Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthnony Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa mkoani
hapa kwenda kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, kugombea
nafasi mbalimbali na hatimaye kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za
Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 ili
wapate viongozi waadilifu.
Mtaka
ametoa wito huo wakati akizungumza na
waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu,
baada ya ibada ya misa takatifu Oktoba 06, 2019 ambapo alibainisha kuwa
wananchi wanapaswa kuchagua viongozi waadilifu na wacahapakazi ambao watasimamia
vizuri fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo
yao.
“Kuanzia
tarehe nane mwezi huu uandikishaji unaanza nendeni mkajiandikishe na wote wenye
sifa chukueni fomu za kugombea nafasi mbalimbali na kujitokeza kupiga kura siku ya tarehe 24
Novemba ili mpate viongozi bora, tumekuwa tunapata migogoro mingi ya ardhi,
fedha za miradi kutotumika inavyotakiwa na moja ya sababu ni vongozi wasio
waadilifu, kajitokezeni mchague waadilifu, “ alisema.
Katika
hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu kusomesha watoto
wao na kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi
wa miundombinu ya elimu ikiwemo vyumba vya madarasa na mabweni ambayo
yatawapunguzia watoto wa kike kutembea mwendo mrefu.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro
Mwanhuzi wilayani Meatu, Paroko Robert Walwa amesemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa
kusisitiza umuhimu wa kupenda elimu jambo ambalo amesema hata Biblia Takatifu
imesisitiza kuishika elimu maana ndiyo chimbuko la imani, hivyo ni vema wananchi wakazingatia elimu ili imani
zao ziimarishwe.
Naye
mmoja wa waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi aliyejitambulisha
kwa jina moja la Jennifer amesema wananchi wanamshukuru Mkuu wa Mkoa kwa
jitihada anazozifanya katika mkoa ambazo zimekusudia kuinua mkoa kielimu na
akabainisha kuwa watashirikiana na Serikali katika kuhakikisha malengo ya
kuinua sekta ya Elimu yanatimia ikiwemo kuongeza ufaulu.
Kuhusu
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Bi. Jeniffer amesema atahakikisha anajiandikisha
na kupiga kura siku ikifika ili aweze kutumia vema haki yake ya msingi ya
kuchagua kiongozi anayemtaka na si wa kuchaguliwa na watu wengine.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu, baada ya ibada ya misa takatifu Oktoba
06, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania(TRC), Bw. Masanja Kadogosa(wa pili
kulia) pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Serikali wakiwa katika ibada ya misa takatifu Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu 06, 2019 pamoja na
waumini wa kanisa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania(TRC), Bw. Masanja Kadogosa(wa pili
kulia) pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Serikali wakiwa katika ibada ya misa takatifu Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu 06, 2019 pamoja na
waumini wa kanisa hilo.
Baadhi ya waumini wa
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu wakifuatilia
ibada ya misa takatifu hapo jana Oktoba 06, 2019 ibada ambayo pia ilihudhuriwa
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Reli Tanzania(TRC), Bw. Masanja Kadogosa(hawapo pichani).
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania(TRC), Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waumini wa
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu, baada ya
ibada ya misa takatifu Oktoba 06, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Komredi. Enock Yakobo akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki
Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu, baada ya ibada ya misa
takatifu Oktoba 06, 2019 (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka .
Paroko wa Parokia ya
Mtakatifu Pertro Mjini Mwanhuzi Meatu, Robert Walwa na Paroko wa Parokia ya
Mtakatifu Yohana ya Mjini Bariadi, Kizito Victor wakiongoza ibada ya misa takatifu katika
Parokia ya Mtakatifu Pertro Mjini Mwanhuzi Meatu, jana Oktoba 06, 2019.
Baadhi ya waumini wa
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu, Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania(TRC), Bw. Masanja Kadogosa(wa pili kulia)wakifuatilia ibada ya misa takatifu
hapo jana Oktoba 06, 2019 ibada ambayo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania(TRC),
Bw. Masanja Kadogosa(hawapo pichani).
0 comments:
Post a Comment