Uongozi wa Mkoa
wa Simiyu umebaini Ubadhilifu wa kiasi cha
shilingi 55,580,000/= ambazo ni sehemu ya mkopo uliotolewa na Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urasimishaji
wa makazi Viwanja 3700 katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Busega
uliofanywa na Watumishi wanne wa Halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw.
Jumanne Sagini wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi huo katika kikao cha Baraza
Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 Busega Septemba 06,2019
Nyashimo Busega.
Sagini amewataja watumishi waliohusika katika
ubadhilifu huo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri, Anderson Njiginya, Mkuu wa
Idara ya Ardhi, Magesa Magesa, msimamizi wa mradi Raymond Mahendeka na mhasibu
wa mradi,Augustina Kitau na kuwataka kurejesha fedha hizo mara moja na kushauri
mamlaka zao za nidhamu kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria
Sagini ameongeza kuwa timu ya uchunguzi imebaini
mapungufu mbalimbali katika matumizi ya fedha hizo ikiwa ni pamoja na ukikwaji
wa sheria, kanuni na taratibu za fedha, ukiukwaji wa masharti ya mkataba,
ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu za manunuzi ya Umma, udanganyifu na
uzembe na usimamizi dhaifu wa Mradi.
“Kutokana na mapungufu yaliyobainishwa katika
uchunguzi huu Uongozi wa mkoa unaelekeza watumishi waliohusika warejeshe fedha
hizo haraka ili mradi utekelezwe kama ilivyokusudiwa na tunashauri mamlaka za
nidhamu zichukue hatua stahiki kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria na
taratibu za Utumishi wa Umma,” alisema Sagini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe.
Vumi Magoti amewashukuru viongozi wa Mkoa kutuma wataalam wa Mkoa kufanya
uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi na kumuagiza Mkurugenzi kuanzisha
utaratibu wa kuwachukulia hatua watumishi waliohusika walio chini ya mamlaka yake kama viongozi wa mkoa walivyoelekeza.
Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe, Goodluck Nkalango amesema
madiwani wa Halmashauri ya Busega wakiwemo wajumbe wa kamati inayoshughulikia
masuala ya ardhi hawakushirikishwa katika utekelelezaji wa mradi wa
urasimishaji, makazi jambo ambalo lilipelekea wananchi kutokuwa na taarifa
sahihi za mradi ikiwemo utaratibu wa kuchangia gharama za upimaji.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu,
Bw. Alex Mpemba amesema TAKUKURU imepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi na
itaanza kuifanyia kazi mara moja kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai kwa
waliohusika.
“Tumeipokea taarifa ya uchunguzi kupitia kikao cha
baraza la dharura na kwa sababu wenzetu wa ukaguzi wamemaliza kazi yao na sisi
tutaanzia pale walipoishia kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai,” alisema
Mpemba.
Halmashauri ya Wilaya ya Busega ilipokea mkopo wa
shilingi 100,000,000/=kutoka Wizara ya Ardhi kutekeleza Mradi wa urasimishaji
wa makazi viwanja 3700 katika kata za Mwamanyili, Mkula, Kiloleli na Lamadi;
kwa mujibu wa taarifa ya Uchunguzi hadi kufikia Septemba 06, 2019 utekelezaji wa mradi ulikuwa
umefikia asilimi 8.5 na fedha zilizokuwa zimetumika ni asilimia 98.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi na madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani,
Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya
fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akifungua kikao cha
Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika
Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya
fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akizungumza kabla ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Vumi Magoti kufungua kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za
mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Madiwani wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za
mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Baadhi ya watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za
mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akiteta jambo na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za
mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Baadhi ya viongozi
wakifuatilia kikao cha Baraza Maalum la
madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya
uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Diwani wa Kata ya
Mkula, Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za
mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Diwani wa Kata ya
Mkula, Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za
mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
0 comments:
Post a Comment