Kuelekea katika Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu elimu ya Msingi
Darasa la saba Septemba 11-12, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewaonya wanafunzi wa darasa la
saba mkoani hapa kujiepusha na udanganyifu
katika mtihani huo badala yake wazingatie yale waliyofundishwa na kufanya
mtihani huo kwa utulivu na
kujiamini.
Mtaka ameyasema hayo Septemba 09, 2019 wakati
akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09,
2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi, kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu,
kwa lengo la kuwatakia heri katika mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya kuanzia
Septemba 11-12, 2019.
Mtaka amesema anaamini walimu
wamefanya kazi yao vizuri ya kuwafundisha na kuwaandaa wanafunzi hao hivyo ni vema wakafanya mtihani huo
wakiwa na ujasiri huku wakipuuza taarifa zozote za kuwepo kwa majibu ya
mitihani mahali popote.
“Ninawatakia kila la heri kwenye
mtihani wenu, nashukuru kwa kazi nzuri iliyofanywa na walimu katika
kuwafundisha na kuwaandaa kwa kutoa majaribio ya mara kwa mara, kambi kambi za
kitaaluma; niwaombe mkaufanye mtihani huu kwa utulivu na ujasiri; asiwadanganye
mtu kuwa kuna majibu ya mtihani au mtihani umevuja sehemu fuulani, mkazingatie
mlichofundishwa” alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka
amewashukuru walimu kwa namna wanavyojituma katika kuwafundisha wanafunzi na
kutoa wito kwa walimu hao kuanzisha madarasa ya maandalizi ya kidato cha kwanza
(pre- form one) kwa wanafunzi hao wanaohitimu
ili wasaidie kuwaandaa wanafunzi hao na
masomo ya kidato cha kwanza na waweze kupata kipato cha ziada kupitia
malipo yatakayotolewa na wazazi watakaokuwa tayari kugharamia masomo hayo.
Kwa upande wake Afisa Taaluma Mkoa wa
Simiyu , Mwl. Onesmo Simime amesema Mkoa wa Simiyu uliweka mikakati mbalimbali
ya maandalizi ya wanafunzi wa darasa la saba ikiwemo walimu kumaliza mada zote
mwezi Juni 2019 na kuwepo kwa kambi za kitaaluma kwa kila shule, hivyo wanafunzi wameandaliwa vizuri na kwa
mikakati hiyo matarajio ya mkoa ni ufaulu kuongezeka zaidi ya mwaka jana 2018.
Akizungumza
kwa niaba ya walimu, Mwalimu Beatrice Ernest kutoka Shule ya Msingi Mwabasabi
amesema wana uhakika na maandalizi waliyofanya kwa wanafunzi wao hivyo ufaulu utaongezeka, huku akimshukuru Mkuu wa
Mkoa kwa kuwaruhusu kuanzisha vituo vya ‘pre-form one’ na kuahidi kuwa walimu
watajiunga kuanzisha madarasa hayo ili kuboresha taaluma ya wanafunzi wao na
kuboresha vipato vyao.
Nao baadhi
ya wanafunzi wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamesema wamejiandaa vizuri na
wamejipanga kufanya vizuri ili waweze
kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na kujiunga na elimu ya sekondari na hatimaye kuendelea
na elimu juu ili waweze kufikia ndoto zao.
“Mimi na
wenzangu wote tumejiandaa vizuri nina uhakika tutafanya vizuri na wote tutaenda
sekondari, ushauri tuliopewa na Mkuu wa Mkoa tutauzingatia naamini tutashinda
tu” Eric Malimi kutoka Shule ya Msingi Lamadi.
“Sisi
tumejiandaa vizuri na tunaweza kuendelea mbali kimasomo, tunamshukuru Mkuu wa
Mkoa kwa kutupa mawaidha na tutayatekeleza ili tuweze kufaulu mtihani wa Taifa
na tufikie tunapotaka” alisema Glorymary
Samwel kutoka Shule ya Msingi Itongo.
Mkoa wa
Simiyu una jumla ya wanafunzi 29,248 wa
darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa Taifa Septemba 11-12, mwaka huu,
ambao kati yao wavulana ni 13, 594 na wasichana 15.654.
MWISHO
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika kata ya Lamadi
wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiwa wamenyoosha mikono yao kama ishara ya kuwa
tayari kujibu swali waliloulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao Septemba 09, 2019 katika Shule ya
Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia
heri katika mtihani wa Taifa wanaotarajia
kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi
wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09,
2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu,
kwa lengo la kuwatakia heri katika mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia
Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika kata ya Lamadi
wilayani Busega Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao Septemba 09, 2019 katika
Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la
kuwatakia heri katika mtihani wa Taifa
wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya walimu kutoka katika shule ya msingi Lamadi,
Mwabasabi na Itongo katika Kata ya Lamadi wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza na
wanafunzi kutoka katika shule hizo kw naiaba ya wenzao wa mkoa wa Simiyu, kwa
lengo la kuwatakia heri katika mtihani
wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson
Njiginya akitoa taarifa ya Ufaulu ya wanafunzi wa darasa la saba katika Halmashauri
wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba
kata ya Lamadi Septemba 09, 2019 katika
Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la
kuwatakia heri katika mtihani wa Taifa
wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya walimu kutoka katika shule ya msingi Lamadi,
Mwabasabi na Itongo katika Kata ya Lamadi wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza na
wanafunzi kutoka katika shule hizo kw naiaba ya wenzao wa mkoa wa Simiyu, kwa
lengo la kuwatakia heri katika mtihani
wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi
wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09,
2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu,
kwa lengo la kuwatakia heri katika mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia
Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika kata ya Lamadi
wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiwa wamenyoosha mikono yao kama ishara ya kuwa
tayari kujibu swali waliloulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao Septemba 09, 2019 katika Shule ya
Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia
heri katika mtihani wa Taifa wanaotarajia
kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019
Baadhi ya viongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakiwa katika mkutano wa mkuu wa mkoa na wanafunzi wa darasa la saba kata ya Lamadi wilayani humo, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, Bw. Anderson Njiginya
0 comments:
Post a Comment