Na Stella Kalinga,
Simiyu RS
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa,
amefunga rasmi kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani
Simiyu, ambapo amewapongeza viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe. Anthony Mtaka kwa ubunifu huo ambao utawasaidia wanafunzi hao kufanya
vizuri katika mitihani yao.
Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo Oktoba
30, 2019 wakati wa kuhitimisha kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha
nne ambayo imefanyika kwa muda wa siku 60 katika Shule ya sekondari Simiyu na
Chuo cha Ualimu Bariadi Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwaandaa na mtihani wa
Taifa unaotarajia kufanyika kuanzia Novemba 04, 2014.
“Nampongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu mkubwa wa kuandaa kambi
hizi kwani, naamini wanafunzi mmejifunza mambo mengi na mtafanya
vizuri katika mtihani wenu, ningeshauri watu wengine waige jambo hili, niwakumbushe
wanafunzi mtakaoanza mtihani wenu Novemba 4, 2019, kumuomba Mungu ili
awaongoze kipindi chote cha mitihani,” alisema Ikupa.
Aidha, Ikupa amesema Serikali
imeendelea kuboresha sekta ya elimu nchi kwa kuongeza bajeti katika shule,
kujenga madarasa, na anaamini kuwa itaendelea kutatua changamoto ya
walimu katika mkoa wa Simiyu, na nchini kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema uongozi wa Mkoa,
walimu, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo wamefanya uwekezaji mkubwa
kwa wanafunzi wote waliokuwa katika kambi za kitaaluma na kupitia kazi nzuri
iliyofanywa na walimu anaamini kwamba watafanya vizuri katika mtihani wa Taifa
utakaoanza Novemba 4, 2019.
Ameongeza Serikali mkoani Simiyu itaendelea kuwapa motisha
walimu, wanafunzi na shule zote zitakazofanya vizuri katika mitihani ya
Kitaifa, huku akiahidi kuwalinda walimu wote, ambapo ameahidi kuwa kuanzia Desemba Mosi, 2019 viongozi wa
mkoa watawatembelea walimu katika Halmashauri zote na kuzungumza nao.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbas amewaomba wadau kuendelea kuunga mkono kambi hizi
ili waweze kutimiza ndoto zao huku akibainisha kuwa kupitia kambi hizo watapatikana
viongozi mahiri wa baadaye.
Katibu Mkuu, Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif amesema walimu
wana imani na Serikali na wameamua kufanya kazi yao kwa bidii na wanaiomba
Serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo
kupandishwa madaraja na mishahara kwa wakati na malipo ya fedha za likizo na
malimbikizo ya mishahara.
Naye Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju amesema tangu kambi
hizi zianze mwaka 2016 zimesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika
matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo kwa kidato
cha nne mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 70.68%
na mwaka 2019, ufaulu umekuwa 86.46%.
Naye Diana Boniphace mwanafunzi kutoka Shule ya sekondari Kidinda
amesema, “kupitia kambi hii wanafunzi tumejifunza mambo mengi kupitia kwa
walimu mahiri na kiwango cha ufaulu kimeongezeka tofauti na tulivyoingia hivyo
tunaahidi kuwa tutafanya vizuri katika mtihani wa Taifa tutakaoanza Novemba 04,
2019.”
Kambi ya Kitaaluma iliyohitimishwa Oktoba 30, 2019 ilihusisha
wanafunzi 1512 ambao walikuwa na ufaulu hafifu(daraja sifuri), wanafunzi
waliofanya vizuri katika mtihani wa Mkoa(Mock) na wanafunzi kutoka shule zenye wanafunzi chini ya 30 na wamekaa
kambini siku 60.
MWISHO
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu
wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, mara baada
ya kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi hao kuhitimishwa Oktoba 30, 2019
Mjini Bariadi.
\
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, akizungumza
na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019
Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha nne kutoka shule
mbalimbali mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, wakati
wa kufunga kambi yao ya kitaaluma ya
siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kulia Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye
ulemavu, Mhe. Stella Ikupa,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu
Tawala Mkoa, Bw. Jumanne Sagini, Afisa Elimu Mkoa, Ernest Hinju na Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakifurahia jambo, wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi
wa kidato cha nne Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu
wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60
kwa wananfunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba
30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi Kidato cha nne kutoka shule
mbalimbali mkoani Simiyu wakicheza na kufurahi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.
Anthony Mtaka mara baada ya kufunga kambi
ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kitu wakati wa
kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba
30, 2019 Mjini Bariadi , kutoka kulia walioketi mbele, Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt Hassan Abbas, Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif na Mbunge la
Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko.
Baadhi ya walimu mahiri waliofundisha kambi ya kitaaluma ya kidato cha
nne wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku
60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa,
Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo
akitoa salamu za Chama, wakati wa hafla
ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa
na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu
wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Sheikh wa Mkoa wa
Simiyu, Mahamoud Kalokola akitoa dua wakati wa hafla ya kufunga kambi ya
kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe.
Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne walio kuwa
katika kambi ya kitaaluma mkoani Simiyu, ambayo imehitimishwa Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi akitoa ushuhuda wa namna kambi zilivyomsaidia
kuongeza ufaulu wake mbele ya wanafunzi wenzake, walimu na viongozi mbalimbali.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan
Abbas(kulia) na Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif wakiteta jambo wakati wa
hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo
imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu
wakimvika skafu Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, ambaye alikuwa Mgeni rasmi
katika ufungaji wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Oktoba
30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi
wakicheza pamoja na waimbaji wa kwaya ya walimu Bariadi, wakati wa hafla ya
kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao ambayo imehitimishwa na
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu
wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu
wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, mara baada
ya kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi hao kuhitimishwa Oktoba 30, 2019
Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili
kushoto) akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani
Simiyu, wakati wa kufunga kambi ya
kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mbunge la Afrika Mashariki, Mhe. Happyness Lugiko ,
akipokea cheti cha shukrani ya kuchangi kambi ya kitaaluma mkoani Simiyu,
wakati wa hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wao
ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, Oktoba 30,
2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto)
akiteta jambo na na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, wakati wa
kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba
30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu, wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka Kushoto Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne
Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakimsikiliza Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu,
Mhe. Stella Ikupa mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kabla ya
hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne
ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri huyo, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu wa CWT Taifa, Mwl. Deus Seif akizungumza na
viongozi wa Mkoa na Simiyu na viongozi wengine, mara baada ya kufika katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kabla ya hafla ya kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60
kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambayo imehitimishwa na Naibu Waziri huyo, Oktoba 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi walioshiriki katika halfa ya
kufunga kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne mkoani
Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba
30, 2019.
0 comments:
Post a Comment