Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kutoka katika Halmashauri sita za Mkoa wa
Simiyu wameapishwa Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi, ambapo Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka wazingatie sheria, kanuni,
taratibu na miongozo katika uchaguzi huo ili kuepusha malalamiko yasiyo ya
lazima.
Sagini amesema wasimamizi
hao wanapaswa kutambua kuwa wamepewa
jukumu zito ambalo linahitaji umakini wa hali ya juu na utulivu wa akili, hivyo
ni vema wakasoma na kuzipitia tena sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi wa
Serikali za Mitaa walizopewa ili wazielewe na waweze kufanya kazi bila
kubabaika.
“Kumbukeni kuwa Uchaguzi
huu unaweka msingi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hivyo ni imani
yangu kuwa kila mmoja wenu atakahakikisha anazingatia sheria, kanuni,miongozo
na taratibu zilizotolewa ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima; matarajio
yangu ni kwamba mtaishi viapo mlivyoapa leo” alisema Sagini.
Aidha, Sagini
amewataka wasimamizi hao kujiepusha na ushabiki wa kisiasa kwa kuwa wao kama
wasimamizi ni waamuzi, hivyo hawapaswi kwa namna yoyote kujihusisha na masuala
ya ushabiki wa vyama vya kisiasa, ili waaminiwe kuwa wanaweza kutoa haki; watakaobainika
kujihusisha na itikadi za kisiasa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Akizungumza mara baada
ya kuwaapisha wasimamizi hao, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio amewataka wasimamizi hao kuishi viapo vyao na
kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa uadilifu na kwa mujibu wa sheria kwa
sababu watakapokiuka sheria , kanuni na taratibu wataiingiza serikali kwenye
gharama.
Kwa upande wao wasimamizi
wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Simiyu mwaka 2019 wamesema
watahakikisha wanatekeleza wajibu na majukumu waliyopewa kwa mujibu wa sheria,
kanuni, taratibu na miongozo kama walivyoelekezwa.
“Tunashukuru kwa
kuaminiwa katika jukumu hili nyeti la Kitaifa, tunaamini kama tulivyoelekezwa
kama wasimamizi tutasimamia yale tunayopaswa tutafanye kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu na tutaviishi viapo vyetu tulivyoapa siku ya leo na kutimiza
wajibu wetu kama watumishi wa Umma” alisema Wilbert Siogopi msimamizi wa
Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
“Tunaahidi kwamba tutakitekeleza
kiapo tulichoapa leo, tunafahamu kuwa kazi hii ngumu lakini kama mlivyotuasa
tukiamua kwa dhati kabisa tukapitia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya
uchaguzi tutafanya kazi inayotarajiwa” alisema Bi . Amina Mbwambo msimamizi wa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 nchini kote ambapo katika Mkoa wa Simiyu
utahusisha Vijiji 470, Mitaa 92 na
Vitongoji 2652.
MWISHO
Msimamizi wa Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Eng. Wilbert
Siogopi Makala akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa
Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo
limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Msimamizi wa Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bibi. Pelagia Daudi Sogoti akila kiapo mbele ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary
Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na
kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini,(kushoto
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa chaguzi wa Serikali za
Mitaa baada ya wasimimizi hao kuapishwa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa
Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo
limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Bi.Amina Mbwambo msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuapishwa ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto),
zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto) akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mara baada ya kuwaapisha Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na
kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanna Sagini
akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya
kuwaapisha Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Joyce Thomas Ndunguru akila kiapo mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary
Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na
kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck
Humbe akitoa neno kwa wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao
waliapiswa Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi
na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa
Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bibi. Mwanaishamu Nassoro Shemagembe akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi
ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na
viongozi wakifuatlia halfa tya kuapisha wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za
Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019
Mjini Bariadi na Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na
kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini

Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Gidion John Burton akila kiapo mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary
Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na
kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri
ya Wilaya ya Itilima, Bibi. Bi . Amina Mbwambo akila kiapo mbele ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary
Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na
kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
0 comments:
Post a Comment