Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dkt Mary Mwanjelwa ametoa wito kwa wanafunzi wa kidato cha nne
mkoani Simiyu ambao walipata ufaulu hafifu katika mtihani wa
utimilifu (mock) walioko kambi ya kitaaluma ,kutumia fursa hiyo
kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.
Dkt Mwanjelwa ametoa wito huo alipowatembelea wanafunzi hao
katika kambi ya kitaaluma iliyopo chuo cha ualimu Bariadi mkoani hapa na
kuwasisitiza walimu mbali na kuwafundisha masomo ya darasani pia
wawafundishe namna ya kukabiliana na maisha baada ya kumaliza masomo ili
ambao hawatabahatika kuendelea na masomo ya juu waweze kujiajri na kuajiri
wengine.
Katika hatua nyingine Mwanjelwa amewataka wanafunzi kuitumia
fursa ya uwepo wao kambini kufanya kile kilichowapeleka, watumie muda mwingi
kujifunza na wajiepusha na mahusiano ya kimapenzi ambayo yatawasababishia
kushindwa kutimiza malengo yao ya baadaye.
“Maisha bila malengo sio maisha nini matarajio yako baada ya
kusoma na endepo hutafaulu ujue namna ya kujiajiri, tumieni fursa ya kuwa
hapa kuhakikisha mnasoma kwa bidii ishike sana elimu MUNGU hatakuacha, maisha
lazima myatafute ,myatolee jasho, ” alisema Mwajelwa
“Wanafunzi wa kike jitunzeni lindeni utu wenu asitokee mtu
akawadanganya mkashindwa kufikia ndoto zenu ninyi ni wa thamani kubwa kumbukeni
mbali na mimba kuna magonjwa, ” aliongeza Dkt Mwanjelwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini amesema kama mkoa wataendelea kusimamia fedha zote
zinazotolewa na serikali ya awamu ya tano za elimu bila malipo ili ziweze kuleta matokeo
chanya .
“Tunatamani kuona elimu bure inayotolewa na serikali inazaa
matunda tutapambana kuhakikisha vituo vya kutolea elimu vinakuwa na mazingira
bora na kama mlivyomuahidi kwa ziro hakuna na iwe hivyo, ”alisema Sagini
Awali baadhi ya wanafunzi waliopo kambini hapo
wamemshukuru mkuu wa mkoa huo kwa kuanzisha kambi za kitaaluma ambazo
wamesema zimewawezesha kuwa na uwelewa wa masomo mbalimbali kupitia walimu
mahiri hatua iliyowatoa kwenye daraja sifuri mpaka daraja la 111 kupitia mitihani
mbalimbali wanayopewa kambini hapo..
“Nilikuja kambini hapa nikiwa na division ziro tulivyofanya mtihani
wa mock ufaulu uliongezaka na nikikapata division 111 awali nilikuwa sijui kuandika
essay sasa hivi najua na nina uwezo wa
kuandika barua ya kuomba kazi ninachokuhakikishia mhe,pamoja na mkoa chini ya
mkuu wetu wa mkoa hatutawaangusha alisema ” Pendo Aguda kutoka shule ya
sekondari Old Maswa.
Akiwa kambini hapo Dkt. Mwanjelwa amekabidhi kwa niaba ya Mbunge
wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga kilo elfu moja za unga wa mahindi, kilo
mia tano za mchele na mafuta ndoo ishirini kwa ajili wanafunzi walioko kambini.
MWISHO
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt Mary Mwanjelwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa
wa Simiyu na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu walio katika kambi ya
kitaaluma wakati alipowatembela kambini hapo Oktoba 5, 2019
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt Mary Mwanjelwa
akikabidhi baadhi msaada wa chakula na mafuta kwa niaba ya Mbunge wa Itilima Njalu Silanga kwa wanafunzi
wa kidato cha nne walio katika kambi ya kitaaluma wakati alipowatembelea,
Oktoba 05, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa
kidato cha nne walio katika kambi ya kitaaluma Chuo cha Ualimu Bariadi wakimsikiliza Naibu Waziri
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt Mary
Mwanjelwa alipowatembelea Oktoba 05, 2019.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu walio katika kambi ya kitaalumakatika Chuo cha Ualimu Bariadi wakati alipowatembela kambini hapo Oktoba 5, 2019
0 comments:
Post a Comment