Mkurugenzi wa shirika la reli nchini(TRC), Bw.Masanja Kadogosa
amesema kuwa shirika hilo limejipanga kuhakikisha linarahisiha huduma za
usafirishaji wa marobota ya pamba kwa njia ya reli lengo likiwa kuwapunguzia
gharama wenye viwanda vya kuchambua pamba.
Kadogosa amesema hayo mara baada ya kutembelea viwanda vya
kuchambua pamba vya Alliance kilichopo kata ya Kasoli na NGS katika wilaya ya
Bariadi mkoani Simiyu.
Pamoja na kupunguza gharama ameongeza kuwa njia hiyo ni salama
na ya uhakika hata kipindi cha mvua mzigo unafika kwa urahisi bila matatizo ya
aina yoyote huku akiongeza kuwa shirika la reli litaweka miundombinu
itakayowarahisishia usafirishaji huo.
"Tumejipanga kuweka miundombinu itayowasaidia mizigo
yakiwemo marobota ya pamba kusafirishwa kwa urahisi bila usumbufu wowote
niwaombe wafanyabiashara watumie fursa hii ya reli kufanya shughuli mbalimbali
zitakazowaingizia vipato hivyo kubadilisha maisha yao," alisema Kadogosa
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa ni vyema jamii ione
umuhimu wa kujenga viwanda vya nyama ili iwe iweze kusafirishwa nyama badala ya
Mifugo ambapo mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa yenye mifugo mingi
nchini .
Awali akimkaribisha mkurugenzi huyo mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema kumekuwepo na changamoto kubwa inayowakabili
wafanyabiashara hususan katika usafirishaji wa robota za pamba kwani
wanalazimika kutumia magari jambo linalopelekea kusafirisha mizigo michache kwa
gharama kubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amewasisitiza wafanyabiashara hao kuona haja ya
kutumia reli kwani huduma hiyo imesogezwa karibu na itawasaidia kuepukana na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama za usafirishaji na potevu wa
robota za pamba.
Aliongezea kuwa ni vyema ujenzi wa eneo la kuhifadhia
marobota ya pamba eneo la Malampaka ukazingatiwa huku akiongeza kuwa ujio
wa usafirishaji wa kupitia njia ya reli utawarahisishia na kuwapunguzia
gharama wenye viwanda vya kuchambua pamba.
Ibrahimu Kadudu ni mrajisi mkoa wa Simiyu amesema kuwa makisio
ya mkoa ilikuwa kuzalisha kilogramu milioni 180 na hadi kufikia septemba 22
2019, jumla ya pamba kilogramu milioni 148,836,601 zilikusanywa kwenye vyama
vya ushirika ,pamba iliyosafirishwa ni kilogramu milioni 116,391,208,
iliyolipiwa kati ya pamba iliyosafirishwa ni kilogramu milioni 85,166,453
, kilogramu milioni 31,106,816 zilisafirishwa bila kulipiwa huku kiasi
kilogramu milioni 32,445,393 zikiwa bado kwenye maghala na kwa baadhi ya
wakulima.
Kwa upande wake meneja wa kiwanda cha kuchambua pamba cha
Alliance ambaye pia ni katibu wa wanunuzi nchini Boaz Ogolla alisema kuwa
uzalishaji umeongezeka ambapo umesababisha uhitaji mkubwa wa magari ya
kusafirishia marobota ya pamba huku akitolea mfano kiwanda cha ni Alliance.
“ Kiwanda hiki kinazalisha robota 400 kwa siku na
zinazosafirishwa kwa siku ni robota 200 hivyo ujio wa usafirishaji kwa njia ya
reli utamaliza changamoto hiyo maana behewa moja lina uwezo wa kubeba maroboto
90 tofauti na gari lina uwezo wa kubeba marobota 25,” alisema Ogola.
Sambamba na hayo ameongeza kuwa usafirishaji huo utawapunguzia
gharama ambazo sio za lazima na kuwa awali changamoto ya usafirishaji
iliwalazimu kulipia mizigo kwa gharama kubwa ambapo kupitia reli watasafirisha
kwa gharama nafuu hivyo kutawawezesha na wao kupata faida kwenye biashara zao.
MWISHO
Mkurugenzi wa Alliance
Ginneries Limited Bw. Boaz Ogola(kulia) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Shirika
la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja Kadogosa(katikati) na viongozi wengine wa Mkoa
wa Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kasoli wilayani
Bariadi, Oktoba 05, 2019 kwa lengo la kujionea uzalishaji wa robota za
pamba ambazo shirika hilo linatarajia kusafirisha,
Mkurugenzi wa kiwanda
cha kuchambua pamba cha NGS, Njalu Silanga (wa tatu kulia akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Shirika
la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja Kadogosa(wan ne kulia) na viongozi wengine wa
Mkoa wa Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mjini Bariadi Oktoba
05, 2019 kwa lengo la kujionea
uzalishaji wa rmarobota ya pamba ambayo shirika hilo linatarajia kusafirisha.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja
Kadogosa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu nawa Kiwanda cha Alliance Ginneries
Limited kabla ya kuanza kukagua hali ya uzalishaji wa robota za pamba kiwandani
hapo, Oktoba 05, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Shirika
la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja Kadogosa katika Kiwanda cha Alliance Ginneries
Limited yenye lengo la kujionea hali ya uzalishaji wa marobota ya pamba
kiwandani hapo, Oktoba 05, 2019.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja
Kadogosa na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiangalia namna marobota
yanayozalishwa katika Kiwanda cha Alliance
Ginneries Limited wakati wa ziara ya kuona hali ya uzalishaji wa marobota ya
pamba kiwandani hapo, Oktoba 05, 2019.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika
la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja Kadogosa, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtakawakipewa maelezo na Mkurugenzi wa Alliance Ginneries Limited
Bw. Boaz Ogola juu ya namna pamba inavyochakatwa wakati wa ziara ya kuona hali
ya uzalishaji wa marobota ya pamba kiwandani hapo, Oktoba 05, 2019.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja
Kadogosa na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakitoka katika moja ya
maghala ya Kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS wakati wa ziara ya kuona hali ya uzalishaji wa
marobota ya pamba kiwandani hapo, Oktoba 05, 2019.
Mkurugenzi wa Alliance
Ginneries Limited Bw. Boaz Ogola(kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Shirika
la Reli nchini(TRC), Bw.Masanja Kadogosa(katikati) na viongozi wengine wa Mkoa
wa Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kasoli wilayani
Bariadi, Oktoba 05, 2019 kwa lengo la kujionea uzalishaji wa robota za
pamba ambazo shirika hilo linatarajia kusafirisha,
0 comments:
Post a Comment