Malipo
ya Wakulima wa zao la Pamba Mkoani Simiyu, katika msimu ujao yanatarajiwa
kufanyika kwa mfumo wa kielektroniki kupitia huduma ya T-PESA ya Shirika la
Mawasiliano Tanzania(TTCL).
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa
Wadau wa Pamba uliowahusisha viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wataalam
wa kilimo, viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS), kwa lengo la
kujadili juu ya malipo ya wakulima wa zao hilo kupitia huduma ya T-PESA
uliofanyika Oktoba 02, 2019 mjini
Bariadi.
Mtaka
amesema kuwa sambamba na mfumo wa ulipaji wa fedha za wakulima wa pamba kwa
njia ya Kielekroniki taarifa zote za kilimo zitapatikana kwa njia hiyo huku
akiongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuondokana na hasara katika vyama vya msingi
vya ushirika(AMCOS) iliyokuwa inasababishwa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu.
“Tumewaleta
hapa TTCL tunataka tufanye digital farming(kilimo kidigitali) malipo ya pamba, mambo
yote ya pamba na kilimo kwa ujumla yawe kwenye kiganja chako kwa sababu leo
hakuna nyumba ambayo haina simu; ni vizuri elimu hii viongozi wa AMCOS
muifikishe kwa wakulima ili wawe na
uelewa wa pamoja,” alisema Mtaka.
Akizungumza
katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL) Waziri Kinamba amesema mfumo huo mpya utaanza
kutumika katika msimu ujao na utawasaidia wakulima kupata fedha zao kwa
usalama, urahisi, kwa wakati na kupunguza matumizi yasiyofaa.
“Lengo
letu ni kutoa suluhu ya matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika vyama vya
msingi vya ushirika kama upotevu wa fedha, uporaji na tunaamini wakulima wakipata
pesa zao kidigitali itaondoa changamoto hizo na kuwafanya wakulima kuwa na
maisha bora kutokana na uchumi utakaoboreka baada ya mauzo watakayofanya
kupitia TTCL PESA,” alisema Kindamba.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Mkoa (SIMCU), Emmanuel
Mwelele amesema kuwa mfumo huu ni mzuri na unalenga kwasaidia wakulima kupata
fedha zao kwa usalama na akaahidi kuwa viongozi wa chama hicho watatoa elimu
kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) ili wakulima wote wawe na uelewa wa
pamoja.
Hadi
sasa mkoa wa Simiyu una wakulima wa pamba wapatao 314,000 na matarajio ya
uzalishaji katika msimu wa mwaka huu yalikuwa ni kufikia kilo milioni 180,
ambapo hadi sasa jumla ya kilo milioni 148 zimekusanywa kutoka kwa wakulima
kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) .
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa pamba
juu ya malipo ya wakulima wa pamba kupitia T-PESA mkoani Simiyu, uliofanyika Oktoba 02, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wa Serikali, Vyama vya
ushirika wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua
Mkutano Mkuu wa Wadau wa pamba juu ya malipo ya wakulima kwa kupitia T-PESA mkoani
Simiyu, uliofanyika Oktoba 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba akizungumza na Wadau wa pamba juu ya malipo
ya wakulima kupitia T-PESA Mkoani Simiyu, uliofanyika Oktoba 02, 2019 Mjini
Bariadi.
Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. George Mayunga akizungumza na Wadau wa pamba katika
Mkutano Mkuu wa Wadau wa pamba juu ya malipo ya wakulima kupitia T-PESA Mkoani
Simiyu, uliofanyika Oktoba 02, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi
wa Serikali, Vyama vya ushirika wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa pamba juu ya malipo ya
wakulima kupitia T-PESA Mkoani Simiyu, uliofanyika Oktoba 02, 2019 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua
Mkutano Mkuu wa Wadau wa pamba juu ya malipo ya wakulima kwa kupitia
T-PESA Mkoani Simiyu, uliofanyika Oktoba
02, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment