Shirika la Bima la Taifa (NIC)linatarajia kuanza kutoa huduma za
bima ya mazao kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Meatu na Maswa Mkoani
Simiyu, ambapo wakulima watakuwa na uwezo wa kukata bima katika zao la pamba
itakayomkinga dhidi ya majanga ukame,mvua zilizozidi kiasi , mafuriko, moto
pori ,magonjwa na wadudu wasiothibitika.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Bima ya mazao
kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter wakati akitoa mafunzo
kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na
ushirika mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na NIC yaliyofanyika Novemba 07, 2019 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya Mazao inayotarajiwa kutolewa
kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
“Huduma ya bima ya mazao itaanza kwanza na kumkinga mkulima dhidi ya
majanga kama vile ukame , mvua zilizozidi kiasi , mafuriko, moto pori,magonjwa
na wadudu wasiothibitika na itakatwa kwa pamoja kwa hiyo tutakuwa tunakinga
mtaji wa mkulima aliouwekeza katika kilimo,” alisema Peter.
Aidha, Peter amesema pamoja na bima kukinga mtaji wa mkulima
katika uzalishaji, NIC kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo itaendelea
kuboresha na kuongeza wigo wa huduma za bima ya mazao kwa kuangalia mahitaji ya
wakulima wa pamba kwa wakati husika ikiwemo suala la bei.
Awali akifungua mafunzo Katibu Tawala mkoa wa
Simiyu,Bw, Jumanne Sagini amesema wakulima wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo upatikanaji wa pembejeo, mvua iliyozidi hivyo Bima itawahakikishia
kupata fidia pale wanapopata hasara inayosababishwa na changamoto hizo na
kusisitiza viongozi na wataalam kutoa ushirikiano kwa NIC wanapotekeleza.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi
amesema kuwa ujio wa bima ya mazao ni wa msingi hivyo ni vema NIC ikatoa bima
kwa mahitaji/changamoto ambayo ni ya kipaumbele katika eneo fulani kwa kuwa
changamoto za wakulima zinatofautiana, huku akitolea mfano kwa mkoa wa Simiyu kuwa
ukame hauna athari sana kwenye zao la pamba.
Afisa kilimo wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bibi. Suzana Sabuni
amesema kuwa ni vyema bima hiyo ijikite kwenye vipaumbele vya wakulima
kutokana na mazao wanayolima ikiwa ni sambamba na kuwapata uhuru wakulima
kuchagua bima wanayoitaka.
Naye afisa ushirika kutoka wilaya ya Itilima Heri Muhina ameshauri
kuwa katika upande wa majanga ni vyema bima ilenge kuwasaidia katika majanga ya
moto ambayo yamekuwa yakitokea kwenye baadhi ya maghala ya vyama vya ushirika
(AMCOS) pindi wakulima wanapokuwa wamehifadhi pamba yao.
Akifunga kikao hicho mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga amesema kuwa ni vyema utekelezaji huo uanze mapema kuelekea msimu mpya
wa kilimo wa mwakani 2019/ 2020 na kusisitiza wakulima wapate taarifa sahihi
kwa wakati ili waweze kuifahamu vizuri kabla ya utekelezaji.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Mratibu wa Bima ya mazao kutoka Shirika la
Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter akitoa
mada kwenye mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na wataalam wa
kilimo na ushirika wakimsikiliza Mratibu
wa Bima ya mazao kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter(hayupo pichani) kwenye mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi akichangia hoja
katika mafunzo kwa viongozi, wataalam wa
Kilimo na ushirika mkoa wa Simiyu iliyoandaliwa na Shirika la Bima la
Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba 07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga
uelewa wa pamoja juu ya Bima ya Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mratibu wa Bima ya mazao kutoka Shirika la Bima la
Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter(hayupo
pichani) kwenye mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Baadhi ya wataalam wa kilimo na mifugo mkoani
Simiyu wakimsikiliza Mratibu wa Bima
ya mazao kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter(hayupo pichani) kwenye kwenye mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), kwenye mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa
wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment