Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga ametoa wito kwa Mifuko na programu za
uwezeshaji wananchi kuangalia jinsi ya kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata
mitaji ya kuanzisha viwanda, ili uchumi wa nchi ukue na kupunguza changamoto
zinazokabili jamii.
Kiswaga ameyasema
wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika uzinduzi
wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu
za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya
kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019
katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
“Sote tunafahamu kwamba
Tanzania inalenga kufikia uchumi wa katika ifikapo mwaka 2025 na viwanda ni
nyenzo itakayowezesha nchi kufika huko; viwanda vina mchango mkubwa sana katika
kukuza uchumi wa nchi kwa kuwa
vinanufaisha jamii kwa kutoa ajira, kulipa kodi, kununua malighafi kutoka kwa
wakulima na mengine mengi,” alisema Kiswaga.
Aidha, Kiswaga alitoa
wito kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali nchini kufika
katika maonesho haya kupata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa mifuko /programu
za uwezeshaji za Serikali, kuonesha bidhaa, kunua bidhaa za wajasiriamali na
kupata uelewa wa masuala ya uwezeshaji wananchi.
Naye Afisa Maendeleo ya
Biashara wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi na Kilimo, (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo amesema
wameandaa mpango mkakati wa miaka mitano ambapo wanatarajia kutoa ajira 700,000
ambao unatarajia kuzifikia familia zaidi ya 200,000.
Kaimu Mkurugenzi wa
Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Bi.Esther Mmbaga kutoka
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), amesema malengo ya
maonesho haya ni pamoja na kukuza uelewa wa wananchi kuhusu uwepo, majukumu na vigezo katika kutoa
huduma za mikopo na programu za uwezeshaji.
Bi. Mmbaga ameongeza kuwa
malengo mengine ni kuhamasisha wananchi ili waweze kunufaika na fursa zilizopo
katika mifuko na programu za uwezeshaji na kuhamasisha wananchi kujenga
utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi yenye tija.
Maonesho
ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji
na vikundi vya kifedha vya kijamii, yenye
Kauli Mbiu “Mitaji ni Chachu ya Kujenga
Uchumi wa Viwanda”ambayo yanaendelea katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi yanatarajiwa kufungwa rasmi Oktoba 20, 2019.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
(aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka), akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa
Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu
wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyemwakilisha
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka), katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Katikati ni Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka), akizungumza na
wananchi katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Watumishi wa BarazalaTaifa la uwezeshaji
wananchi kiuchumi katika Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za
uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya
kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
akimsikiliza mmoja wa wanufaika wa mikopo kutoka SIDO katika ufunguzi wa
Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati
ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya
kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba
16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya
mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(mwenye
suti nyeusi) akiangalia bidhaa za wajasiriamli kutoka mikoa ya Tabora na Dodoma
wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Afisa Biashara wa
Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine
Mungo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga alipotembelea
mabanda ya maonesho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu
za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya
kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mahaza Gamitwe (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa
Watanzania katika Uwekezaji , B. Esther Mmbaga kutoka Baraza la Taifa la
Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), akiwasilisha taarifa wakati wa ufunguzi wa
Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji
kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), wakifuatalia
masuala mbalimbali wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za
uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya
kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(mwenye suti nyeusi) akiangalia kukuwanaofugwa
na wajasiriamali wakati alipotembelea
mabanda ya maonesho wakati ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za
uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya
kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
akimsikiliza Afisa kutoka UTT, alipotembelea mabanda ya maonesho katika
ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya
kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba
16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya
mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimsikiliza Afisa kutoka mfuko wa kuhifadhi wanyamapori
, alipotembelea mabanda ya maonesho katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Kikundi cha Ucheshi Cha
mjini Bariadi kikiwaburudisha wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu.
Kikundi cha Ngoma
BASEKI kutoka mjini Bariadi kikiwaburudisha
wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji
na vikundi vya kifedha vya kijamii,
uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment