Wilaya ya Maswa imezindua mfuko
wa walimu kwa lengo la kuwasaidia walimu ambao hawana sifa za kukopesheka
katika taasisi zingine za fedha ili waweze kupata mikopo kwa riba nafuu.
Mfuko
huo umezinduliwa na Katibu wa Chama cha Walimu nchini, Mwl. Deus Seif wakati wa
hafla ya kuwapongeza walimu zaidi ya 1400 wa shule za msingi 123 za wilaya hiyo
kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na
kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9
mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019.
Akizungumza
na mamia ya walimu walioshiriki katika uzinduzi huo, Seif amewaasa walimu
kutambua thamani waliyopewa na viongozi wa wilaya na mkoa kwa kuendelea kuwajibika
kwa uadilifu mkubwa.
“
Nitoe wito kwa walimu wenzangu ambao si waadilifu wabadilike, wale watoro
waache utoro, ambao ni walevi wache ulevi wafundishe watoto; lakini wazazi na
ninyi mtusaidie kuhimiza watoto wawe na mahudhurio mazuri shuleni ili walimu
waweze kufanya kazi yao vizuri,” alisema Seif.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko amesema hadi
sasa mfuko huo umeingiziwa kiasi cha shilingi
milioni 15 na halmashauri na baadaye wadau kuongeza kiasi cha shilingi milioni
15 na kuufanya mfuko huo kuwa na jumla ya shilingi milioni 30.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka amewataka walimu kuacha tabia ya kukopa
fedha katika taasisi nyingine za fedha hususani za binafsi zenye riba kubwa ambazo
huwalazimu kuweka kadi zao za benki kama rehani, huku akishauri Benki ya walimu
kuja na huduma zinazojibu changamoto za walimu ikiwemo kutoa mikopo kwa riba
nafuu
Kwa
upande wake Katibu wa CWT ameipongeza Wilaya ya Maswa kwa kuona haja kuwapongeza
walimu na ya kuwasaidia walimu kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kupitia mfuko
huo, ambapo CWT pia imeunga mkono juhudi Wilaya kwa kuchangia kiasi cha
shilingi milioni Nane (8).
Wilaya
hiyo pia imetoa zawadi ya majiko ya gesi 101 kama zawadi kwa shule hizo ili
kuwawezesha walimu kupata chai asubuhi wakiwa shuleni na kuwapunguza walimu muda
wa kwenda kutafuta huduma hiyo nje ya maeneo ya shule.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe amesema mwaka 2018 Wilaya ilitoa
majiko ya gesi kwa shule 20 zilizofanya
vizuri hivyo, majiko hayo yanatolewa kwa shule 101 ambazo hazikupata awali,
pamoja na zawadi ya majiko shule zilizofanya vizuri zimepewa fedha taslimu
shilingi 500,000.
Katika uzinduzi huo pia
ilifanyika harambee kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa nyumba nne za walimu ikiwa
ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa nyumba za
walimu
MWISHO
Katibu
wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif (kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu
wakiwa wameshika mfano wa hundi ya shilingi milioni 15 ambayo imetolewa na
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa walimu
uliozinduliwa rasmi Novemba 29, 2019 Mjini Maswa.
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredricka Sagamiko(kushoto) wakipokea hudni ya shilingi milioni nane kutoka kwa Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif(kulia) zilizotolewa an chama hicho kuchangia Mfuko wa walimu uliozinduliwa rasmi Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi ya walimu kutoka shule mbaimbali wilayani Maswa wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Mmoja wa Wakurugenzi katika Benki ya Walimu akitoa maelezo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu juu ya namna benki hiyo itakavyounga mkono mfuko wa walimu wilayani maswa uliozinduliwa rasmi Novemba 29, 2019 Mjini Maswa.
Mmoja wa Walimu akipokea zawadi ya jiko la gesi iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kila shule kwa ajili ya kutumia kupikia chai asubuhi wakiwa shuleni, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa CWT
Taifa, Mwl.Deus Seif katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi
123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa
la saba na kuongeza ufaulu kutoka
asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019.
Baadhi
ya Maafisa Elimu Kata wakifutailia matukio katika hafla ya
kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya
kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia
asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi
ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika hafla ya
kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya
kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia
asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi ya viongozi na wadau wa elimu wakicheza wimbo maalum uliondaliwa na kwaya ya walimu Maswa wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali mkoa wa Simiyu na viongozi wa CWT na wakifutailia matukio katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali mkoa wa Simiyu na viongozi wa CWT na wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimishwa kwa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Majiko 101 yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Maswa kwa ajili ya shule za msingi kwa ajili ya kupikia chai asubuhi, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif akizungumza na walimu wa shule a msingi wilayani maswa(hawapo pichani), katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Katibu
wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif akimshukuru Mbunge wa Maswa mashariki na Naibu
Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo kwa kukubaki kuchangia ujenzi wa nyumba
za walimu wilayani Maswa, katika hafla ya
kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya
kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia
asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Mmoja wa Walimu akipokea zawadi ya jiko la gesi iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kila shule kwa ajili ya kutumia kupikia chai asubuhi wakiwa shuleni, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi
ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika hafla ya kuwapongeza
walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya
vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia
asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka wakiteta jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Mmoja wa Walimu akipokea zawadi ya jiko la gesi iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kila shule kwa ajili ya kutumia kupikia chai asubuhi wakiwa shuleni, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Baadhi
ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika hafla ya kuwapongeza
walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya
vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia
asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka wakiteta jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
0 comments:
Post a Comment