Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi
kwa weledi na uadilifu na kuwaasa wasikimbie maeneo yao kazi badala yake wawe
chachu ya mabadiliko na utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo katika maeneo
yao
Dkt. Mwanjelwa ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Viongozi, watumishi
wa umma na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Oktoba 04, 2019 Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Dkt. Mwanjelwa amesema
watumishi wa umma wana maarifa hivyo
wanapaswa kutumia maarifa hayo kukabiliana na changamoto zinzzowakabili badala
ya kuhama maeneo ya kazi kwa kuwa Watanzania wanawahitaji kwa ajili ya kuwapa
huduma wanazostahili.
“Utumishi wa umma ni
fursa, utumishi wa umma ni fursa fanyeni kazi kwa weledi, uadilifu na ubunifu
maana dunia inabadiilika na ndiyo maana tunasisitiza waajiri watoe mafunzo ya
mara kwa mara ili watumishi waendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia,”
alisema Dkt. Mwanjelwa.
Katika hatua nyingine
Mwanjelwa anawaagiza waajiri kuwalipa kwa wakati fedha za mizigo wastaafu na
utoaji wa mafunzo kwa waajiriwa wapya.
Kwa upande wake rais
wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA Tumaini Nyamhokya anaomba
watumishi kupandishwa madaraja na wanapopandishwa wapate stahiki zao kwa wakati
ikiwemo mishahara.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amesema mbali na upandishwaji madaraja lakini kumekuwepo na
tatizo la kupandishwa mishahara ambapo alibainisha kuwa wapo maafisa elimu
wanne ambao bado hawajabadilishiwa mishahara yao inayoendana na vyeo vipya
hivyo akaomba Mhe. Naibu Waziri alifanyie kazi ili watumishi hao wapate haki
yao.
Ziara ya naibu waziri
,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Mary
Mwanjelwa Mkoani Simiyu imelenga kuzungumza na watendaji na
watumishi wa umma na kubadilishana uzoefu, kusikiliza kero na changamoto
zinazowakabili .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza na viongozi na
watumishi wa Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba
04, 2019 wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa (kushoto) akiteta jambo na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kikao chake na viongozi na
watumishi wa mkoa wa Simiyu Oktoba 04, 2019 wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi
mkoani hapa.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa mkoa wa Simiyu wakiwa
kwenye kikao na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa Oktoba 04, 2019 wakati akiwa kwenye ziara ya
kikazi mkoani hapa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa (kushoto) akiteta jambo na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakati wa kikao chake na viongozi
na watumishi wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 04, 2019
wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa.
Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi
Tanzania(TUCTA), akichangia hoja katika kikao cha Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa na viongozi
na watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 04, 2019
wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment