Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Oktoba 16, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka Mjini Bariadi Mkoani hapa, ambapo washiriki kutoka taasisi za
Umma na binafsi zaidi ya 100, mifuko ya uwezeshaji zaidi ya 40 na vikundi vya
kijamii (VICOBA) wanatarajiwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 15, 2019
Mjini Bariadi Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi
Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy ambao
ndiyo waandaaji amesema maonesho haya ni fursa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya
ziwa kujifunza huduma za mifuko ya uwezeshaji, taasisi za fedha na programu
mbalimbali.
“Maonesho haya yameanza Oktoba 14, 2019 na
yatafunguliwa rasmi Oktoba 16, 2019 na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na
yatahitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2019 na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa, nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waje wajionee
huduma mbalimbali za mifuko, taasisi na vikundi vya kijamii,” alisema Kessy.
Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural
Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo ametoa wito kwa wananchi kutembelea
banda lao kujua huduma zao, huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo kupitia mpango
mkakati wa miaka mitano ulioanza mwaka 2018 inatarajia kuzifikia familia
235,000 kwa kudhamini mikopo kiasi cha shilingi bilioni 210.6 .
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tanzania
tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi amesema benki hiyo kwa kushirikiana na NEEC
na PASS imetoa mikopo ya vikundi mbalimbali vya kijamii, vikundi rasmi na
visivyo rasmi, wafanyabiashara, hivyo ni vema wananchi wafike kwa wingi
kujionea fursa hizo ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naye mnufaika wa mikopo ya mifuko ya uwezeshaji, Bw.
Emmanuel Nyambi Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi kutoka Kahama, ametoa
wito kwa wananchi kufika katika maonesho hayo ili waweze kuona fursa za
upatikanaji wa mikopo kupitia mifuko, programu na taasisi mbalimbali za kifedha
huku akieleza kuwa hakuna urasimu katika utoaji wa mikopo.
“Natoa wito kwa wajasiriamali wadogo au vyama
mbalimbali, wafike kwenye maonesho haya waje wajifunze namna ya kupata mikopo
ya kuendeshea shughuli za kiuchumi, niwahakikishie hakuna urasimu kwenye mikopo,
tunaipata kwa wakati na Benki Kuu inadhamini kikubwa ni kuwa waaminifu
kurejesha mikopo,” alisema Nyambi.
Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu: “Mitaji
ni Chachu ya Kujenga Tanzania ya Viwanda”.
Afisa Biashara wa Taasisi
ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
wananchi Kiuchumi (NEEC) uliofanywa kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya
maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba,
2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa wa
Baraza laTaifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Edward Kessy
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo
Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya katika
maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba,
2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Meneja wa Benki ya Posta
Tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi (wa pili kushoto) akizungumza akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini
Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu
za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya
kijamii yanayoendelea ambayo yameanza
tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu.
Afisa kutoka Benki ya
Tanzania (BOT), Bi. Edista Njau (kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa
lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji
na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba,
2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanufaika wa
mikopo ya mitaji kutoka katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi wakitoa
ushuhuda kwa waandishi wa habari namna mifuko hiyo ilivyowasaidia kupata
mitaji, wanufaika hao wamehojiwa katika banda la Benki Kuu ya Tanzania, katika
maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba,
2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa
Mkoa wa Simiyu wakitembelea baadhi ya mabanda katika maonesho ya tatu ya mifuko
ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20
Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wataalamu
kutoka Mfuko wa Misitu nchini (TFS) wakiendelea na maandalizi ya banda lao kwa
ajili ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20
Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wajasiriamali
wakionesha bidhaa zao katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji
na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20
Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya zana za
kilimo zinazopatikana katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji
na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20
Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya waoneshaji
wakiwa katika maandalizi ya mabanda yao kwa ajili ya maandalizi rasmi ya
ufunguzi wa maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya
kifedha vya kijamii yanayoendelea katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20
Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment