba mabweni ya kuhimili angalau wanafunzi 500
tu, Mhe. Naibu Waziri tunaomba kuwezeshwa kujenga mabweni haya mengine utuachie
tutafanya, tusipofanikiwa hili Mhe. Naibu Waziri, juhudi za Mhe. Mkuu wa Mkoa
na viongozi wenzake zinaweza kuishai mahali ambapo si pazuri,” alisema Dkt.
Bana.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inatambua
juhudi za Mkoa wa Simiyu katika elimu na kuahidi kujenga mabweni yenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 500 kama alivyoomba Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo,
ili wanafunzi watakaodahiliwa wapate malazi hususani wanafunzi wa kike.
“Hizi
changamoto mlizozitaja na hasa hili la mabweni kwa ajili ya watoto wetu
linafanyiwa kazi kwa haraka na ujenzi wa mabweni ya watoto 500 mpaka
tutakapofika mwezi Machi inawezekana,” alisema Dkt. Kijaji.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameushukuru uongozi wa Chuo cha IFM
kwa uamuzi wa kujenga Kampasi mpya Simiyu na kuamua kuifungua mwaka 2020 ambapo
amesema kuwepo kwa chuo hicho kutachangia kuongeza mwamko wa elimu katika mkoa
wa Simiyu, huku akiwaalika wawekezaji kuwekeza katika huduma mbalimbali katika
kampasi hiyo.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof.Tadeo Satta amewashukuru
viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa namna walivyowezesha kupata eneo la ujenzi lenye
ukubwa wa ekari 30 ambalo lilitolewa bure na pia walivyosaidia katika hatua ya
ujenzi ambapo wametoa wataalam kusaidia kusimamia ujenzi na kupelekea ujenzi
kwenda kwa kasi.
Ameongeza kuwa majengo yanayotarajiwa kujengwa katika
kampasi ya Simiyu ni jengo la utawala, maktaba, madarasa, maabara ya kompyuta,
hosteli za wanafunzi, nyumba za wafanya kazi, kafteria na holi kwa ajili ya
mikutano; ambapo kwa awamu ya kwanza ujenzi ulianza mwezi Julai 2019 mpaka sasa
jengo la utawala lenye ghorofa moja limefikia asilimia 62 na madarasa yamefikia
asilimia 92.
MWISHO
Katibu Tawala Msaidizi
sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba
(mbele) akiwaongoza Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na Wajumbe
wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea
majengo ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa
ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya
Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kijiji cha
Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), juu ya
ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa
ya Chuo hicho, wakati wa ziara ya Naibu
Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo Kijiji cha Sapiwi wilayani
Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi
katikati), juu ya ujenzi wa majengo mbalimbali unaoendelea katika Kampasi ya
Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho, wakati wa
ziara ya Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu aliyofanya
kwa lengola kuona maendeleo ya ujenzi.
Kutoka kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza
la uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mhe. Balozi Dkt. Benson Bana
na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Satta, mara baada ya mazungumzo kati
yake na wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)
walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya
kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa katika Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi.
Sehemu ya jengo la
Utawala katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya
Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) katika Kijiji cha Sapiwi wilayani
Bariadi Mkoani Simiyu, ambayo ujenzi wake umefikia asilimi 62 na ikitarajiwa
kukamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza
la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mara baada ya mazungumzo kati
yake na wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)
walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya ziara ya Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo pichani) mkoani Simiyu ya
kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta akizungumza na baadhi ya wananchi
wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo
hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani
Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo
inatarajiwa kuanza kufunguliwa Machi 2020.
Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), juu ya ujenzi wa
majengo mbalimbali unaoendelea katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho, wakati wa ziara ya Naibu Waziri
Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi
Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya
Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu
Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba
21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa
kufunguliwa Machi 2020.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya
Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu
Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba
21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa
kufunguliwa Machi 2020.
Diwani wa Kata ya
Sapiwi akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika
kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye
alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba
21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa
kufunguliwa Machi 2020.
Katibu Tawala Msaidizi
sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba
(mbele kushoto) akiwaongoza Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na
Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea
majengo ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa
ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya
Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi
ya wananchi wa Kata ya Sapiwi waliofika kumsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji ambaye alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya
Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi
wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo
ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.
Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji(kushoto)
akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Kampasi
ya Kanda ya Ziwa ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika Kata ya Sapiwi
wilayani Bariadi. Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo
ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020
Katibu Tawala Msaidizi
sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba
(mbele) akiwaongoza Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi), Viongozi na Wajumbe
wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
na viongozi wa mkoa wa Simiyu, kutembelea majengo ya Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya
Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Jengo la Maktaba katika
Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo cha
usimamizi wa Fedha (IFM) katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu,
ambalo liko katika hatua ya ukamilishaji
ikitarajiwa kukamilika kabla ya Machi 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akiwa ameongozana na
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye
ushungi), Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa
Fedha (IFM) na viongozi wa mkoa wa
Simiyu, kutembelea majengo ya Kampasi ya
Kanda ya Ziwa ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM(Simiyu), wakati wa ziara ya
Naibu Waziri Kijaji Novemba 21, 2019 katika kampasi hiyo inayojengwa Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, aliyofanya kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Chuo(IFM), Prof. Tadeo Satta na viongozi wengine wakiwasikiliza baadhi ya
wananchi wa Kata ya Sapiwi ambao walikuwa wakiwasilisha hoja zao kwa Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi katikati) ambaye
alitembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi. Novemba
21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa
kufunguliwa Machi 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mhe. Balozi Dkt. Benson Bana wakati
wajumbe wa bodi hiyo, walipomtembela ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya
ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo
pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa katika Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi.
Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya
Sapiwi waliofika kumsikiliza wakati wa ziara yake katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo
hicho, Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Novemba
21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa
kufunguliwa Machi 2020.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt.Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake katika Kampasi
ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho, Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi Novemba 21, 2019 kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi
hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi
kwa ajili ya ziara yake katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho, Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi Novemba 21, 2019
kuona maendeleo ya ujenzi wa kampasi hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa Machi
2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiagana na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wajumbe wa Baraza
la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), mara baada ya mazungumzo kati
yake na wajumbe hao walipomtembelea ofisini kwake Novemba 21, 2019 siku ya
ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (hayupo
pichani) mkoani Simiyu ya kutembelea Kampasi ya Kanda ya Ziwa ya Chuo hicho
katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.
0 comments:
Post a Comment