Mamia ya
wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Mwanza na Dar es Salaam
wameshiriki katika mazishi ya mtoto wa Mkuu wa Majeshi marehemu Nelson Mabeyo aliyekuwa rubani wa
ndege ya Shirika la Auric Air, ambaye alifariki Septemba 23, 2019 kwa ajali ya
ndege iliyotokea katika Uwanja mdogo wa Seronera uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
mkoani Mara.
Mazishi
hayo yamefanyika Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanzakona wilaya ya
Busega Mkoani Simiyu, ambapo yalitanguliwa na ibada ya mazishi iliyofanyika
katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yuda Tadei lililipo kijijini hapo ambapo ni
nyumbani kwao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.
Akihubiri
wakati wa ibada ya mazishi, Askofu Michael Msonganzila, Jimbo Katoliki Musoma
amewasihi waombolezaji wote kuendelea kuifariji na kuiombea familia ya Mkuu wa
Majeshi ili wapokee msiba huo kwa jicho la imani, masikio ya imani na kama
mpango wa Mungu.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akitoa salamu za
serikali amesema “marehemu Nelson Mabeyo
alikuwa kijana mcheshi na mchapakazi leo
hatuko naye tena nitoe pole kwa familia ya Jenerali Mabeyo, sisi ni wa Mwenyezi
Mungu na kwake tutarejea niwaombe tuendelee kuwaombea katika kipindi hiki
kigumu Mwenyezi Mungu awape ustahimilivu.”
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Simiyu na
wakuu wa mikoa ametoa pole kwa familia ya Mkuu wa Majeshi na kumshukuru kwa
namna Mkuu alivyowaunganisha watu wa
Masanza, Busega na Simiyu katika masuala mbalimbali ya ikiwemo Ujenzi wa Kanisa ambalo ibada ya
mazishi ya marehemu Nelson imefanyika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenrali Venance Mabeyo amewashukuru watu wote walioshirikiana na familia yake
tangu msiba wa mwanaye Nelson ulipotokea , ambapo amesema kama familia
hawauchukulii msiba huo kama adhabu bali makusudi ya Mungu mwenyewe kwa mtoto
wao .
Mazishi
ya marehemu Nelson Mabeyo yalihudhuriwa
na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa
dini, viongozi na Maafisa wa JWTZ walioko kazini na wastaafu, mawaziri na
manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa Taasisi, viongozi wa Vyombo vya
Usalama, wabunge, Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Kagera, Kigoma,
Mwanza na Dar es salaam , kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu na
wakuu wa wilaya.
MWISHO
Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na mkewe Tina Mabeyo wakiweka shada la maua katika kaburi la mtoto
wao Rubani Nelson Mabeyo ambaye
alifariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya
Taifa ya Serengeti Mkoani Mara ; ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika
Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiweka shada la maua katika
Kaburi la Rubani Nelson Mabeyo mtoto wa
Mkuu wa Majeshi ambaye alifariki katika
ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani
Mara ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani
Busega Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) na wakuu wa mikoa ya Mwanza, Mara,
Shinyanga, Kagera, Kigoma na Dar es Salaam wakiweka shada la maua katika Kaburi
la Rubani Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa
Majeshi ambaye alifariki katika ajali ya
ndege iliyotokea Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya
Serengeti Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha
Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
Baadhi ya askari wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiweka Jeneza lenye mwili wa mtoto wa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo
aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera Mkoani Mara ; ambaye
amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani
Simiyu.
Maaskofu wa Katoliki kutoka Majimbo ya Mara na Geita wakiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo aliyefariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya mazishi ya mtoto wa Mkuu wa majeshi
Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo aliyefariki katika ajali ya ndege Septemba
23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, ambaye
amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani
Simiyu.
Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi(mwenye miwani katikati) akizungumza
jambo na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali mara baada ya ibada ya mazishi
ya mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson
Mabeyo aliyefariki katika ajali ya ndege
Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara,
ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega
Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment