Monday, October 14, 2019

JPM ANAMUENZI MWALIMU NYERERE KWA VITENDO: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema serikali ya awamu ya tano chini ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe inamuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo hususani katika kuendeleza kazi nzuri alizozifanya.

Mtaka ameyasema hayo Oktoba 14, 2019 katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi, likiwashirikisha viongozi wa Serikali, wananchi na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu, UVCCM Simiyu, UVCCM kutoka mikoa mbalimbali nchini na ngazi ya Taifa(makao makuu).

“Mwalimu amepewa heshima ya kuenziwa ninyi  kizazi hiki mnashuhudia kwa macho, wapo watu wanasimuliwa tu kuwa ile barabara inaitwa ‘Nyerere road’, lakini hamkuwepo; leo mnajua kwamba hifadhi fulani inaitwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, mnasikia Mradi mkubwa wa kufua umeme wa maji wa  J.K. Nyerere,  Mhe.Rais amemheshimisha Mwalimu kwa vitendo,” alisema Mtaka

“Mwalimu aliamini katika Watanzania kufanya shughuli za kiuchumi  ikiwemo kilimo,  ufugaji na uvuvi  na akataka waongeze thamani katika shughuli hizo; ndiyo maana Mhe Rais ameanza kufufua viwanda vya nguo, viwanda vya korosho, viwanda vya kahawa na mengine aliyoyaacha Mwalimu, “ aliongeza Mtaka.

Aidha, Mtaka amemzungumzia Mwalimu Nyerere kuwa alikuwa kiongozi wa karne mwenye utu, maono na msimamo ambaye alijua wapi anapotoka na anapotakiwa kwenda kama kiongozi na aliyewaheshimisha Watanzania.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa Vijana wa UVCCM  kuwaeleza ukweli na kuwashauri viongozi vijana ndani ya Serikali kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya uongozi na kuepukana na tabia ya kuweka urasimu wa kufikika na watu , ili viongozi hao watekeleze vema wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na kumsaidia Mhe. Rais Magufuli katika majukumu aliyowapa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo amewataka vijana kumuenzi Hayati  Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere kwa kufanya kazi kwa bidii, ili wajiletee maendeleo kwa kuwa Mwalimu aliamini kuwa kazi ni kipimo cha uhai.

Naye Kaimu Katibu Idara ya Mahusiano ya Kimataifa na Vyuo Vikuu, Bi Asha Feruz amesema kwa kuwa vijana wengi wamezaliwa wakati Hayati Baba wa Taifa,Mwl. Julius K. Nyerere akiwa amefariki ni vema vijana hao wakasoma  vitabu, ili wajue historia ya mwalimu na waasisi wengine wa Taifa la Tanzania.

Mmoja wa Wajukuu wa Mwalimu Nyerere Chifu Edward Magige amesema pamoja na Watanzania kuendelea kukumbuka na kuenzi mambo mazuri yaliyofanywa na Hayati Mwalimu Nyerere ni vema pia wakaukumbuka mchango wa Mama Maria Nyerere katika kazi zilizofanywa na mwalimu.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga ametoa wito kwa Vijana hapa nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, ili waweze kuitumia vema haki yao kuchagua viongozi bora ikiwa ni namna mojawapo ya kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuchagua viongozi watakaosimamia misingi ya uongozi aliyoiweka.
MWISHO
Mkuu  wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wananchi na viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya Mkoa, Mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya mkoa, Mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , wakishangilia jambo katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. George Mayunga akizungumza na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya mkoa, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , wakishangilia jambo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kushoto) na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu, UVCCM Simiyu, UVCCM mikoa mbalimbali na ngazi ya  Taifa wakishangilia jambo, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Haula Kachwamba, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, wakiteta jambo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mjumbe wa NEC Taifa kupitia mkoa wa Simiyu, Ndg. Gungu Silanga akizungumza na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)  mkoa, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa, wakishangilia jambo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa, wakishangilia jambo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baaadhi ya vijana wa UVCCM wakiwa katika maandamano ya amani kuelekea katika ukumbi ambapo limefanyika kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi..

Mmoja wa wajukuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Chifu Edward Magige  akichangia hoja katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Lumen Mathias akizungumza na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , wakishangilia jambo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Haula Kachwamba, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, wakiangalia kitu katika kitabu wakati wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya mkoa na Taifa , wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali  na Taifa , wakishangilia jambo katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Wajukuu wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakiwasalimia baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa, katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa , wakishangilia jambo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya mkoa na Taifa , wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi


 Baadhi ya wananchi na baadhi ya viongozi  CCM Mkoa wa Simiyu, viongozi na wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu, mikoa mbalimbali na ngazi ya Taifa, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wananchi wakicheza wimbo maalum ulioimbwa na Msanii Elizabeth Maliganya(wa pili kushoto mbele) akitoa burudani Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wananchi wakicheza wimbo maalum ulioimbwa na Msanii Elizabeth Maliganya(wa pili kushoto mbele) akitoa burudani Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Haula Kachwamba, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, wakifurahia  jambo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!