Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wameomba
Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini(TNMC) kupunguza gharama za ada ya leseni za uuguzi ambazo
wamedai kuwa ni kubwa na zinaathiri vipato vyao.
Ombi hilo limetolewa na Katibu wa Chama cha wauguzi Tanzania
Bara(TANNA) Bw. Sebastian Luziga wakati akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipofungua Kongamano la kisayansi na Mkutano wa 47
wa wauguzi kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Oktoba 01, 2019
Mjini Bariadi.
Luziga amesema awali ada hiyo kwa ngazi ya
astashahada ilikuwa 20,000/= stashahada
na shahada na shahada ya uzamili ilikuwa
shilingi 40,000/=, hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la ada ambapo
astashahada wanapaswa kulipa shilingi 40,000/=, stashada 60,000/=shahada 80,000
na shahada ya uzamili na uzamivu ni 120,000/=.
“Ongezeko hili ni kubwa na linaathiri sana kipato
cha wauguzi kwani hakuna uwiano kati ya
kupanda huko kwa ada na ongezeko la mshahara; kupitia Wizara ya Afya tunaomba
lishughulikiwe upya kwa kufuata utaratibu wa kushirikisha wadau,” alisema
Luziga
Akizungumza mara baada ya kupokea risala hiyo Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameahidi kulifikisha suala hilo pamoja na
mengine yaliyowasilishwa kwa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, huku akiwaomba
viongozi kulitafakari kwa upya ongezeko la ada wakizingatia hali halisi ya
mishahara ya wauguzi, kodi na makato na waone busara kama ipo haja na hoja ya
kuongeza ada hiyo.
“Suala hili ni hoja ya walio wengi, ninyi nyote
mmemuona Mhe. Rais akizungumzia kuondolewa kwa tozo nyingi zisizo na sababu
kwenye kilimo, mifugo, uvuvi; hata hili la kwenu linaweza kusababisha serikali
iwe na nia ya kufahamu mabaraza yake yote na tozo zao, nawaomba viongozi
mlitafakari muone kama ipo hoja na haja ya kuongeza gharama za ada,” alisema
Mtaka.
Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo
Dugange amesema mkoa unatambua kazi inayofanywa na wauguzi ya kutoa elimu kwa wajawazito nakuhamasisha
wajifungulie kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya, ambapo mwaka 2017 wanawake waliojifungulia kwenye vituo vya
afya ni asilimia 55 na mwaka 2018 ikapanda kufikia asilimia 70.
Naye Afisa Muuguzi kutoka Halmashauri ya Ubungo Bi.
Aliho Ngeregenza amesema wauguzi walio
wengi vipato vyao wanavyopata haviendani na gharama za leseni wanazolipia hivyo
ombi lao wapunguziwe gharama hizo
Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi
Tanzania Bara ambalo linahusisha wauguzi zaidi ya 800 litafanyika kwa muda wa
siku nne Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
MWISHO
Baadhi ya wauguzi
wakishangilia wakati Mgeni rasmi akiingia ukumbi wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba,
2019 ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao
unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akifungua
Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, kwa
niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Rais wa Chama cha
Wauguzi nchini, Bw. Paulo Magesa akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu
wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa siku nne
Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akifungua
Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, kwa
niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu
wa Chama cha Wauguzi nchini, Bw. Sebastian Luziga akisoma risala ya wanachama
kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Kongamano la kisayansi
na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi
wakiwa katika maandamano ya amani 01 Oktoba, 2019 kuelekea ukumbi wa Shule ya Sekondari Kumbukumbu ya Kusekwa mjini Bariadi, mahali ambapo Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, ambao unafanyika kwa
siku nne Mkoani Simiyu.
Wauguzi wakicheza
wakati muuguzi mwezao akitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao
unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa na
baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu(kushoto) na viongozi wa Chama cha Wauguzi
Tanzania bara wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kisayansi
na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi
wakiwa katika maandamano ya amani 01 Oktoba, 2019 kuelekea ukumbi wa Shule ya Sekondari Kumbukumbu ya Kusekwa mjini Bariadi, mahali ambapo Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, ambao unafanyika kwa
siku nne Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi
wakiwa katika maandamano ya amani 01 Oktoba, 2019 kuelekea ukumbi wa Shule ya Sekondari Kumbukumbu ya Kusekwa mjini Bariadi, mahali ambapo Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, ambao unafanyika kwa
siku nne Mkoani Simiyu.
Baadhi
ya wauguzi wakiwa wamsimama kuonesha heshima yao kwa ajili ya kumkaribisha Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kisayansi
na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na akizungumza na wauguzi wakati wa
Ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania
Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu.
Baadhi ya wauguzi
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akifungua
Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, kwa
niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa siku nne Mjini Bariadi Simiyu.
0 comments:
Post a Comment