Shirika
lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home limetoa msaada wa vitendea kazi kwa
wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa
lengo la kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kutoa elimu kwa jamii juu
mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kupitia mradi wa “BADILISHA TABIA TOKOMEZA MALARIA,” Mkoani Simiyu.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi hivyo Meneja Miradi wa Amani Girls
Home, Bw. Revocatus Sono, amevitaja
vifaa hivyo kuwa ni baiskeli 46, makoti ya
mvua 46, mabuti ya mvua 46, fulana na
vitini vya kutolea elimu kwa jamii vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi
milioni tisa, ambavyo vimetolewa kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 46 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega
na Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Nao
wahudumu wa afya ngazi ya jamii wameishukuru
Taasisi ya Amani Girls Home kwa kutoa msaada
wa vitendea kazi ambavyo wamesema vitawarahisihsia kazi na kuwawezesha kuwafikia
wananchi wengi na kutoa elimu iliyokusudiwa kwa jamii ili kufikia lengo la
kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria mkoani Simiyu.
“Tunaishukuru
Amani Girls Home kwa kutoa vitendea kazi hivi, awali tulianza kazi tukiwa
hatuna vifaa ilikuwa ni changamoto kubwa kwa kuwa tuna mitaa mikubwa na
hatukuweza kuwafikia walengwa wote, leo tumekabidhiwa vifaa zikiwemo baiskeli
naamini vitatusaidia kufanya kazi yetu kwa wepesi katika kuifikia jamii” alisema
Abadi James Mhudumu wa afya ngazi ya Jamii Kata ya Malambo Bariadi Mjini.
Mratibu
wa Mpango wa Kudhibiti Malaria Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mugune Maeka amewataka wahudumu
wa afya ngazi ya jamii kuhakikisha wagonjwa wa malaria watakaowaibua katika jamii
wanafikishwa katika vituo vya kutolea huduma, ili wapate matibabu sahihi na kwa
wakati lengo likiwa ni kupunguza maambukizi ya malaria kutoka asilimia sita ya
sasa na hatimaye kufuta kabisa ugonjwa
wa malaria.
Awali
akizungumza na wahudumu hao, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Bw.
Melkizedeck Humbe amewataka kutumia vitendea kazi walivyopewa kwa malengo yaliyokusudiwa, huku
akiahidi kuwa Serikali itaweka utaratibu wa kuendeleza juhudi za wadau wa afya
katika mapambano dhidi ya malaria ili ugonjwa wa malaria ubaki kuwa historia
katika mkoa wa Simiyu.
Katika
hatua nyingine Humbe amewataka wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoa elimu kwa
jamii kutumia vituo vya kutolea huduma za Afya kupata matibabu kila wanapoona dalili za
ugonjwa badala ya kwenda kwa waganga wa jadi ili waweze kupata tiba sahihi kwa
wakati sahihi.
Amesema
Serikali imejenga vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo mbalimbali
ikiwemo zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
zinaendelea kujengwa, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa umuhimu wa kutumia vituo
hivyo kupata huduma za tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Malaria badala ya kwenda kwa waganga wa jadi.
“Hospitali
za wilaya zinajengwa, vituo vya afya vimejengwa, zahanati zimejengwa
kawaelimisheni watu watumie vituo vya kutolea huduma za afya ajili ya kwenda
kupima afya na kupata matibabu sahihi kwa wakati wanapokuwa wagonjwa, badala ya
kwenda kwa waganga wa jadi ili tutokomeze kabisa malaria kwenye mkoa wetu”
alisema Humbe.
MWISHO
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akiwakabidhi wahudumu wa
afya ngazi ya jamii baiskeli kwa niaba ya wenzao ambao wote wamepewa baiskeli
na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home ambavyo vimekabidhiwa kwao Septemba 04, Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akizungumza na wahudumu wa
afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya
ya Bariadi na Busega wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi zikiwemo
baiskeli vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home na
kukabidhiwa Septemba 04, Mjini Bariadi.
Baadhi ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Busega wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe(hayupo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi zikiwemo baiskeli vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa kwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akimkabidhi mmoja wa wahudumu
wa afya ngazi ya jamii fulana kwa niaba ya wenzake 45 ambao wote wamepewa
baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani
Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa
wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akimkabidhi mmoja wa wahudumu
wa afya ngazi ya jamii kitini cha kutolea elimu kwa jamii kwa niaba ya wenzake
45 ambao wote wamepewa baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la
Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya
malaria na kukabidhiwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akimkabidhi mmoja wa wahudumu
wa afya ngazi ya jamii kitini cha kutolea elimu kwa jamii kwa niaba ya wenzake
45 ambao wote wamepewa baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la
Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya
malaria na kukabidhiwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.
Mratibu
wa Mpango wa Kudhibiti Malaria Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mugune Maeka akitoa taarifa
ya hali ya malaria mkoani Simiyu, wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi vya
wahudumu wa afya ngazi ya jamii zikiwemo
baiskeli na makoti ya mvua, yaliyofanyika Septemba 04, Mjini Bariadi.
Baadhi
ya baiskeli zilizotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home Wahudumu
wa Afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Shirika lisilo
la Kiserikali la Amani Girls Home, Septemba
04, Mjini Bariadi
Baadhi
ya baiskeli zilizotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home Wahudumu
wa Afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Shirika lisilo
la Kiserikali la Amani Girls Home, Septemba
04, Mjini Bariadi.
Baadhi
ya vitendea kazi vilivyotolewa pamoja na baiskeli na Shirika lisilo la
Kiserikali la Amani Girls Home kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri
ya Mji wa Bariadi na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home, Septemba 04, Mjini Bariadi kwa ajili ya kutoa
elimu juu ya vita dhidi ya malaria .
Baadhi
ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii
kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na
Busega wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck
Humbe(hayupo pichani) wakati wa hafla ya
makabidhiano ya vitendea kazi zikiwemo baiskeli vilivyotolewa na Shirika lisilo
la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya
malaria na kukabidhiwa kwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi
0 comments:
Post a Comment