Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama ,
ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya uhikiki wa kina wa taasisi
ndogo za kifedha zinazotoa mikopo kwa wananchi na vikundi, ili kuzibaini
taasisi uchwara ambazo zimekuwa zikiwaibia watanzania badala ya
kuwanufaisha kiuchumi..
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo, katika kilele
cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha
vya Kijamii, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Oktoba
20, 2019.
“Ninajua baadhi ya taasisi ndogo
za fedha badala ya kuwasaidia wanachama
zimekuwa ziifanya kazi ya kuiba fedha za wanachama na kuwafanya wanachama warudi nyuma badala kusonga
mbele, agizo hili Baraza la Taifa la Uwezesheshaji wananchi Kiuchumi mlifuatilie
kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alisema Mhagama.
Katika hatua nyingine ameitaka mifuko/programu
za uwezeshaji wanachi kiuchumi kutoa mikopo kwa riba nafuu tofauti na taasisi
nyingine za kifedha, ambapo amebainisha kuwa takribani wajasiriamali 1,237,984 wamenufaika
na mikopo ya mifuko hiyo na hadi kufikia Juni 2019 jumla shilingi bilioni 388.4
zimetolewa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za kifedha kuhakikisha zinajibu
changamoto za wananchi huku akiwataka wananchi (wajasiriamali) walioshiriki maonesho
haya kutumia vema fursa walizoziona katika mifuko ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi ili wakuze uchumi wao.
Baadhi ya wanufaika wa mikopo wilaya ya Bariadi na Busega mkoani Simiyu
na Chato Mkoani Geita wamezishukuru Taasisi za kifedha zilizowakopesha
mitaji jambo ambalo limewasaidia kuimarsisha shughui zao za kiuchumi
wanazofanya ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.
“Naishukuru Benki ya AZANIA na wadhamini wangu Taasisi ya PASS kwa
kuniwezesha kupata mkopo wa shilingi milioni 20, kuanzia sasa nitalima kisasa na
nitaenda kuongeza miundombinu ya maji kwenye shamba langu maana nilikuwa nalima
ekari 10 kwa kumwagilia badala ya ekari 30 nilizo nazo,” alisema Elisha Malugu
kutoka wilayani Busega.
Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) Dkt. Festus Limbu
amesema NEEC inaendelea kufuatilia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
alilolitoa Juni 2019 la kila mkoa kuwa na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi,
lengo likiwa kuvifanya vituo hivyo kuwa kitovu cha uwezeshaji wananchi
kiuchumi.
Katibu
Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’ Issa amesema Maonesho haya yameshirikisha Taasisi
45, wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya, Pwani, Mwanza,
Tabora, Kagera , Mara, Singida na Dar es Salaam na kutoka nchi jirani za Burundi
na Kenya.
Maonesho ya tatu ya Mifuko/
Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii chini ya Kauli Mbiu, “Mitaji
ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda” yametanguliwa na maonesho
ya kwanza yaliyofanyika Mbeya mwaka 2017, ambapo ya pili yalifanyika mwaka 2018
jijini Dodoma.
MWISHO
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Bi. Efrancia Kabuga kutoka Wilaya ya
Kishapu mfano wa Hundi ya shilingi 50,000,000/=mkopo kutoka benki ya CRDB , ambao amefadhiliwa na
Taasisi ya PASS, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji
na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama ( katikati) akikata utepe kama ishara ya kuzindua Mpango mkakati wa
Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi
Kiuchumi(NEEC) kwa kipindi cha 2018/2019 mpaka 2022/2023, katika kilele cha
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya
Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi
Mkoani Simiyu(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na kulia
ni Mwenyekiti wa NEEC, Dkt. Festus Limbu
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akimsikiliza mwakilishi wa Kiwanda cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu asali inayozalshwa na kiongozi huyo wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/
Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.
Baadh ya viongozi na
watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo
pichani), katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji
na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa
Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), katika
kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha
vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Baraza la
Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) na wawakilishi wa mifuko ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/
Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akiangalia trekta alilokopeshwa, Bw. Donald Swai kutoka Bunamhala
wilayani Bariadi , trekta hilo ni mkopo aliopewa kwa ufadhili wa Mfuko wa
Pembejeo,trekta hilo ni mkopo kutoka Mfuko wa Pembejeo, katika kilele cha
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya
Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akimkabidhi kadi ya trekta Bw. Donald Swai kutoka Bunamhala wilayani
Bariadi , trekta hilo ni mkopo aliopewa kwa ufadhili wa Mfuko wa Pembejeo, katika
kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha
vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, wakuu
wa wilaya na baadhi ya viongozi wa Baraza
la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), katika kilele cha
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya
Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Nakala ya Mpango mkakati wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi
Kiuchumi(NEEC), kwa kipindi cha 2018/2019 mpaka 2022/2023Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/
Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Bw. Elisha Malugu kutoka Wilaya ya Busega mfano wa Hundi ya shilingi 20,000,000/=mkopo kutoka kutoka AZANIA benki chini ya ufadhili wa
Taasisi ya PASS, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji
na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa
Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji,Bi. Esther Mmbaga katika kilele cha
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya
Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi
Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano
Mwera, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na
Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwakilishi wa wafanyakazi wa Kiwanda cha
Chaki Maswa, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji
na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiwasilisha salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na
Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, katika kilele cha Maonesho
ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii,
Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani
Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, katika kilele cha
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya
Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi
Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akiwasikiliza baadhi ya watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati
alipotembelea mabanda ya maonesho, katika
kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha
vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye
ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na maafisa wa Taasisi ya PASS wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/
Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akihoji jambo katika Banda la Mfuko wa Misitu , wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/
Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama (wa sita kushoto) akicheza pamoja na Msanii Elizabeth Maliganya na
viongozi wengine, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji
na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa tatu kulia) akimsikiliza Afisa kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS), wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment