Mkoa wa Simiyu umeanzisha mfumo rasmi
wa ukusanyaji takwimu na utunzaji wa kumbukumbu za wakulima wa pamba uitwao ‘Kilimo
Maendeleo’ utakaowawezesha wakulima kusajiliwa katika Vyama vya msingi vya
Ushirika (AMCOS), kuuza pamba yao kwa njia ya mtandao na kupata pembejeo zote
kutoka kwa wauzaji wa pembejeo.
Akizungumza katika uzinduzi wa
mafunzo juu ya mfumo huo, Meneja wa huduma za ugani kutoka GATSBY AFRICA, Bw.
Sunday Mtaki amesema Mfumo huo utaanza kutekelezwa katika AMCOS 24 zilizoteuliwa
kwa kuanzia.
“Katika utekelezaji wa mkakati wa
miaka mitano ya mkoa wa Simiyu katika zao la pamba, eneo la usajili wa wakulima
na matumizi ya TEHAMA kwenye kilimo ni muhimu sana, tumeileta kampuni inaitwa
LITENGA ambayo ina mtandao unaitwa Kilimo Maendeleo kazi yake ni kuwaunganisha
wakulima kupitia AMCOS na taarifa zote za mkulima zitapatikana kupitia simu za
mkononi,” alisema Mtaki.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema mfumo huo ni sehemu ya
utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa kilimo cha zao la pamba ulioandaliwa
na Mkoa kwa kushirikiana na wadau, kwa lengo la kuboresha kilimo cha pamba,
huku akiwataka Maafisa Kilimo na Maafisa ushirika kutimiza wajibu wao.
“Maafisa
Kilimo na Maafisa Ushirika timizeni wajibu wenu msisubiri mgombane na mtu hii
kazi ndiyo inayowapa heshima, Serikali ya Rais Magufuli imeweka mkakati wa
kuhakikisha zao la pamba linakuwa zao muhimili kwenye nchi yetu, ndiyo maana sisi
kama Mkoa tumeanza utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano wa kilimo cha zao la
pamba,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka ameongeza kuwa dhamira ya mkoa ni kufanya mapinduzi
katika kilimo cha pamba ili wakulima walime kilimo cha kisasa chenye tija na
kuwa na ushirika imara, ambapo amesema viongozi wa AMCOS wasio waaminifu
watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa
zao.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw.
Charles Madata amewaonya viongozi wa AMCOS kuwa waaminifu na kuhakikisha kila mmoja anakuwa na nidhamu ya fedha ili
mali za wakulima ziweze kuwa salama.
Kwa upande wake Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa
Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu amesema viongozi wote wasio waaminifu watachukuliwa
hatua, ambapo amebainisha kuwa takribani viongozi 107 wa AMCOS wilayani Maswa waliohusika
na ubadhilifu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa
ukaguzi.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema
kupitia mkakati wa miaka mitano ya mkoa wa Simiyu katika zao la pamba, mkoa wa huo
unatarajia kuongeza tija ya uzalishaji wa pamba kutoka kilo 200 kwa ekari hadi kufikia
kilo 600 hadi 1000 au zaidi kwa ekari.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo
ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo
wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi
wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu
ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika
Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.Oktoba 18, 2019.
Baadhi
ya wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi
wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu
ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika
Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za Chama, wakati wa
uuzinduzi wa mafunzo ya wakulima na
viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji
Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18,
2019 Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa neno la shukrani wakati wa
uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
(AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa
Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu,(SIMCU)Bw. Charles Madata
akiwasilisha hoja katika kikao cha uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi
wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na
Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi
wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu
ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika
Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi
wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu
ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika
Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment