Saturday, November 2, 2019

CWT TEGUENI KITENDAWILI CHA WALIMU KUKOPA NJE YA MFUMO RASMI: RC MTAKA


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kuja na majawabu ya kuwasaidia walimu kuacha kukopa katika taasisi za fedha zisizo rasmi ambazo hazijasajiliwa na wafanyabiashara binafsi ambao wamekuwa wakichukua kadi zao za benki (ATM) na kukaa nazo na kuwatoza riba kubwa.

Mtaka ameyasema hayo katika Mkutano wa ujirani mwema wa Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) ulioshirikisha viongozi kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera, Mkutano uliofanyika Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Amesema ni vema walimu wabadilike na kutumia taasisi rasmi za fedha kuchukua mikopo badala ya kukopa kwa wafanyabiashara binafsi au taasisi za fedha zisizo rasmi(ambazo hazijasajiliwa) ili waondokane na mikopo inayowaumiza kwa kuwa na riba kubwa.
“ Kuna wafanyabiashara wanakaa na kadi za ATM za walimu wetu, wakati  mshahara unapotoka wanaenda kuchukua fedha na wanabaki na hizo kadi, ni lazima CWT mje na majawabu ya kuwasaidia walimu wanaokopa nje ya mfumo wa kibenki usio rasmi kwa sababu CWT sasa hivi ina benki; vilevile Benki kuu, benki zote za biashara na HAZINA wana utaratibu wa mikopo kupitia mishahara yetu,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka ameahidi kuwa katika Mkoa wa Simiyu, Viongozi wote watahakikisha wanawapa kipaumbele na hawatakuwa tayari kuona watumishi wa kada nyingine wakiwadhalilisha walimu

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenyeulemavu,  Mhe.Stella Ikupa amewapongeza Chama cha Walimu kwa kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika ngazi za uongozi na kusisitiza walimu kupata mafunzo ya elimu maalum  ili waweze kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum waliopo katika shule zao.

“Niwapongeze CWT kujumuisha walemavu katika uongozi pia iwapongeze walimu wote kwa kazi kubwa mnayofanya,  mna mchango mkubwa kwa ustawi wa mtu mmoja mmoja, kada mbalimbali na jamii kwa ujumla, Serikali imeendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali za walimu, ikiwemo kuwapandisha madaraja ambapo hivi karibuni walimu 124,000 walipandishwa madaraja,” alisema Ikupa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa  Serikali, Dkt. Hassan  Abbas amesema Serikali imehakikisha wananchi  wanapata taarifa kwa wakati, hivyo imetungwa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa mwaka 2016, ili kuruhusu kila mwananchi kufahamu mambo mbalimbali yanayoendelea kuhusu utendaji wa Serikali.

Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa kiuchumi,  ndio maana kuna utekelezaji wa miradi mikubwa kama mradi wa  kufua umeme wa Julius Nyerere, na mradi wa reli ya kisasa, huku akibainisha kuwa pia  Serikali inaendelea kununua ndege, kwa sababu ndege ni uchumi na zinasaidia kukuza sekta ya utalii nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif amesema walimu wataendelea kuchapa kazi huku akiomba Serikali kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kutopandishwa madaraja na mishahara kwa wakati, malipo ya fedha za likizo, uhamisho na malimbikizo ya mishahara.

Akichangia hoja katika mkutano huo Kiongozi wa CWT kutoka wilayani Misungwi Mwanza, Mwl Rosemary Mboneko ameiomba Serikali iwasaidie walimu wanaoomba uhamisho kuwafuata wenza wao waruhusiwe ili kuepuka ndoa za masafa na kuwafanya watumishi hao wakafanya kazi kwa amani.
MWISHO



Baadhi ya viongozi wakishangilia jambo wakati wa Mkutano wa ujirani mwema wa Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera, Mkutano uliofanyika Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.



Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyia  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali na Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) wakiwa katika Mkutano wa ujirani mwema wa Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera, Mkutano uliofanyika Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Vongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyia  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera wakiimba wimbo wa mshikamano  katika Mkutano wa Ujirani mwema wa Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera, uliofanyika Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko  katika Mkutano wa Ujirani mwema Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa walimu akiwasilisha hoja yake katika Mkutano wa Ujirani mwema Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Vongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera wakiwa  katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif (kushoto)  na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko  wakifuatailia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Ujirani mwema Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyika  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Walimu(CWT) kutoka mikoa ya Simiyu, Kigoma,Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa katika Mkutano wa Ujirani mwema uliofanyia  Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!