Msajili
wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na
Sheria, Bi. Felistas Mushi amesema takribani wananchi 1018 wamepata huduma ya msaada wa kisheria katika
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba
25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Mkoani Simiyu.
Mushi ametoa taarifa hiyo katika
Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha kuwa asilimia
kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi na yameshafikishwa
mahakamani na yako katika hatua
mbalimbali.
Amesema huduma walizopata wananchi
katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi, ushauri wa
kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu sahihi ya kwenda pindi wanapopata migogoro.
“Mbali na huduma kwa wananchi mafunzo
yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao 1300 wakiwemo,
wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe wa kamati ya parole,
wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji, wajumbe wa kamati ya maadili ya
mahakimu, askari polisi na magereza, wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa
vijiji na kata, “ alisema Mushi.
Kwa upande wake Hakimu Mary Nyangusi
akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary
Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo
mingi inatokea mara nyingi wanaume(baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto
kudhulumiwa haki zao.
Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi waliofika
kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema, “nashukuru
nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba mwenye mji anapokuwa
amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana mamlaka juu ya mali
iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake wakati mzee hakuacha hata wosia”.
Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya
Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema
wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho ya wiki ya
msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, ili
wananchi wapate uelewa wa masuala ya kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana.
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa Kisheria kwa
Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya kimeenda sambamba na
uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na
viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria
lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria
Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta
jambo na Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara
ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki
ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na
wananchi wa mkoa mkoa huo(hawapo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa jarida la msaada wa kisheria katika Kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21,
2019.
Baadhi ya wataalam wa sheria na watoa huduma za kisheria wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada
wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya
Katiba na Sheria na taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktioba
21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati
walioketi) akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo, wataalam wa
Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na wawakilishi wa taasisi za watoa
huduma za kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria
Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa huduma ya msaada wa kisheria
ya Mama’s Hope Organisation for Legal Assistant (MHOLA),Bw. Saulo Malauri (kulia)
akipokea nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi
Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya
Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria,
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimkabidhi
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, nakala ya Jarida la Msaada wa
Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba
25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi
mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto)
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, nakala ya Jarida la
Msaada wa Kisheria, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria
Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa huduma ya msaada wa kisheria
ya Mama’s Hope Organisation for Legal Assistant (MHOLA),Bw. Saulo Malauri (kushoto)
akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, katika Kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21,
2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na
viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida la Msaada wa Kisheria
lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria
Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu
za wilaya ya Bariadi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mwakilishi wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Mary Mrio akitoa taarifa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya
Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe. Tano Mwera akitoa salamu,
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi, akitoa taarifa ya namna
wananchi wa Mkoa wa Simiyu walivyohudumiwa katika masuala ya kisheria wakati wa
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria,
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25,
2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi
mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa msaada wa huduma ya kisheria
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya viongozi na watoa msaada wa huduma ya kisheria
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), katika
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mwanasheria
kutoka Wizara ya Mambo ya ndani, akipokea cheti cha pongezi kwa kushiriki
kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyoadhimishwa
Kitaifa Katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21, 2019 cheti hicho kimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka katika kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) na viongozi wengine
wakishuhudia burudani kutoka kwa Eliza Band wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Wasanii wa Eliza Band ya mkoani Simiyu, wakitoa burudani
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na
viongozi wengine wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Afisa Uhusiano wa Shule ya Sheria Tanzania(LST), Bi.
Scholastica Njozi akipokea cheti cha pongezi kwa kushiriki kikamilifu katika
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyoadhimishwa Kitaifa Katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019
cheti hicho kimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika
kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 25, 2019.
0 comments:
Post a Comment