Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde amezindua rasmi Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo
yanafanyika Kitaifa
Mkoani
Simiyu na kutoa wito kwa viongozi wa Serikali kuwatumia wasajili wasaidizi na
watoa huduma za kisheria kutatua matatizo ya kisheria yanayowakabili wananchi.
Akizungumza
na wananchi Oktoba 21, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Mkoani Simyu Mavunde amesema matatizo ya kisheria yanashughulikiwa
kisheria na siyo kisiasa hivyo ni vema wakawashirikisha na wakaambatana nao
hata katika ziara zao ili waweze kutoa msaada wa kisheria kila unapohitajika.
“Yapo
mambo mengi sana ambayo ni ya kisheria wananchi mmekuwa mkikimbilia kwa
viongozi wa kisiasa, siasa ina sehemu yake inakoma inabaki sheria, wiki ya
msaada wa kisheria ni fursa ya kipekee kuelewa namna ya kushughulikia matatizo
yenu na mnaendelea kujifunza kuwa sheria inabaki kuwa sheria na utatuzi wake
unakuwa katika mfumo uliowekwa kisheria,” alisema Mavunde.
Awali
akitoa taarifa ya wiki ya msaada wa kisheria
Msajii wa Taasisi za watoa huduma za kisheria, B. Felistas Mushi amesema
lengo la kuwepo wa huduma ya msaada wa kisheria ni kuhakikisha haki inapatikana
kwa wananchi wasioweza kumudu gharama za wawakili”tunaamini kuwa baada ya
maadhimisho haya kutakuwa na mtazamo chanya katika kutatua matatizo ya wananchi
kisheria.”
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa
Simiyu wahakikishe katika ziara zao wanaambatana na wasajili wasaidizi na watoa
huduma za kisheria walio katika maeneo yao ili waweze kutatua na kutoa ushauri
wa namna ya kutatua matatizo yote kisheria.
Aidha,
amewataka viongozi na wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji, kata na wilaya
kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri mafunzo wanayopewa na wakayatafsiri kwa vitendo
katika utatuzi wa matatizo ya watu kwa haki na kushirikiana na viongozi wa Serikali,
taasisi na vyombo vyote vya maamuzi.
Katika
hatua nyingine Mtaka ameshauri kuwa ingekuwa vema pia kama masuala ya kisheria
yakajumuishwa katika baadhi ya masomo kama vile somo la Uraia ili kuendelea
kujenga uelewa wa pamoja juu ya namna ya kukabiliana na matatizo yote ya
kisheria.
Kwa
upande wake Mkuugenzi Mtendaji wa TANLAP, Bi. Christina Ruhinda ameiomba
Serikali na taasisi zake kushirikiana na watoa huduma za kisheria ili huduma
hizo ziwe endelevu na matatizo ya wananchi yaweze kufanyiwa kazi kwa haki.
Mkurugenzi
wa Miradi Shirika la Legal Services Facility, Bi. Scholastica Jullu amesema
shirika ilo litaendelea kufadhili mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi.
Maadhimisho
ya Wiki ya Msaada wa kisheria mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu “Msaada wa
Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”, wakati yakiadhimishwa kitaifa mkoani SIMIYU
yanapotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, 2019 pia yanaadhimishwa katika mikoa ya
Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kigoma,
Kilimanjaro,Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga.
MWISHO
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde (wa pili kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Bariadi
Mkoani Simiyu aliyefika katika banda la
Wizara ya Mambo ya Ndani kupata msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa
Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 yanayofanyika Uwanja
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25,
2019.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde (aliyesimama) akishuhudia wanasheria kutoka Kituo cha Haki za Binadamu
wakitoa huduma ya msaada wa kisheria kwa
mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, katika uzinduzi wa
Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba
25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde na viongozi wengine
kutembelea mabanda ya watoa huduma ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa
Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Baadhi ya wananchi ,
Wenyeviti na Wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya Vijiji na kata mkoani Simiyu,
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,
Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani ), katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25,
2019.
Baadhi ya viongozi na
watoa huduma ya msaada wa kisheria, wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (kulia)
akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, katika uzinduzi wa
Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria uliofanyika Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba
25, 2019.
Mtaalam kutoka Chama
cha Wanasheria Tanganyika(TLS), akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira, Mhe. Anthony Mavunde ( wa pili kulia) alipotembelea banda la Taasisi
hiyo, katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria
uliofanyika Oktoba 21, 2019 maadhimisho
haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Msajili wa Taasisi za
Watoa huduma ya msaada wa kisheria nchini, Bi. Felistas Mushi akiwasilisha
taarifa ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa
maadhimisho hayo Oktoba 21, 2019
maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde , akizungumza na baadhi ya wananchi , Wenyeviti na Wajumbe wa mabaraza
ya ardhi ya Vijiji na kata mkoani Simiyu,katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019
maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa kwanza mbele), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde(mwenye suti mbele) na viongozi wengine wakifurahia jambo mara baada ya kutembelea mabanda ya watoa huduma ya
msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa
kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati
walioketi), akiwa katika picha ya pamoja
baadhi ya viongozi wa Mkoa na watoa
huduma ya msaada wa kisheria mara baada ya uzinduzi wa Maonesho ya Wiki ya
Msaada wa kisheria, Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25,
2019.
Wakili wa Serikali
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Lilian Kilembe akitoa maelezo mbele ya
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde, alipotembelea banda la wizara katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019
maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani
Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Baadhi ya wananchi
wakipata huduma ya msaada wa kisheria katika mabanda mbalimbali ya watoa huduma
hiyo, katika Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria, maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mtaalam kutoka Chama
cha Wanasheria Tanganyika(TLS), akitoa taarifa ya chama hicho katika uzinduzi
wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria
Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mshauri wa Masuala ya
Kijinsia Bungeni, Bi Stella Manda kutoka UN WOMEN akiwasilisha taarifa ya Shirika
hilo kwa niaba ya Mkurugenzi, katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada
wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho
haya yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati
walioketi), akiwa katika picha ya pamoja
baadhi ya viongozi wa Mkoa na wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Simiyu, mara baada ya uzinduzi wa
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa kisheria, Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Baadhi ya viongozi na
watoa huduma ya msaada wa kisheria, wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Baadhi ya viongozi na
watoa huduma ya msaada wa kisheria, wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde na viongozi wengine
kutembelea mabanda ya watoa huduma ya msaada wa kisheria, katika uzinduzi wa
Maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria Oktoba 21, 2019 maadhimisho haya
yanafanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia
Oktoba 21- Oktoba 25, 2019.
0 comments:
Post a Comment